Bin Maryam
JF-Expert Member
- Oct 22, 2007
- 685
- 13
Waheshimiwa, mbona hamsemi kwenye ofisi gani ya serikali, Tanzania na hata Ulaya mmeona mtu amevaa bikini? Condoleeza Rice ambaye inawezekana ndiye mwanamke mwenye nguvu kuliko wote anavaa nguo ambazo wenzetu mtaziita mini(zinaishia juu ya magoti) lakini kwa wengi ni nguo za staha. Hakuna mtu anayeweza kudai kuwa uvaaji wake wa nguo hizo na boots za nguvu zikisisitiza uanamke wake zinampunguzia heshima na ufanisi wake. Eddy, chuo kikuu ni mahali ambapo wanafunzi wanatakiwa wa'test' mipaka ya authority. Mimi binafsi ninapomuona mwanafunzi wa chuo kikuu amevaa suti na tai naingiwa na wasiwasi. Pale ni mahali ambapo non-conformity ndio wajibu. hii inaendana na mpaka mavazi. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu akiingia uchi darasani sitamshangaa maana pengine kuna kitu anachotaka kuieleza jamii. Chuo kikuu ni mahali pa fukuto la mawazo. Kamwe usipachanganye na ofisi za serikali. Katika matatizo yote tuliyonayo leo tumapoteza muda wote huu kuangalia jambo ambalo hata halipo( hakuna mtu aliyeweza kutoa mfano wa ofisi ya serikali wanakovaa bikini au pajama)? Kuzungumzia hili ni kama kusimama jukwaani na kusema kuwa kuanzia leo unakataza kunywa pombe katika ofisi za serikali. Kama hii code(ambayo mimi naona ni ya kipuuzi) ipo angeikazia badala ya kuileta katika public realm.
Mchundo:
Dunia imebadilika sana. Utafiti unaonyesha kuwa watoto marekani wanapenda chips zilizo kwenye packet zenye label ya MacDonald kuliko zilizowekwa kwenye sahani japokuwa mpishi ni mmoja na radha ni sawa.
Nimebadilisha kazi zaidi ya mara tatu na kila sehemu ninapewa manual ya dress code.