MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) iko njia panda kutokana na matokeo yaliyotangazwa jana na ZEC kuonesha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) peke yake ndicho chenye haki ya kuunda Serikali.
Ni CCM pekee ambayo mgombea wake wa urais amepata zaidi ya asilimia 10 ya kura na ndiyo imezoa wawakilishi karibu wote na hivyo kubaki chama pekee chenye sifa ya kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.
Mshindi wa pili wa matokeo ya kura za urais ni Hamad Rashid Mohamed aliyeambulia kura 9,734 sawa na asilimia3.
Akizungumzia hatma ya SUK, alisema serikali hiyo itaendelea kuwepo kwani Rais aliyepo madarakani lazima ateue watu kutoka kwenye vyama vya upinzani kuunda serikali hiyo. Alisema kwamba yeye ana matumaini makubwa kuwa Dk Shein atamteua yeye awe makamu wa kwanza wa rais kwa sababu katiba inaelekeza kuwa mshindi anayefuatia kwa kura za urais ndiye mwenye sifa.
Mwanasheria wa ZEC, Issa Khamis alisema kwamba Katiba ya Zanzibar iliyofanyiwa marekebisho inafafanua kuwa mgombea aliyepata kura sio chini ya asilimia 10 ndiye ataingia kwenye serikali hiyo na akaongeza kuwa Katiba hiyo iko kimya kama sifa hiyo haitakuwepo. Alifafanua kuwa kutokana na hali hiyo kuundwa kwa Serikali hiyo kutategemea na maamuzi na utashi wa Rais aliyeshinda kwenye uchaguzi huo.
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai alikiri kuwa kwa kuwa hakuna chama ambacho kimefikisha asilimia 10 ya kura za urais isipokuwa CCM kama inavyotamkwa na Katiba ya Zanzibar.
Vuai alisema serikali ya kitaifa inaundwa kikatiba na kama hakuna chama ambacho kina sifa za kuingia kwenye serikali hiyo ni wazi kuwa hapo uundwaji wake unategemea busara na maamuzi ya Rais aliyepo madarakani.
“Katiba ya Zanzibar inasema chama chenye sifa ya kuingia kwenye serikali ya umoja wa kitaifa kimewekewa kifungu maalum kuwa ni lazima kipate kura za urais walau asilimia 10 kwa matokeo ya leo hakuna chama kilichopata asilimia hiyo isipokuwa Chama Cha Mapinduzi. “Kwa hiyo kwa haraka haraka unapata majibu hiyo maana yake nini na huko mbele katiba hiyo inasema kama hujapata hiyo asilimia 10 basi upate viti vingi kwenye baraza la wawakilishi, lakini katika uchaguzi huu viti vyote vimechukuliwa an CCM.
Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Mtungi alipoulizwa kuhusu maoni yake kama kwa matokeo hayo nini hatima ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa alisema hawezi kuzungumzia jambo hilo. Aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria wa Zanzibar, Awadhi Said, alisema suala la uwepo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni la kikatiba na kwamba muundo na uwepo wake umeidhinishwa kikatiba.
Akizungumza jana kwa simu, alisema katiba inatamka wazi matakwa ya atakayekuwa Makamo wa Kwanza wa Rais lazima apate asilimia 10 ya kura za urais na huo ndiyo msingi wa awali na sio kusubiri busara ya Rais.
Muundo wa SUK
Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) imetamkwa katika Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 Toleo la 2010 Kifungu cha 9(3). Kifungu hicho kinasema “ Muundo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar utakuwa wa Umoja wa Kitaifa na utendaji wa kazi zake, utafanywa katika utaratibu utakaohakikisha kuendelezwa kwa umoja nchini na lengo la kufikia demokrasia”.
Katiba hiyo ilianzisha cheo cha Makamu wa Kwanza wa Rais na Makamu wa Pili na kufuta wadhifa wa Waziri Kiongozi.
Kwa mujibu wa Marekebisho ya 10 ya Katiba, Makamo wa Kwanza wa Rais atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama cha siasa kilichopata nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa Rais.
Kifungu cha 39(3) cha Katiba hiyo kinasema kuwa Makamo wa Kwanza wa Rais atatakiwa awe na sifa za kumwezesha kuchaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi ; na atateuliwa na Rais baada ya kushauriana na chama kilichopata nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa Rais, kama chama hicho kilichopata nafasi ya pili katika matokeo ya kura ya uchaguzi wa Rais, kitapata asilimia kumi ya kura zote za uchaguzi wa rais.
Katiba hiyo inasema Makamu wa Pili wa Rais atateuliwa na Rais kutoka miongoni mwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka katika chama cha siasa anachotoka Rais.
Kwa hisani ya habarileo