Mzao wa Tippu Tip uko wapi?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,816
Ikumbukwe kwamba wakati wa Biashara ya Utumwa ni Waafrika wenzetu ndiyo waliokuwa wanakamata ndugu zetu kama Watumwa na kuwauzia Waarabu na Wazungu mmoja wao ni mtu maarufu Mchotara Tippu Tip ambaye alikuwa ni Mchotara wa Kiarabu na Kikwetu!
Mama yake Tippu Tip alikuwa ni Mbantu mweusi kama mimi na ni Mzaliwa wa Dar yetu kipindi hicho haikuitwa Dar wakati Baba yake ni alikuwa ni Mwarabu wa kuapia kutoka Oman, huyu ndiyo alikuwa kinara wa kutuuuza Waafrika, sasa swali langu ni Je, mzao wake Tipp Tip uko wapi?
Kwa maana Tipp Tip alioa wake wengi na watoto wengi sana tu hivyo ina maana kizazi chake kipo na kwa kuwa alikuwa ni tajiri, utajiri alioupata kwa njia haramu ya kuuza Watumwa basi aliurithisha kwa vizazi vyake vilivyofuatia, sasa viko wapi vizazi vyake?

Muuza watumwa Maarufu Afrika Mchotara Tippu tip!

images

Kazi ya Tippu Tip!

Islams+african+slaves.jpg

Mkuu Barbarosa sehemu ya ukoo wa huyu jamaa wapo sehemu moja Tabora inaitwa "Kwihala".Ni nje kidogo ya mji wa Tabora,njia ya kwenda Sikonge karibu na Seminary Kuu ya Kipalapala ya Kanisa Katoliki iliyojengwa toka miaka ya 1880's.

Huku Kwihala ndio ulikuwa mji wa zamani wa Tabora,kabla ya watu kusogea kuifuata reli ya Kati ya kwenda Kigoma,Mwanza na Mpanda.Lkn mji haswaa ndio huku Kwihara ambapo unamkuta Mzee Nassoro Mwarabu ambaye ni ukoo wa Tippu Tipu.

Na ukifika pale Tabora,hawa Waarabu Ukoo wa Tippu Tipu wanafahamika kama "Waarabu wa Kwihala".Pembeni ya hiki kijiji chao,kuna Makumbusho ya Kale,ambapo unakuta historia ya kina Livingstone,Henry Stanley,Wamisionary wa Holy Ghost Fathers ambao kwa mara ya kwanza wanafika Unyanyembe walipokelewa na hawa Waarabu wa Kwihala.

Eneo hili kuna miembe mingi sana,kuna maembe aina ya boribo na embe dodo.Miembe hii ni miembe "pori" maana haina mmiliki zaidi ya mtu yoyote kuchuma na kula.Miembe hii ilipandwa miaka ya 1880's ikiwa na lengo ya kutumika kama kiashiria cha njia ya kutoka Unyanyembe mpaka Ujiji-Kigoma kutokea Kalambo.

Wapagazi na Waarabu kila walipopita,ili wasisahau njia wakati wa kurudi walipanda miembe,ili wakati wa kurudi waitumie kama "Routes" za kufika.Na kumbuka safari wakati huo ilikuwa inachukua miezi hadi miaka.Ndio maana hata mkoloni toka Tabora mpaka Ujiji,alijenga reli akifuata miembe iliyopandwa na Mwarabu wa Kwihala ambapo ilikuwa sehemu ya makazi ya mke wa Tippu Tipu.
 
Asante sana kwa maelezo na somo zuri sana, je vipi hali yao ya Kiuchumi kwa sasa si ni lazima watakuwa matajiri sana?
 
Imekaa poa sana.
Barafu wewe Mwarabu wa Kayenze?
 
Imekaa poa sana.
Barafu wewe Mwarabu wa Kayenze?
Mkuu platozoom sasa hawa Waarabu wa Kwihala wamechoka kama walivyochoka wale Waarabu wa Kayenze Mwanza,unaopanda nao magari ya Igombe wakati wewe unashukia kwenu Iloganzara.Mwanza mnawaita Waarabu Koko.

Hivyohivyo ndio kwa wale wa Tabora...mkuu Barbarosa hawa jamaa wamechoka sana.Biashara zao ni mkaa wanachoma na kuleta mjini Tabora.Pia wanashughulika na kulima kilimo cha hapa na pale!Ukiwaona ni weusi tiii lkn wana nywele za "kiarabu".

Ni wauzaji wazuri wa Uyoga pori,maembe boribo na na dodo.Nafikiri mabadiliko ya uchumi wa dunia yaliwaacha kando.Wamebaki jina tu
 
Mkuu nina bahati mbaya sijawahi kulala Tabora zaidi ya siku moja.

Nikipata fursa nitapita Kwihala nijifunze Historia. Hivi hawawezi kuwa na nyaraka za Babu yao hata kidogo?

Halafu Tabora ni maarufu kwa black mamba. Ukiniambia wapo sipiti!
 
loh salaaaale....
 
Kwa maisha yale sidhani kama wametunza.Mahali pazuri pa kupata historia ya huyu bwana na kwa Majirani zake Kipalapala Seminary,pale wana mpaka nyaraka za makabidhiano ya kuuziana/kupeana eneo la kujenga Seminary na kanisa miaka ya 1880's.
 
