Omari Makoo
Member
- Sep 6, 2016
- 78
- 39
Na Omari Abdallah Makoo
Profesa Ibrahim Lipumba ambae anatajwa kuwa msomi wa kipekee mwenye CV nchini(full bright professor) .Profesa Lipumba ni miongoni mwa wanasiasa wakongwe nchini Tnzania ambaye amedumu kwenye siasa tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka1992.
Aliiongoza CUF kutoka kuwa chama cha pili kwa nguvu Tanzania nyuma ya NCCR MAGEUZI mwaka 1995 mpaka kuwa cha kikuu cha wapinzani mwaka 2000.
Profesa Lipumba amegombea nafasi ya uraisi katika uchaguzi mkuu Tanzania mara nne(yaani mwaka 1995,2000,2005 na mwaka 2010).Mara zote nne kura zake hazikutosha kumfanya kuwa rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwenye utawala wake kama mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF taifa mwaka 2005 CUF ilipata wabunge wa kuchaguliwa na wananchi 19 kwa Zanzibar na kuambulia sifuri kwa Tanzania bara.
Mwaka 2010 walipata wabunge waliopigiwa kura na wananchi 22 kwa Zanzibar na 2 kwa Tanzania bara.
Pia kwa Tanznaia bara walipata madiwani 96 kwa mwaka 2005 na kusonga mbele mpaka kufikia madiwani 152 kwa mwaka 2010.
Hivyo mwaka 2010 ndio chama pekee kilichopata wabunge katika maeneo yote matatu ya Tanzania yaani Bara,Unguja na Pemba.Huku CHADEMA wakipata wabunge bara pekee yake na CCM wakipata wabunge Bara na Unguja pekee.
Hivyo 2010 CUF kilikuwa ndio chama pekee cha wapinzani chenye wabunge wengi wa kuchaguliwa na wananchi yaani wabunge 24 kikifuataiwa na CHADEMA waliokuwa na wabunge 20 wa kuchaguliwa na wananchi.
Mafanikio ya Profesa Lipumba kwenye chama cha wananchi CUF yanaonekana wazi kabisa hata kwa aliyefumba macho.
Tarehe 6 Mwezi wa nane mwaka 2015 Profesa Ibrahim Lipumba aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake ya uwenyekiti CUF na kubakia kuwa mwanachama wa kawaida.Hii ilikuja baada ya kukerwa na hatua ya umoja wa katiba ya wananchi(UKAWA) ambao CUF ni chama shiriki kushindwa kusimamia makubaliano yaliyopelekea kuundwa kwa umoja huo.
Profesa Ibrahim Lipumba alisema UKAWA ilianzishwa kwenye rasimu ya katiba pendekezwa iliyowasilishwa kwenye bunge maalumu la katiba,Hivyo nafsi yake inamsuta kuendelea na uongozi hukuwaliokuwa wanaipinga rasimu ya katiba ya Jaji Warioba wakikaribishwa kuwania uongozi wan chi kupitia umoja huo.
Tarehe 14 mwezi wa sita mwaka 2016 taarifa za Profesa Lipumba kutaka kurejea kwenye nafasi yake ya uwenyekiti taifa zilianza kusikika kwenye vyombo mbali mbali vya habari pamoja na mitandano ya kijamii.
Profesa Lipumba alisema amechukua maamuzi hayo baada ya barua zake za kutaka kujiuzulu kutojibiwa lakini pia kuombwa na wanachama wa CUF pamoja na kushauriwa na wadau mbali mbali kurejea kwenye kiti chake cha Uenyekiti.
Tarehe 28 mwezi wa nane mwaka 2016 ndio tarehe ambayo ilikuwa inatarajiwa CUF kufanya uchaguzi wa mwenyekiti mpya.Tarehe 21 ya mwezi nane mwaka 2016 CUF walifanya mkutano mkuu ambao huudhuliwa na wajumbe takribani 800 kwa nchi nzima.
Profesa Lipumba nae aliibuka kwenye mkutano huo ambao hakua amelikwa kama anavyothibisha mmoja ya wanakamati ya maandalizi na mapokezi Mbalala Maharagande kwenye Azam tv tarehe 22/8/2016 majira ya saa mbili na nusu usiku kwenye mahojiano ikiwa kama sehemu ya taarifa ya habari ya Azam.
M/kiti wa muda wa mkuatano huo Julius Mtatiro ambaye mara kadhaa ameonyesha msimamo wake dhidi ya Profesa Lipumba kwenye mitandano ya kijamii aliwataka wajumbe wa mkutano mkuu kupiga kura ya wazi ili kutoa maamuzi ya kukubaki kujiuzuru kwa Lipumba au kukataa kama katiba ya CUF ibara ya 117 inavyoeleza.
Hivyo aliruhusu wapige kura kwa kunyoosha mikono,wajumbe 476 walikubali profesa ajiuzulu huku wajumbe 14 pekee wakitaka profesa Lipumba aendelee na uwenyekiti taifa.
Hata hivyo akidi ya mkutano huo inatiliwa mashaka na baadhi ya wapenzi wa chama hicho kwani wajumbe wa bara walikuwa wachache sana ukulinganisha na wale wa Zanzibar.
Ukimpima Profesa Lipumba kwa misimamo yake iliyompelekea kujiondoa kwenye uwenyekiti CUF hapo awali basi chama pekee amabacho ni mujarabu kwake ni ACT WAZALENDO amabacho kimejipambanua kwa kupinga ufisadi na kujikita kwenye siasa za maendeleo na uatawala bora kwa kurejesha azimio la Arusha katika mtindo mpya(yaani Azimio la Tabora).Azimio hilo limerejesha miiko ya uongozi ikiwa ni sehemu ya kusimamia maadili ya viongozi.