Acheni wenye elimu zao walipwe mamilioni

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,697
Unakuta watu wamekaa wanafurahia eti haiwezekani mtu apokee mil.40 halafu mwalimu laki tatu , ukimuuliza huyo mtumishi ametumia gharama gani kupata taaluma yake utakuta kalipa ada mil. Moja na laki tano kwa mwaka mwenzako unayemlalamikia kalipa ada mil.

Hamsini kwa mwaka tena kasoma oxford, havard nk. Vyuo vinavyotambulika ulimwenguni , Popote anaajirika ulimwenguni. Ukimpa organization aiendeshe inakuwa efficiently and effectively. Mtu unamkuta kasoma open univers. Kutwa anasoma past paper hiyo competence ataitoa wapi .

Acheni wivu.
 
Inamana huiamini elimu ya Open University? Then unafahamu competence inapimwaje?
 

millioni 40...sio katika nchi masikini kama tanzania
 
watanzania tuna wivu sana. hata mtu akipokea lak 3 badala ya milion 40 wewe mwana nchi wa kipato cha chini itakusaidia nini? mtu anaepokea mil 40 ni wazi ana ujuzi na kazi yake ndo mana analipwa kiasi kikubwa hivo. hata ukimlipa lak 3 ataenda kuomba kaz nchi nyingine, afu hapa kwetu kazi ambazo anaweza kufanya mtanzania atapewa mzungu au mchina kisa wasomi wetu wamekimbia nchi. tz nchi ya ajabu sana sijawahi kuona serekali yoyote duniani inafurahi raia wao kuwa maskini. badala ya kusema utasaidia maskini kuwa tajiri. unasema utasaidia tajiri kua maskini. wakati china na marekani wanashindana nani ana ma billionaire wengi sisi eti tunakomaa na hawa wa milion 40
 
Unafanya kazi EWURA au TAMESA na unalipwa mil 40, hizo Taasisi zinatengeneza faida kiasi gani ?
Taasisi za Huduma wanataka kushinda mishahara na Ma co wa Voda na Airtel !
 
Leo nimekubal post yako
 
TZS 15,000,000.00
-free house
-usafiri
-matibabu
-Posho kiasi
Hataki aende UN akaombe kazi huyo hatufai kuwa mtumishi wa Umma tena kwa nchi ambayo watu wanashindia mlo mmoja kwa siku
hahahaa.aya bhana kwahio kwa mawazo yako watu wasipolipwa hzo pesa ndo mlo mmoja kwa cku utaisha,,,watu wanalipwa kulingana na how much they produce..c tanzania pekee mku ni nchi zote
 
Mkuu umeongea ukweli lakini uliposema juu ya OUT tu watu watakurarua. Maana huko hata mawaziri walio na diploma ndio walikimbilia. Bado wabunge, walimu, maofisa mbalimbali nk.
 
Hapa tujadili concepts mbili kuu. 1.) Leadership: je? ni kweli kwamba kama umesoma Harvard, basi wewe unaweza uongozi; kama ukisoma Open University of Dar es salaam (duniani zipo open universities nyingi) au hata University of Dar es Salaam, basi wewe huwezi uongozi. 2.) ni concept ya equity katika payment of benefits ktk organization (chukulia organization ni utumishi wa umma) Je kuna equity kweli kiongozi mmoja wa juu alipwe Tshs 40,000,000/= pm peke yake halafu msaidizi anayemfuata Tshs. 4,000,000/= pm. Hivyo sio suala la wivu, ni suala la kuangalia equity. Vile vile sio suala kwamba kwa vile umesoma katika shule za ghali nje ya nchi basi unafaa kuwa kiongozi. Wengi wa hao wanaolipwa mamilioni "inasemekana" hawana kabisa leadership skills, ingawa ni wazuri sana wa kufanya kazi na media.
 
Hiyo mishahara ya 40m. huko mbelez kama utaifanyia kazi, likizo ni siku 28 + 8 days za bank holidays. Siku 5 kwa mwaka kuwa mgonjwa bila cheti cha dakatari. Line manager anakaa na wewe kucheck perfomance yake every once a year. Hii inaangalia uwezo wako wa kumudu yale yaliyo kwenye job description. Kama ulitakiwa uandike research papers na imepita miaka miwili hujafanya hivyo, wanareview contract.

Kupata kazi nyumbani kuna relaxation kidogo. Ufuatilianaji hauko ki hivyo, huyo boss mwenyewe muda wa kukaa na wewe na kuangalia perfomance yako hana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…