Paul Makonda awataka Geita Gold Mining kuhakikisha Fedha za CSR wanazotoa kwa ajili ya jamii zinafika kwa walengwa ambao wengi wao ni walala hoi

Doubleclick

Member
Apr 26, 2024
41
18
IMG-20240502-WA0026.jpg
Makonda aisisitiza GGML kuhakikisha CSR inabadilisha maisha ya wana-Geita
-
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ametoa wito kwa Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kuhakikisha fedha zinazotolewa na kampuni hiyo kutekeleza miradi mbalimbali ya kijamii (CSR) zinagusa na kubadilisha maisha ya wananchi wa mkoa wa Geita na Tanzania kwa ujumla.

Mbali na kuipongeza GGML kwa kuja na tenolojia mbalimbali za uokoaji katika maonesho ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa kazi (OSHA) yanayoendelea kwenye viwanja vya General jijini Arusha, pia alieleza kuridhishwa na elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu masuala ya afya na usalama mahali pa kazi.

Makonda ambaye alitembelea banda la GGML katika maonesho hayo jana alisema mara nyingi maisha ya watu wa Geita hayafanani na utajiri uliopo katika mkoa huo.

“Mimi sioni aibu kuitwa tajiri, kwa sababu hilo ni jambo la kujivunia hivyo siwezi kujivunia umaskini ndio maana nataka ninyi Watanzania mliopo kwenye mgodi huu kuendelea kuwa chanzo cha mabadiliko ya watanzania wenzenu wanaozunguka mgodi huu,” alisema.

Aidha, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi alimpatia maelezo Makonda kwamba mpango wa CSR wa mwaka huu ni mwendelezo wa mipango ya awali unaolenga kujumuisha maendeleo yaliyofikiwa na GGML hadi sasa katika maeneo ya mazingira, miundombinu, afya, elimu na biashara ndogondogo na za kati (SMEs) katika jamii ya mwenyeji wa Geita.

Dk. Kiva alitoa mfano kuwa mwaka jana GGML imesaini Mkataba wa Makubaliano (MoU) na wenyeji wake Halmashauri ya Mji Geita, Wilaya ya Geita pamoja na Halmashauri za jirani za wilaya za Chato, Bukombe na Mbogwe kutekeleza Mpango wa Uwajibikaji wake kwa Jamii (CSR) kwa mwaka 2022/2023 wenye thamani ya Sh bilioni 19.

“Jumla ya Sh bilioni 9.8 zilitengwa kwa ajili ya Halmashauri ya Mji wa Geita ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Geita, bajeti ya Sh bilioni 8.6 ilitengwa," amesema.
 
Makonda hana shape kama maji,kila utakapomuweka anafit.

Tukiweka kando mapungufu mengine,bado ni mtu ambaye angarau akiwepo sehemu kama kiongozi,utahisi uwepo wake.
 
Hii ngoma bado ngumu sana, Jamaa apewe uPM next time
Makonda Bomayee.

Anasema Utajiri ni mzuri
😅😅🙏

Nyerere alisemaga kama mtu anataka utajiri ni sawa ila kwanza atuachie ofisi yetu ili akautafute utajiri kwenye Biashara na akalipe kodi inayostahili 😅😅🙏 !
 
Back
Top Bottom