Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,430
- 118,838
Wanabodi
Hiki ni kisa cha kweli, mwenzenu leo yamenikuta ya kunikuta nimepata a shock of my life! Nilikuwa na furaha na matumaini tele, mara ghafla furaha yangu ikageuka shubiri.
Kisa chenyewe kilianzia miaka ya mid 1990s enzi hizo mimi ni mtangazaji nyota, naandamana na Rais Mkapa ziara za ng'ambo zikiwemo za UN, naendesha kipindi cha Kiti Moto, siogopi mtu!, sina heshima, sina adabu, sina nidhamu! Baadhi ya maswali yangu yalikuwa so provocative hadi baadhi ya viongozi wa serikali wakawa wananiogopa! Hivyo nikavimba bichwa hilo nikajiona mimi ndiyo mimi, sioni, sisikii wala mtu haniambii kitu. Kila kinachokatiza mbele ya macho yangu halali yangu!
Siku moja nikiwa nchi fulani, nikafuatwa na mtu mmoja raia wa nchi hiyo, baada ya kuelezwa kuna ujumbe wa Watanzania. Basi huyo jamaa akatafuta mwanahabari akanimegea info tip ya issue fulani kumhusu mdada fulani mrembo wa Tanzania mwanasiasa kijana al maaruf enzi hizo akitaka iripotiwe kwenye vyombo vya habari.
Sisi waandishi sometimes tunakuwa vimbelembele sana, ukipata habari mbaya ya mtu maarufu ama unakimbilia kuilipua na sisi pia ni binadamu au unampenyezea mhusika na kumtishia kumlipua ili 'akuone', asipokuona una mlipua. Na kama mhusika ni mwanamke, na sisi watu wa Kanda ile na ule udhaifu wetu na wanawake weupe!, then unaitumia hiyo news tip kama fimbo ya kumchapia au gear ya kuingilia ili.
Mimi kurejea nchini, nikamtafuta mwanasiasa huyu mrembo ili nimbananishe ili angalau na mimi, si unajua tena mambo ya ujana!
Bi dada akakana taarifa hizo kuwa sii za kweli ni uzushi wa uongo, huyu mtu anamzushia tuu. Mimi sikumuamini bi dada na kwa hoja moja tu, why her?
Nika amua kumtishia kumlipua kwenye media kama vipi 'tuzungumze' tuelewane nipotezee kwa kukauka na kukausha. Bi dada akagoma katakata kufanya 'mazungumzo yale' kwa hoja kuwa ni uongo na uzushi, na mimi naendelea kumuaminia source wangu alichoniambia ni ukweli mtupu.
Mimi na bi dada tukashindwa kufikia any compromise, hivyo nikamlipua kwa kuiandika story na kuiripoti na ikatoka, watu wa magazeti nao waka i pick from TV nakuishikia kidedea, ika trend kama wildfire na usually bad news spread faster!
Issue ilipojulikana, wenye kazi zao nao wakaingia kazini kuifuatilia na kilichofuata bi dada moto ulimuwakia akawekwa pending pembeni kupisha uchunguzi. Kwa muda huo mimi wala sikujali what happened to her. Kumbe baadae issue ikwisha she was cleared hivyo bi dada akaendelea na kazi kwa kupanda vyeo sasa ni bosi mkubwa!
Na mimi kwa upande wangu umaarufu wangu wa kipindi cha Kiti Moto ulikuja kuisha, kipindi kilipigwa marufuku kutokana na kuwabananisha viongozi na kuwalipua. Nikaja kuacha kazi na kutimkia zangu ughaibuni.
Mwaka 2000 nikarejea Bongo nikajiunga TBC sikudumu nikakumbana na mabalaa chungu tele, mara kukimbiwa na mke, mara kupata ajali mbaya na ku paralyze, kumbe ni malipo ya accumulation ya karma za matendo yangu ya nyuma, tutendeni mema jameni, ukitenda ubaya wowote, malipo ni hapa hapa duniani!
Sasa leo, niko mkoa fulani kwenye lile jambo letu lile, leo ndio interview! nimelikamilisha vizuri kuhojiwa, nimejibu maswali yote vizuri kwa ufasaha bila kubabaika, nikiwa na furaha tele na matumaini chanya kwasababu niko vizuri kwenye kujieleza, uzoefu umesimama, shule imepanda, kwa sifa tuu, uwezo na vigezo kiukweli kabisa sijifagilii, ninavyo na niko vizuri, ila unaweza kukuta kwenye watu 186 wazuri wako 40 na wengine ni wazuri zaidi yako nafasi zenyewe ni 6, kati ya 6 hizo, nafasi 3 ni za wanawake!, hivyo mijiba 100 mnagombea nafasi 3!, kati ya tatu hizo moja ni ya Zanzibar!, mtu ukikosa utalalamika?.
