Jina langu ninaitwa Soka (sio jina halisi) na kwetu ni huko Moshi uchagani. Nilisoma kwa shida na kufanikiwa kupata elimu ya Sekondari na kisha kujiunga na mafunzo ya ualimu katika chuo cha Marangu na kuhitimu kwa kutunukiwa Daraja A. Baada ya kuhitimu nilipangiwa kituo cha kazi ni huko Kwamsisi...