JamiiCheck

A citizen-centered approach in countering misinformation and disinformation Online and Offline by JamiiForums

JF Prefixes:

Juni 15, 2023, Mdau wa JamiiForums aliweka chapisho linaloelezea jinsi alivyokwenda kupata chanjo ya COVID-19 na kupatiwa cheti ya chanjo husika. Mdau huyu anaeleza kuwa alitishwa sana kabla ya kupata chanjo hiyo na wengine walimuomba alipie tu pesa ili apatiwe cheti kama sehemu ya uthibitisho wa kuchanjwa. Katika Mjadala huo, mchangiaji mmoja alisema kuwa Taasisi ya Msalaba Mwekundu (Red Cross) ilikuwa imetoa taarifa inayokataza watu waliochanja kuchangia damu kwa wahitaji. Taarifa hii ni sahihi?
Kumekuwa na debate kubwa kuhusu uchezaji wa Michael Jackson kwenye wimbo wa Smooth Criminal, kuna ile dance aliinama digrii 45 akiwa sakafuni mgongo ukiwa umenyooka, alikaa sekunde kadhaa kabla ya kurudi wima. Wataalamu wa uti wa mgongo wanaonya wengine dhidi ya kujaribu hatua inayoweza kuwadhuru. Wanadai uchezaji wa vile hauwezekani kabisa kwa binadamu yeyote. Wengine wanasema Mfalme huyo wa Pop alikuwa na kipaji kikubwa cha uchezaji hivyo suala lile lilikuwa jambo la kawaida. Wengine wanadai kuwa alivaa viatu vilivyoshikilia sakafu ili kumwezesha kuinama mbele digrii 45. Ukweli ni upi kuhusu 'Smooth Criminal Lean Dance'? VIDEO: Smooth criminal Lean Dance
Salaam Wandugu, Nimepata taarifa mtandaoni kuwa ndege ya Malaysia iliyopotea miaka tisa iliyopita imekutwa kwenye maji ikiwa haina abiria. Habari hiyo ilichapishwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwamo Twitter linaonesha picha ya mbele ya ndege yenye kutu inayosomeka: “Ndege ya Malaysia MH370 iliyotoweka miaka 9 iliyopita imepatikana chini ikiwa haina abiria. Ndege hiyo ilikuwa na abiria 239.” Je, kuna ukweli wowote? Picha inayoenea kwenye mitandao Picha ya ndege ya Lockheed Martin L1011 Tristar kwa upande wa pembeni Source: Deepbluedivecenter Video credit: Deepbluedivecenter
Ulaji wa viazi vitamu kwa kipindi kirefu unadaiwa kusaidia uzalishwaji wa mayai mengi kwa Mwanamke na hivyo kupelekea kupata watoto mapacha. Jiji la Igbo-Ora lililopo nchini Nigeria ni jiji lenye mapacha wengi na Nigeria imepewa jina la mji mkuu wa Mapacha Duniani kwa kuwa na watoto mapacha wengi zaidi kuliko eneo lolote duniani huku viazi vitamu vikiliwa zaidi nchini humo. Ni kweli kuwa Viazi vitamu huongeza homoni aina ya ‘phytoestrogen’ ambayo huchangia kwenye kupevusha yai zaidi ya moja kwa wakati mmoja hivyo kusababisha kuzaliwa kwa watoto mapacha?
Back
Top Bottom