Nimetoka chumba cha interview na furaha yangu, kabla sijafika nje ya ukumbi naitwa nimeambiwa subiri. Mara namuona mama mtu mzima kidogo, na mshepu ambaye ndiye katibu wa ile kamati ya interview, ananisalimia kwa majina yangu yote mawili huku ana smile, "unanikumbuka?"
Nikamwangalia trying to recall nimemuona wapi, sikukumbuki but the face looks bit familiar.
Nikamjibu sikumbuki naomba unikumbushe, akanitajia "mimi ni fulani bin fulani, umenikumbuka?"
Duh.m! Nilipigwa na a shock ya mwaka of my life! Kumbe yule bidada niliyemlipua mwaka 1995, miaka 27 iliyopita, sasa ndiye boss wa interview yangu!
"Interview umefanya vizuri nikaona nije kukusalimia tuu na kukumbusha ili unikumbuke ulichonifanyia!. Nenda salama mimi ngoja nirudi kwenye kikao"
Ghafla mwili uliingia baridi kama barafu nili freeze, nikataka kuishiwa nguvu na kuanguka, miguu imeingia ganzi ghafla haiwezi kuubeba mwili, nikaegemea ukuta nisianguke.
Mmama huyo kageuza kurudi ndani!, anatembea taratibu with confidence huku nikikodolea mshepu kwa nyuma nikibaki sina hili wala lile! Kwa sekunde kadhaa nilibaki mdomo wazi na adrenalin rush sauti imenikauka, macho yamenitoka kama nakabwa nimeona jini!, huku mwanga ukififia naona giza. Napata kama kizunguzungu!
Nikaambaa ambaa huku nimeshika ukuta hadi kwenye viti vya karibu nikakaa na kuvuta pumzi kwa nguvu kama umeachiwa baada ya kukabwa nataka kushindwa kupumua.
Just tell me, in such a situation, kuna kusubiria tena majibu positive ya lile jambo letu?!. Tena nikivuta picha kukumbuka when she was begging me, nisimlipue, tears dropped on her dimples cheeks, she almost cried!. She insisted if it was true, she would have done anything that I ask but it was not true!.
Lessons
Hii shock of my life niliyokutana nayo leo, na furaha yangu kugeuka shubiri, imenifunza lile somo la be good to people on your way up, you might meet them on your way down!. Usijisikie wewe ndio wewe wakati ukiwa juu na kuwatenda wengine kuwadharau, kuwaonea, kuwalipua, na kuwatesa, huijui kesho yako utakutana nao wapi wewe ukiwa nani na wao wakiwa nani!
Yule mdada mrembo niliyemlipua kwenye media enzi hizo mimi ni mimi, leo yeye ndio boss anayetakiwa kutia tick jina langu lisonge mbele, na mimi leo ndio a beggar begging for her mercy!.
Mwenzenu leo yamenikuta, na ikitokea hata kama na mimi nimekidhi sifa na vigezo na niko among the top aspirants, msiponiona jina langu kusonga mbele, mjue sio upungufu wa sifa, bali nimezidiwa sifa na wengine na sio nimeenguliwa kwasababu ya hii issue! Ila pia ikitokea nimekidhi sifa na vigezo ila poa nina mzigo mkubwa wa makando kando ambayo hayabebeki, nawaomba ndugu zangu, tukubaliane na matokeo yoyote, na ikiwa hivyo, I don't point fingers or shift the blame to anyone, the cause ni mimi mwenyewe, "ME, MYSELF & I" na karma reprisals hit back za matendo yangu ya nyuma on what goes around, comes around!
Kwa vile mimi yamenikuta, naomba niwe darasa kwa wengine, always be humble na kuwatendea mema watu wote, heshima watu wote wakubwa na wadogo na usidharau watu. Wadogo wa leo ndio wakubwa wa kesho!
Sasa hivi natafakari nilipata nini kwa kumuwasha yule dada kwenye media wakati huo nikiwa top, compared to sasa nakosa nini mimi nikiwa down and she is top!
Karma is real na majuto ni mjukuu!
We mama niliyo kukosea kwa kukutenda ulipokuwa msichana, nakuomba sana unisamehe kwa yote nilio kutendea.
Nimekosa mimi,
Nimekosa mimi,
Nimekosa sana!
