GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 4,968
- 6,742
Kwenye Biblia, Adam alipoulizwa kwa nini kala tunda alilokatazwa, alijitetea kuwa si kosa lake, bali kashawishiwa na mke wake. Ingelikuwaje kama angelikubali kosa na kuomba msamaha?
Daudi alipofahamu kuwa kagundulika kuwa alimwua Huria baada ya kuzini na mke wake, hakujitetea kuwa ni mke wa Huria ndiye aliyezembea kwa kuoga kwenye bafu lisilo na paa kulikopekekea yeye kumwona na kumtamani, bali alilikubali kosa lake na kuwa tayari kuwajibika kwa makosa yake. Kulikiri kosa lake kulimfanya asamehewe.
Ni kanuni iliyothibitishwa kuwa huwezi kukibadili usichokikabili.
Huwezi kurekebisha kosa ambalo unaamini kuwa umesababishiwa na mtu au kitu chochote. Ni mpaka kukubali kuwajibika kwa asilimia mia moja ndipo utakapoona njia ya kutokea.
Kwa nchi za Afrika Mashariki, hasa Tanzania, Kenya, Rwanda na Uganda, inafahamika kuwa ni Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa Kiingereza cha kiubabaishi.
Ingawa tuna lugha yetu adhimu ya Kiswahili, lakini si kizuizi cha kuielewa na English ambayo kimsingi, ndiyo lugha ya Kimataifa kwa sasa. Kwa nini tusikijue kwa ufasaha na huku:
1. Ndiyo lugha ya kufundishia kuanzia Sekondari hadi Chuo Kikuu
2. Ni kati ya "official languages" katika taasisi za uma.
Mtu pekee mwenye uhalali wa kutokukijua ni ambaye hajapitia Sekondari, lakini kwa wengineo wote, ni "uzembe", na mpaka mtu akubali kuwa ni uzembe wake ndiyo atachukua hatua. Miaka minne mtu aliyokaa Sekondari ingemtosha kukijua Kiingereza fasaha, hata kama hatamfikia Kiranga na Nyani Ngabu.
Kuwa na lugha ya Kiswahili isiwe kikwazo. "English" ndiyo lugha inayoongoza duniani kwa kuwa na waongeaji wengi. Inakadiriwa kuwa na watumiaji bilioni moja na nusu.
Kwa wale ambao Kingereza kilitupiga chenga tulipokuwa masomoni, tusione haya kuchukua hatua za makusudi kujinoa katika uwezo wa kuimudu 'English". Ukiwekeza masaa mawili kwa siku, baada ya miezi sita, hutakuwa kama ulivyo sasa(kama hukijui kwa ufasaha kwa sasa).
Kujitetea hakutusaidii. Tukubali kuwa tulizembea, na tujisahihishe, huku tukivisaidia vizazi vijavyo visirudie makosa yetu.