A man is not a man until he has a house of his own."

MKATA KIU uko sawasawa wewe?
'
Mandela kafanya nini kipya?
'
Maamuzi gani ya ajabu na ya kutisha aliyoyafanya?
'
Kwako uanaume ni nini?
'
Sikutaka kusema haya lakini kwa kauliyako nakueleza kuwa hapa Mandela alipotoka sana na hakupaswa kuzungumza maneno ya hovyo kama haya!

Ha ha ha babu naona nimekugusa,,

Sikatai kila mtu ana mapungufu yake na hakuna aliye perfect,, lakini nina imani mapungufu yamazidiana na mandela ana mchango mkubwa kwenye jamii kuliko Eiyer na MKATA KIU

Au babu unataka kusema wewe ni zaidi ya mandela?
 
Last edited by a moderator:
ukizaliwa maskini unaweza kuwa na mawazo mengi sana ya ajabu na mengine ya kuchekesha, mtu anaona kuwa na nyumba ni kitu cha ajabu sana, pia mwingine anaona kumiliki gari ni kitu cha jabu saana. wakati mtu mwingine anawaza kuwa na kampuni yake inayokua kwa faida na kufungua kiwanda a day ndio awe "man" . wewe unawaza eti kumiliki tu ka-kibanda ndio roho yako iwe kwatu, au mwingine anawaza tu amiliki ka-miguu minne ndio roho yake iwe kwatu. sikushangai ni kwasababu umezaliwa kwenye familia maskini.

kauli yako watu wanaweza kuichukulia juujuu lakini ina ukweli sana........ukiwa masikini unasumbuliwa na mwenye nyumba lazima uwaze kujenga ili UKAMILIKE.....na kama hujakulia kwenye magari umepata shida sana na madaladala lazima ukipata ahueni ununue kigari uepuke shida za madaladala......
 
aiseeeee babayangu sasa haka kabanda changu nilichojenga kwa kushirikiana na mama mkuu rombo inamanisha mimi si mwanaume wa shoka
 
kuna watu wana pesa zao nyingi tu na hawana mpango wa kujenga nyumba, nenda mjini waone wahindi wana pesa chafu lakini wameamua kupanga, kwahiyo hao sio vidume? mwanaume kamili ni yule anayetimiza wajibu wake unaompasa kwenye jamii inayomzunguka, ukianzia na familia yako. kutimiza kile kidogo anachoweza kuifanyia jamii yako, familia yako.

kama ww ni mbunge timiza wajibu wako kwa nafasi yako kwa jamii yako, kama wewe ni mtu wa kawaida timiza wajibu wako kwa jamii inayokuzunguka kuanzia familia yako. baba usilewe pombe kupita kiasi na kuacha watoto wakakosa ada, mama timiza wajibu wako watoto wasilale njaa na ww upo ngomani, dada/kaka jua wajibu wako kwa wadogo zako na familia yako. lakini hii definition ya "man" ya mandela ni ya kipuuzi na ya kimaskini sana.
 
"The house itself was identical to hundreds of others built on postage-stamp sized plots on dirt roads. It had the same standard tin roof, the same cement floor, a narrow kitchen and a bucket toilet at the back... It was the opposite of grand but it was my first true home of my own and I was mightily proud. A man is not a man until he has a house of his own."

— Mandela, on 8115 Orlando Wes
is it true ?????????????mimi naunga hoja mkono .kwamba
''A man is not a man until he has a house of his own."
Hakika umenena, hata kama ni ya matope ikiwa ya kwako utajivunia, hata kama hautaishi humo, lakini unajua ikitokea siku ukihamishwa na mwenye nyumba wako unaelekea kwako walau utaweka mizigo yako..!!
It is something that every man is longing to see it happens on his life earliest possible before his end...
 
ukizaliwa maskini unaweza kuwa na mawazo mengi sana ya ajabu na mengine ya kuchekesha, mtu anaona kuwa na nyumba ni kitu cha ajabu sana, pia mwingine anaona kumiliki gari ni kitu cha jabu saana. wakati mtu mwingine anawaza kuwa na kampuni yake inayokua kwa faida na kufungua kiwanda a day ndio awe "man" . wewe unawaza eti kumiliki tu ka-kibanda ndio roho yako iwe kwatu, au mwingine anawaza tu amiliki ka-miguu minne ndio roho yake iwe kwatu. sikushangai ni kwasababu umezaliwa kwenye familia maskini.

Nyumba ya kuishi = Shati/gauni la kuvaa? I think Investments ndiyo mpango mzima!!
 
Back
Top Bottom