Naomba huruma yako, maana nimeshakula bakora za karma za kutosha.
Ila pia ikitokea ukashindwa kusamehe mimi nikikatwa ni tayari nimejikubali nimekatwa kihalali kabisa kufidia matendo yangu enzi za ujana maji ya moto. Mungu unisamehe, unifundishe kunyamaza and being humble.
Naahidi kuwa mtu mwema zaidi sasa na yale mazuri yote ninayoitendea nchi yangu, hata bila uteuzi nitaendelea kuyatenda na kuwa raia mwema wa JMT, tena kwa taarifa, ile tabia ya ku lipua lipua watu kwenye media due to info tip sasa nimeisha achana nayo na mfano hai ni ile siku napata info tip hii Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli by this time, already I had a certain info tip fulani ya mtu huyu kutoka kwa Mkuu britanicca , hiyo info tip niliizungumza tuu humo
Huyu Pascal Mayalla wa sasa, japo bado ni mwandishi wa habari wa kujitegemea kwa kujitolea, kwanza ameachana na kuandika habari za kiuchunguzi, Investigative Journalism (IJ) na kujikita kwenye Developmental Journalism (DJ), pili akikutana na damaging info tip, anatumia objectivity zaidi kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa Swali la Morality: Je, ni lazima kuusema kila ukweli unaousikia au tutangulize mbele maslahi ya Taifa?
Hivyo sasa wajemeni mimi ni a completely changed person!, nisihukumiwe au kuadhibiwa kwa makosa yangu ya zamani bali nihukumiwe kwa mawazo, maneno na matendo yangu ya sasa, kama nilivyo shauri hapa Tum-judge Rais Samia kwa mawazo, maneno, na matendo yake ya sasa akiwa ni Rais wa JMT na siyo kwa alivyokuwa VP! tukianza kuhukumiana kwa mawazo, maneno, matendo na makosa ya nyuma, nani atasimama?
Mungu nisaidie.
Amen.
Paskali.

Just imagine kama ningekuwa ni yule Pasco wa Kiti Moto, nikaziweka hizo sababu, could you imagine ingekuwaje?!.Wanabodi,
Leo nimekutana na rafiki yangu wa siku nyingi tuliyepotezana naye kipindi kirefu nyuma, ambaye ni mtu wa sehemu na wa kuaminika sana ambaye yuko attached CCM kama kada tuu wa kawaida wa Chama cha Mapinduzi-CCM, akanieleza seriously habari za kushtusha kidogo ambazo mimi zimenitisha, zimenisikitisha, kunihuzunisha, kuniogopesha, kunisononesha na kuninyongonyeza!, kuwa eti imeishaamuliwa (sitaji imeamuliwa na nani), kuwa mgombea wa urais wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi-CCM ni Mhe. John Pombe Magufuli!.
Kilichonistua, kunitisha, kunihuzunisha, kunisikitisha, kunisononesha, kunigopesha na kuninyongoneza ni the reasons behind, sababu alizonitajia kada huyu za why mgombea wa CCM mwakani ni Magufuli, ambazo ndizo zimepelekea the inner core ya CCM kuamua mgombea wake wa urais wa 2015 ni lazima awe John Pombe Magufuli tuu, and no one else!.
Kwa vile sababu hizo alizonitajia, baadhi kweli ni sababu za msingi na ziko justifiable kwa any reasonable man, sababu nyingine alizonitajia sio tuu ni unreasonable, bali pia ni unjustifiable! na hazikubaliki kabisa katika Tanzania ya leo!.
Naomba kwa sasa nisizitaje kwanza hizo sababu nilizotajiwa za kwa nini ni Magufuli, kwa sababu habari zenyewe nimezisikia juu juu tuu tena from just a single source, hivyo nahitaji kwanza kujiridhisha kwa kufanya verification kwa ku double check, na ku cross check ikiwemo kupata a collaborative verification na attribution ya third parties ili nijiridhishe kuwa hii ni habari za kweli na kuthibitisha kuwa kumbe hivyo ndivyo the inner core ya CCM inavyoweza kufikia maamuzi ya mgombea wake wa urais based on sababu nilizo tajiwa!, then nitaziweka hadharani hizo sababu za kwa nini CCM imeamua mgombea wake wa urais kwa uchaguzi wa 2015 lazima awe ni John Pombe Magufuli tuu na sio mtu mwingine yoyote!, na kiukweli mkizisikia hizo sababu nilizotajiwa, naamini hata nyinyi sio tuu mtashangaa, bali mtakubaliana na mimi kwanini mtu huyu asiwe!.