JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Kuna tetesi zimeibuka leo 25/10/2022 zinadai kuwa Yanga imeachana na kocha wake Mkuu Nasreddin Nabi. Tetesi hizi zimeshika kasi baada ya kuchapishwa na Gazeti la Mwanaspoti pamoja na kutumwa kwenye mitandao ya kijamii. Mpaka kufikia saa saba mchana Uongozi wa Yanga, umeendelea kuwa kimya na kutokuwa tayari kulizungumzia suala hilo, hata walipotafutwa wamesema Nabi bado ni kocha wa timu hiyo hadi hapo itakaptangazwa kivingine.
Madai Shirika la utangazaji la BBC liliripoti kuwa nchi ya China ina mpango wa kufungua vituo vya polisi nchini Nigeria, Lesotho na Tanzania ili kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyofanywa na raia wake wanaoishi katika nchi hizo tatu za Afrika, tovuti inayomilikiwa na mtu binafsi ya Nigeria ya Vanguard imeripoti. Wakiwanukuu watetezi wa Usalama, Vanguard amesema mpangilio wa China unaweza kuonekana kama shambulio dhidi ya uhuru wa eneo husika. Aidha inaelezwa kuwa, [China] imeamua… kushirikiana na United Front linked, mashirika ambayo yako nje ya nchi katika mabara matano, kuanzisha mfumo mbadala wa polisi na mahakama ndani ya nchi tatu, na kuhusisha moja kwa moja mashirika hayo katika mbinu zisizo halali zinazotumiwa kuwasaka...
Ukurasa wa mbele wa Gazeti la The Scotsman la Scotland umekuwa ukisambaa mitandaoni ukiwa na kichwa kinachosema "Rais Samia aongeza matumaini mapya kwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Scotland na Tanzania," Gazeti hilo linalosomeka kuwa ni toleo la 1 Novemba 2021 la gazeti la kitaifa la Scotsman, linaonesha picha ya Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania. Maandishi yaliyo chini ya kichwa cha habari yanasomeka: “Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko Scotland na atakutana na balozi wa Uingereza katika kuendeleza majadiliano kuhusu maendeleo ya mataifa yote mawili kupitia sekta ya Teknolojia na Viwanda.” Ukurasa huu umesambaa katika makundi ya Facebook nchini Tanzania, huku wakimwagia sifa Samia kwa "kuchapishwa" kwenye gazeti...
Video moja iliyowekwa kwenye mtandao wa Facebook inadai kuwa Naibu Rais wa Kenya William Ruto "ameichochea" jamii yake ya Wakalenjin dhidi ya Wakikuyu wakati wa mkutano wa kampeni kabla ya uchaguzi wa Agosti 9 2022. Katika kipande hicho cha video kilichochapishwa tarehe 29 Julai, Ruto anazungumza kwa Kiswahili na Kiingereza, akimwambia rais aache kutaja jina lake. Katika video hiyo Ruto anasema "Zungumza kuhusu mgombea wako,"Nilikuunga mkono ulipohitaji mtu wa kukusaidia. Ikiwa hutaki kuniunga mkono, niache peke yangu.” Ruto alitofautiana na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na yeye akamuunga mkono kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwania urais. Katika video hiyo, Ruto anaendelea kuhutubia rais: “Sasa eti wewe unaanza kuni-threaten...
Kufuatia kutangazwa kwa tukio la uzinduzi wa takwimu za shirika lisilo la kiserikali la TWAWEZA East Africa linalotarajiwa kufanyika leo tarehe 25 Agosti, 2022, kumekuwepo madai/uvumi kuwa tukio hilo limeahirishwa. Taarifa hizo ambazo zimekuwa zikisambazwa katika makundi sogozi ya WhatsApp pamoja na mtandao wa Twitter, zimedai kuwa tukio hilo ambalo linatatajia kuwashirikisha wananchi matokeo ya utafiti uliyofanywa na TWAWEZA unaolenga kuutaarifu umma matokeo hayo yenye uwakilishi wa kitaifa kutoka Sauti za Wananchi - ambalo ni jukwaa la kupigia kura kwa njia ya simu ya mkononi - umeahirishwa, ingawa bila kutoa taarifa kuwa umesukumwa hadi siku/tarehe gani. Hapa chini ni picha ambayo imetumika kusambaza uvumi huo.
MADAI Yapo madai kuwa Fedha za Mfuko wa Jimbo kwa Jimbo la Hai Kilimanjaro hazionekani Jimboni tangu 2020-2022. Mbunge wa Jimbo la Hai, unaulizwa Fedha Za mfuko wa jimbo kwa Jimbo la Hai zimeweza kusaidia shughuli gani tangu 2020 hadi 2022? Aidha, inadaiwa kuna kila dalili fedha hizo wanalamba asali wachache. Miaka ya 2015-2020 fedha hizo zilioneka jimboni na Kufanya shughuli muhimu ila kwa sasa mbunge anajengea nyumba yake ya kuishi.
Najiuliza hiv inakuaje msanii Kama Rayvanny ameshindwa kumalizana na Diamond hadi kaamua kumpeleka Diamond BASATA. Hivi anadhani mikataba inaweza kuvunjwa kirahisi tu na BASATA. Afate masharti ya mkataba basata hawataweza msaidia Kitu. Ajifunze Kwa Harmonize mwenzake hakuhangaika na BASATA alilipa alichotakiwa na kusepa vyema, ikiwemo kuachiwa akaunti zake za mitandao ya jamii kama YouTube. Ajifunze pia Kwa Mavoko hta alipompeleka Diamond basata bado akaunti yake ya YouTube hadi leo inamilikiwa na wasafi Kwa Sababu hakuheshimu mkataba na ikambidi afungue akaunti nyingine ya billionaire kid. Rayvanny zingatia mkataba basata yeye ni mlezi tu hawez kamwe kushurutisha Diamond akusamehe kirahisi na ukumbuke Diamond Yuko na mtu mbad Sana...
Mdau wa JamiiForums.com ameelezea wasiwasi wake juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa UTI kwa wanawake. Anahoji inakuwaje sababu kubwa inayotajwa kuwa ni uchafu ipate mashiko kwa nyakati hizi, kwani wanawake wa zamani ndio walikuwa wasafi zaidi kuliko hawa wa sasa? Mdau huyu anashauri wataalam wa afya waingie upya maabara kuchunguza nini hasa chanzo halisi cha kuongezeka kwa maambukizi ya UTI. Kwake hoja ya kuwa ugonjwa huu unaweza kusababishwa na uchafu anaona kama haina mashiko. Sayansi inasemaje juu ya hoja hizi za mdau?
Habari zenu wakuu Hivi nmekua nikijiuliza sana ni hali ya hewa ndio inapelekea watu kuumwa sana sasahivi au ni nini?? Maana nmekua nikishuhudia watu wangi wakikohoa sana ambapo hali hii yakukohoa wengi wamekua wakieleza kua huwakuta sana ifikapo mida ya saa 12 jioni ambayo huwafanya hata washindwe kulala kwa kikohozi icho kikali. Je, mabadiliko ya hali ya hewa yana mchango wowote katika kusababisha magonjwa?
Back
Top Bottom