tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 23,589
- 21,667
Sasa nawe mbona unalalamika au umeishachukua? Great loser!Salaam,
Za masiku wandugu...
Nimeona humu kuna watu wanalalamika na kulialia kuhusu baadhi ya watu wanaoenda kuchukua fomu za kugombea ubunge hususan kwenye Chama Cha Mapinduzi.
Watu wanalalamika sijui Babu Tale kachukua fomu, Nabii gani naye sijui kachukua, mara Gwajima naye kachukua, n.k.
Sasa ni hivi, kila Mtanzania aliye na sifa, ana haki ya kugombea.
Wewe uliyeko humu JF acha kulialia ukiona wenzio wanajitosa kuchukua fomu ili wagombee.
Kama unaona hao wanaochukua fomu hawafai, uamuzi wa kuwa wanafaa au hawafai, utafanywa na wananchi kwenye sanduku la kura.
Nawe, badala ya kushinda JF kutwa kucha huku ukinung’unika, kachukue fomu ugombee huo uteuzi, kama unajiona una uwezo zaidi kushinda hao watangaza nia.
Zaidi, waweza pia himiza watu wengine uwaonao kuwa wanafaa, kwenda kuchukua hizo fomu ili waweze kugombea.
Muda wa kutenda ndo huu, kama kweli vilio vyenu ni vya dhati.
Kinyume na hapo, itakuwa ni kelele za mtandaoni tu.
Acha kulialia JF. Tinga ofisi za chama ukipendacho katika jimbo lako, uchukue fomu.