Janabi amesema kuwa wana mkakati maalum wa kutoa huduma za kisada za tiba kwa wagonjwa wanaofika hospitalini

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Sep 6, 2020
812
513
TUNA MKAKATI MAALUM NA COMORO - Prof. JANABI

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Mohamed Janabi amesema kuwa wana mkakati maalum wa kutoa huduma za kisada za tiba kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kutoka visiwa vya Comoro kutokana na ongezeko la idadi yao katika siku za karibuni.

Prof. Janabi alisema hayo alipokuwa akizungumza na Balozi Mteule wa Tanzania nchini Comoro, Saidi Yakubu aliefika kumuaga.

Prof. Janabi ambaye pia ndio Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Utalii wa Matibabu alieleza kuwa kwa hivi sasa wana mratibu maalum wa wagonjwa toka nje ya nchi na pia mkalimani wa lugha ya kifaransa ili kurahisisha mapokezi ya wagonjwa toka Comoro na wako tayari kuwa na kliniki za ufuatiliaji kwenye visiwa hivyo.

“Kwa idadi yao na inavyoongezeka, tunakusudia tuwe na wadi maalum ya wanaotoka Comoro katika siku za karibuni” alisema Prof. Janabi.

Kwa upande wake, Balozi Yakubu aliahidi kwenda kufanyia kazi na kuwa na uratibu mzuri wa wananchi wa Comoro kuja nchini kwa matibabu.
 

Attachments

  • IMG-20240520-WA0025.jpg
    IMG-20240520-WA0025.jpg
    219.1 KB · Views: 1
  • IMG-20240520-WA0026.jpg
    IMG-20240520-WA0026.jpg
    178.9 KB · Views: 1
  • IMG-20240520-WA0024.jpg
    IMG-20240520-WA0024.jpg
    141.5 KB · Views: 1
Back
Top Bottom