Guin
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 68,618
- 163,378
Bado karma kwa;Wanabodi
HIki ni kisa cha kweli, mwenzenu leo yamenikuta ya kunikuta nimepata a shock of my life!. Nilikuwa na furaha na matumaini tele, mara ghafla furaha yangu ikageuka shubiri!.
Kisa chenyewe kilianzia miaka ya mid 1990s enzi hizo mimi ni mtangazaji nyota, naandamana na rais Mkapa ziara za ng'ambo zikiwemo za UN, naendesha kipindi cha Kiti Moto, hadi baadhi ya viongozi wa serikali wananiogopa, hivyo nikajiona mimi ndio mimi, sioni, sisikii wala mtu haniambii kitu!, kila kinachokatiza mbele ya macho yangu nikitaka lazima nipate!.
Siku moja nikiwa nchi fulani, nikafuatwa na mtu mmoja raia wa nchi hiyo, baada ya kuelezwa kuna ujumbe wa Watanzania. Basi huyo jamaa akanimegea issue fulani kumhusu mdada fulani mrembo wa Tanzania mwanasiasa kijana al maaruf enzi hizo.
Sisi waandishi sometimes tunakuwa vimbelembele sana, ukipata habari mbaya ya mtu maarufu ama unakimbilia kuilipua au na sisi pia ni binadamu, au unampenyezea mhusika na kumtishia kumlipua ili 'akuone', asipokuona una mlipua!, na kama mhusika ni mwanamke, then unaitumia hiyo news kama fimbo ya kumchapia au gear ya kuingilia ili ...
Mimi kurejea nchini, nikamtafuta mwanasiasa huyu mrembo shombe shombe ili nimbananishe ili angalau na mimi... si unajua ujana!
Bi Dada akaniambia taarifa hizo ni uongo, huyu mtu anamzushia tuu. Mimi sikumuamini bi dada na kumtishia kumlipua kama vipi 'tuzungumze'. Bi dada akagoma kufanya 'mazungumzo yale' kwa hoja kuwa ni uongo na uzushi, na mimi naendea kumuaminia source wangu alichoniambia ni ukweli mtupu!.
Mimi na bi dada tukashindwa kufikia any compromise, hivyo nikamlipua!. Kilichofuata bi dada moto ulimuwakia akamwaga unga na sikujali what happened to her!.
Sasa leo, niko mkoa fulani kwenye lile jambo langu fulani lile, leo ndio interview, nimelikamilisha vizuri nikiwa na furaha tele na matumaini chanya.
Nimetoka chumba cha interview kabla sijafika nje ya ukumbi naitwa nimeambiwa subiri. Mara namuona mama mtu mzima ambaye ndie katibu wa ile interview, ananisalimia kwa majina yangu yote mawili huku ana smile,
"Unanikumbuka?"
Nikamwangalia trying to recal nimemuona wapi, sikukumbuki but the face looks bit familiar.
Nikamjibu sikumbuki naomba unikumbushe,
Akanitajia
"Mimi ni fulani bin fulani...umenikumbuka?"
Duh...!. Nilipigwa na a shock of my life!.
Kumbe yule bidada niliyemlipua mwaka 1995, miaka 27 iliyopita, sasa ndiye boss wa interview yangu!.
"Interview umefanya vizuri nikaona nije kukusalimia na kukumbusha!, nenda salama mimi ngoja nirudi kwenye kikao"
Ghafla mwili uliingia baridi kama barafu nili freezi, nikataka kuishiwa nguvu na kuanguka, miguu imeingia ganzi ghafla haiwezi kuubeba mwili, nikaegemea ukuta nisianguke!.
Mmana huyo kageuza kurudi ndani!
Kwa sekunde kadhaa nilibaki mdomo wazi na adrenalin rush sauti imenikauka, macho kama naona giza!, napata kama kizunguzungu, nikaambaa ambaa huku nimeshika ukuta hadi kwenye viti vya karibu nikakaa na kuvuta pumzi kwa nguvu kama nataka kushindwa kupumua!.
In such a situation, kuna kusubiria tena majibu ya lile jambo letu?.
Tena nikivuta picha kukumbuka when she was begging me, nisimlipue, she cried!. She insisted if it was true, she would have done anything that I ask but it was not true!.
Lessons.
Hii shock of my life niliokutana nayo leo, na furaha yangu kugeuka shubiri, imenifunza lile somo la be good to people on your way up, you might meet them on your way down!, usijisikie wewe ndio wewe wakati ukiwa juu na kuwatenda wengine kuwadharau, kuwaonea, kuwalipua, na kuwatesa, huijui kesho yako, utakutana nao wapi wewe ukiwa nani na wao ni kina nani.
Yule mdada mrembo niliyemlipua enzi hizo mimi ni mimi, leo yeye ndio boss anayetakiwa kutia tick jina langu lisonge mbele!. Mwenzenu leo yamenikuta, na ikitokea msiponiona kusonga mbele, sio upungufu wa sifa, bali ni karma reprisals hit back za what goes around, comes around!. Be humble na kuwatendea mema watu!. Sasa hivi natafakari nilipata nini kwa kumuwasha yule dada wakati huo nikiwa top, compared to sasa nakosa nini mimi nikiwa down and she is top!.
Majuto ni mjukuu!.
We Mama nilio kukosea kwa kukutenda ulipokuwa msichana, nakuomba unisamehe sana kwa nilio kutendea,
nimekosa mimi
nimekosa mimi
nimekosa sana!
Naomba huruma yako!, maana nimeisha kula bakora za karma za kutosha!.
Ila pia ikitokea ukashindwa kusamehe
MImi nikikatwa ni nimekatwa kihalali kabisa kufidia matendo yangu enzi za ujana maji ya moto!.
Mungu unisamehe, unifundishe kunyamaza and being humble!.
Karma is real!.
Amen
Paskali.
1. Kabendera
2. Lissu
Mbona utakoma?
Hivi Pascal kaka si huwa tunakuonya sana jukwaani kuwa ubadilike?
Kumbe tabia ya kuumiza umeianza kitambo?