Mkuu Barafu...umedadavua vyema,ila hiyo miembe si pori bali Mjerumani aliwalazimisha wazee kupanda kwani maeneo hayo ni karibu na Boma la Mjerumani na Shule ya Tabora School.Makazi ya Kwihara ni ya Mtemi wa Unyanyembe Fundikira. Ni kweli yawezekana Kumbukumbu za Tiputipu zikawepo seminary ya Kipalapala.

Maeneo ya Kwihala kuelekea Sikonge kulikuwa na "Wanangwa'' waliojihusisha na biashara ya watumwa na Titputipu huku wakilipwa vioo,nguo,bangili nk..kama pesa ya kununulia watumwa.

Umeeleza vema.
 
Ikumbukwe kwamba wakati wa Biashara ya Utumwa ni Waafrika wenzetu ndiyo waliokuwa wanakamata ndugu zetu kama Watumwa na kuwauzia Waarabu na Wazungu mmoja wao ni mtu maarufu Mchotara Tippu Tip ambaye alikuwa ni Mchotara wa Kiarabu na Kikwetu!
Mama yake Tippu Tip alikuwa ni Mbantu mweusi kama mimi na ni Mzaliwa wa Dar yetu kipindi hicho haikuitwa Dar wakati Baba yake ni alikuwa ni Mwarabu wa kuapia kutoka Oman, huyu ndiyo alikuwa kinara wa kutuuuza Waafrika, sasa swali langu ni Je, mzao wake Tipp Tip uko wapi?
Kwa maana Tipp Tip alioa wake wengi na watoto wengi sana tu hivyo ina maana kizazi chake kipo na kwa kuwa alikuwa ni tajiri, utajiri alioupata kwa njia haramu ya kuuza Watumwa basi aliurithisha kwa vizazi vyake vilivyofuatia, sasa viko wapi vizazi vyake?

Muuza watumwa Maarufu Afrika Mchotara Tippu tip!

images

Kazi ya Tippu Tip!

Islams+african+slaves.jpg

Huyo nae chotara?
 
Mkuu Barafu...umedadavua vyema,ila hiyo miembe si pori bali Mjerumani aliwalazimisha wazee kupanda kwani maeneo hayo ni karibu na Boma la Mjerumani na Shule ya Tabora School.Makazi ya Kwihara ni ya Mtemi wa Unyanyembe Fundikira. Ni kweli yawezekana Kumbukumbu za Tiputipu zikawepo seminary ya Kipalapala.

Maeneo ya Kwihala kuelekea Sikonge kulikuwa na "Wanangwa'' waliojihusisha na biashara ya watumwa na Titputipu huku wakilipwa vioo,nguo,bangili nk..kama pesa ya kununulia watumwa.

Umeeleza vema.
Asante kada Wakudadavuwa ndio maana niliandika "pori" nikiwa na maana si pori haswaa,bali ilipandwa miaka mingi kiasi imekuwa kama msitu na hakuna mwenye nayo.

Eneo lote hilo likiitwa "Kazeh" likianzia eneo ilipo Hospital kongwe ya Karunde,unapita BOMANI ambapo sasa ndio makao makuu ya Jeshi Bregedia ya Kanda ya Magharibi,unashuka lilipo gereza la Tabora Mjini,Halafu shule za Sekondari za Tabora Schools zilizojengwa na Mjerumani...Moja ikiitwa Berlin(Tabora Boys) na nyingine ikiitwa Warsaw (Tabora Girls) kuna shule ya Msingi Kazeh Hill na baadae ukishuka kidogo unakutana na Seminary ya Kipalapala na Mashariki ya Seminary ni uwanja wa ndege wa Tabora ambao wakati wa vita ya kwanza na ya pili ulitumika sana kwa ndege kutua.

Kumbuka Tabora ndio ilikuwa "Administrative Centre" ya Mjerumani,baada ya yeye kufika na kukuta Arabs Traders wameikamata Unyanyembe na kufanya biashara nzuri kati ya pwani na Bara ya Tanganyika mpaka Congo na Zambia.Hapa ndipo Mjeruman akaamua kujenga reli na kufanya kitovu kikuu cha usafiri.Ndio maana karakana kuu ya reli ilikuwa Tabora(Wakati huo reli ndio njia kuu ya usafiri).Mtu hawezi kwenda Mwanza,Kigoma,Mpanda bila kupita Unyanyembe.

Tippu Tipu na vizazi vyake wakaishi hapo Kwihala....wakiwa ndio "conteoller" wa biashara zooote za kutoka pwani kwenda bara,na kinyume chake.Pitia hapa kidogo

Historical information.
Kwihala is a historical site; a center where Slaves were assembled from the Congo, Burundi, Rwanda, and Western Tanganyika (now Tanzania). It was a stop-over as arrangements were made to take the slaves to Bagamoyo and Zanzibar on the way to Europe and other parts of the world.
It is in this area where Stanley met Dr David Livingstone as he was trying to find out the origin of the Nile. Dr David Livingstone was on the way to Ujiji along the shore of Lake Tanganyika in the 1800s.
Dr Livingstone lived in a hut previously inhabited by an Arab slave trader, which was constructed at Kwihala in the 1800s. Since Tabora (originally called Kazeh) is not a tourist destination few know about this historical location."

Mzee Mohamed Said atatusaidia,maana licha ya kuwa ni mzaliwa wa K'koo,lkn huyu ni "mtoto" wa Ujiji...
 
Back
Top Bottom