ACACIA; Taarifa ya mkutano na wanahabari uliomalizika UK ;Kuhusu sakata la mchanga "Makinikia"

Hichi kitendo cha ACACIA kusema...'following which we would welcome the opportunity to discuss the findings directly with the Government. We remain hopeful that we will be able to reach a resolution to the current situation with the Government..... yaani eti sasa wanataka wakae chini na serikali yetu tuzungumze...na wanasema 'tunaamini tutafikia mwafaka mzuri...' maana yake ni kwamba ACACIA wametambua kwamba tumejua WANA MAKOSA na ushahidi upo. Mbona mwanzoni walikuwa wanatishia kwenda mahakamani?
 
Kwani na hii Tume ya pili inachunguza kile kilichochunguzwa na Tume ya kwanza?

Ndugu yangu wapotoshaji hawasemi ukweli Kazi ya tume ya pili sio kuchunguza tume ya kwanza. Ukiona wanalia lia na press mara waseme hili na lile jua Magu kawashika pabaya. Hawa jamaa inaelekea hawatuibii sisi tu bali wanapiga hadi kwa wamiliki wao. Yani mzigo wanaouongeza haufiki kwa wakubwa wao, wanachowakilisha ni kile walicholipia kodi kwetu halafu hiyo wanayoongeza kwa kushirikiana na watu wetu wanapiga juu kwa juu. Hivi ndivyo wanavyofanya middlemen wa kimataifa.
 
Sasa Hao wanatoa Vipi updates UK wakati Tatizo liko hapa TZ..

Huo ndio upuuzi wa Wazungu kujiona wao ni mungu watu na kila kitu kinakuwa controlled Ulaya..
Kama umeisoma hiyo tipoti kwa makini ungegundua wala haikutulenga sisi bali imelenga kutuliza kihoro cha investors... kwa maana ya public shareholders!!!

Hawa jamaa wapo registered kwenye stock exchange huko huko uzunguni! Na kwa sasa thamani ya hisa zao nadhani bado inaendelea kuporomoka! So, the idea behind ni kujenga investor's confidence ili waone this's just turbulent business situation and in no time, kila kitu kitakuwa settled na kurudi kwenye hali ya kawaida!!!
 
Hakuna ku reach settlement. Wezi wakubwa nyie. Mje mchukue ma vijiko yenu mkachimbe dhahabu Uingereza. Mbona mnang'ang'ania hapa kwetu? Kwani dhahabu ni Tanzania pekee? Kwanza hamna faidia kwa uchumi wetu. Kila kitu mnaagiza kutoka nje, hapa mnatuchia mashimo tu, na mrahaba pia mnatunyonya! Go to hell you thieves.
 
Hichi kitendo cha ACACIA kusema...'following which we would welcome the opportunity to discuss the findings directly with the Government. We remain hopeful that we will be able to reach a resolution to the current situation with the Government..... yaani eti sasa wanataka wakae chini na serikali yetu tuzungumze...na wanasema 'tunaamini tutafikia mwafaka mzuri...' maana yake ni kwamba ACACIA wametambua kwamba tumejua WANA MAKOSA na ushahidi upo. Mbona mwanzoni walikuwa wanatishia kwenda mahakamani?
We unadhani hiyo habari wanatuambia Watanzania?! Hiyo ni taarifa kwa wanahisa wao kwahiyo lazima watafute lugha ya kuwapoza kuwaaminisha haya yanayoendelea ni suala la muda na soon yatapatiwa ufumbuzi!!! Hilo kwao ni muhimu kutokana na ukweli kwamba hisa zao zinashuka thamani and the only way kwao hivi sasa ni kujenga shareholders confidence!
 
Kamitii ya pili ikijaribu kuja mwelekeo tofauti na mfalme atawatumbua na atawaambia mmepewa rushwa.d
Tusibiri muda ni mwalimu mzuri hisa za ACACIA zitaimarika nijinunue zangu
Tatizo lenu hampendi kuhangaisha kichwa ndio maana mnafeli hizo shule za kata.
Kamati ya pili inakuja na ripoti ya kisheria na kiuchumi,baada ya ripoti ya kwanza kuvumbua madudu.
Itaangalia matatizo ya kisheria na kiuchumi na itashauri jinsi ya kutatua.Yaani kama tunadai chetu tufuate njia ipi kutokana na mikataba tuliosaini n.k
 
Ndugu zangu watanzia ngoja niwaambie hapa niko neutral kabisa.
Katika biashara kuna nafasi ya kuepuka regal proceeding.
Na katika medani ya kijeshi tuna sema you can win the battle but not the war.
Sisi tulishinda vita ya Uganda lakini tulipata makovu ikiwemo ukimwi.
Sasa tuache tume ya pili imalize kazi yake. Na ikisha maliza na kumkabidhi Mheshimiwa asitangaze matokeo bali awaite ACASIA wakae na wataalamu wa mheshimiwa tu negotiate upya mikataba kwa faida ya pande zote mbili.
Na hapa mheshimiwa amuongeze Tindu Lissu kwenye meza yake tufanye kazi kwa manufaa ya watanzania na waewkezaji.
Huo utakuwa ushindi kwa nchi.
Kwetu wahaya wakigombana mke na mume ukapeleka kesi kwa wazee huwa hakuna mshindi(gwasinga
enyomyo).
Issue imalizike salama tuendelee na biashara.
Wabeja
 
Hakuna ku reach settlement. Wezi wakubwa nyie. Mje mchukue ma vijiko yenu mkachimbe dhahabu Uingereza. Mbona mnang'ang'ania hapa kwetu? Kwani dhahabu ni Tanzania pekee? Kwanza hamna faidia kwa uchumi wetu. Kila kitu mnaagiza kutoka nje, hapa mnatuchia mashimo tu, na mrahaba pia mnatunyonya! Go to hell you thieves.
Mbona povu lakutoka wakati babu zako wa cccm walitia wino wao na kula chao
 
Wamekuwa wapole sio kama kutokana na picha ya jamaa waliompatia mlungula basi yale makontena pale bandari nahisi kuna vitu vinafichwa hapa.
 
Back
Top Bottom