50 Greatest Tanzanians (minus politicians)

hayo mabomba ya mianzi ya lipangile, bora yaliwekewa zengwe, yalikuwa yanadumu mwaka mmoja tu yanaoza kama hakuna flow ya maji nalo pia lilikuwa tatizo, kuvujisha maji pindi yakianza kupita.

acha kupotosha jamii unauhakika na maneno unayoyasema haya mabomba yapo kwetu mgama toka mwaka 1985 hadi leo, halafu unavyosema yanadumu mwaka mmoja umefanya research au unalopoka tu ilimradi tu umeongea
 
Haitoshi kutaja jina peke yake mkuu,
wengine tuko darasani hapa kujifunza

Aliyetunga wimbo wa Taifa, mzee Beda Amuli huyu ni Architect aliyesanifu soko la Kariakoo. Moses Nnauye rtd Brd Gen alitunga wimbo wa "Tazama ramani utaona nchi nzuri..............".
 
Tundu Antipas Mugwai Lissu-shujaa na mtetezi mkuu wa watu wanaoishi maeneo ya mgodi aliyeanika uovu wa fukiafukia ya Bulyanhulu. Amekamatwa na kufungwa na kuwekwa korokoroni mara kadhaa kutetea wanyonge hao.

Ametumia taaluma yake ya sheria kutetea waathirika wa migodini huko mahakamani ingawa kwa sasa ni mwanasiasa lakini kwa makubwa aliyofanya kutetea wanyonge anastahili kuwa shujaa wa wanyonge Tanzania.
Noma sana
 
Kusherekea 50 years naomba mtuletee list ya 50 greatest Tanzanians (tukimtoa Nyerere na wanasiasa ambao tushawajadili sana)

Itakuwa si vibaya mkatuletea na sababu why these unsung heroes are great

Si lazma mje na list ya majina 50 lakini muhimu ni kutuambia kwa nini hawa watu japo hawaenziwi na watawala wetu lakini muhimu kuwajaua na michango yao kwenye historia ya Tanzania.

Personally nitaanza na Mashado Plantan ambaye nilikuwa simjui mpaka member mmoja humu alipoingia na jina lake na nikatafuta wasifu wake. Mashado was the original INVISIBLE wa enzi zake kwani alikuwa ni Mwafrika Mtanzania wa kwanza kuanzisha Gazeti lake lilikuwa linaitwa ZUHURA in the 1950's !

Muhimu wawe wanatoka from all walks of life kasoro wanasiasa.

we might learn a thing or two
Dada Manka ,(Mange Kimambi) wa Marekani, Amongst all stands a national hero Oscar Kambona a bright handsome minister kama mnavyoweza kumuona kwenye Avatar ya member mmoja wa JF. Watu wengi walimpenda na kumuiga kwa stairi yake ya nywele huyu ndiye aliyewatuliza wanajeshi wakati wa maasi.
Chief Ndambile wa Nzega aliyethubutu kumtandika makofi mzungu wakati wa ukoloni aliyemuonesha dharau kwenye ikulu yake ya ghorofa ya miti kama ile ya Mkamba.
 
Mwaka 1963, Mtanzania aitwaye Erasto Mpemba alifanikiwa kufanya ugunduzi ambao moja kwa moja uliweza kupingana na ile kanuni ya Newton.
Mpemba alibaini kuwa, maji yaliyochemka yakiwekwa kwenye jokofu pamoja na maji yenye ubaridi wa kawaida, yale yaliyochemka yanaganda haraka zaidi na kuwa barafu kuliko yale yenye ubaridi wa kawaida.
Tangu Mtanzania huyu kugundua kanuni hiyo iliyopewa jina la Mpemba effect, mpaka leo ni miaka 50 lakini hatambuliki kabisa na taasisi za kisayansi wala zile za kitaaluma kama vyuo hapa nchini. Jambo la kushangaza, Mpemba ni maarufu sana kwenye taasisi za kimataifa, wanayansi wamehangaisha vichwa kujua sababu ya maji ya moto kuganda haraka zaidi kuwa barafu kuliko yale ya baridi.
 
Yan wewe mpemba effect imekusaidiaje wewe, acha hizo
 
2.Reginald Mengi
3.Jenerali Ulimwengu
4.Somebody Nyirenda
5.Riz1 JK
6

1. Baba na Mama yangu mzazi kwa kunizaa na kunisisitizia kusoma mpaka nimefika hapa nilipofikia
6. Mimi binafsi (Nina mashamba kadhaa huko Tanga, Morogoro, Arusha, Singida na ninaajiri watu karibia ya 460 depending on msimu.
 
Yan wewe mpemba effect imekusaidiaje wewe, acha hizo
Kumpinga Sir Isack Newton sio mchezo..Newton’s law of cooling’ vs Mpemba effect....Ulimwengu wa wanasayansi unatambua kazi yake au ndugu ulisoma Yale masomo ya kike
 
1/Freeman Mbowe.
Kupambana na CCM si kazi ndogo.
2/CHADEMA.
Ndio sauti ya wananchi.
3/Tundu Lissu, John Mnyika, Saed Kubenea, Mch Peter Msigwa hawa kazi yao tunaitambua.
 
1. JPM- Kuwashughulia mafisadi ,kuweka mkazo katika uwajibikaji, kuwabana wanyonyaji, kubana punzi ya matapeli Wa kisiasa hasa mbowe na kundi lake, kufanikisha ujenzi Wa miundombinu na kuleta nidhamu ya kiutumishi serikalini

2. Kassim Majaliwa- kumsaidia jpm kuwashughulia wazembe na mafisadi, uchapakaji kazi Wa kupigwa mfano, busara ya kimaamuzi na kiutendaji.

3.Mama samia - kuonesha njia kama mwanamke Wa kwanza kuwa makamu Wa rais,moyo Wa kujali , utulivu Wa akili, mshauri wa rais.

.

.

.

50. Mimi FPT
 
Kama uko kwa madiba jitahidi kupunguza kiwango cha weed kidogo
 
OSALO OTANGO na PAULO HAMISI hawa pia wanahistoria kali ya jinsi walivyo pambana na WAKOLONI wakitumia MAPANGO YA AMBONI kujificha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom