Anonymus
Member
- Sep 2, 2014
- 12
- 52
Habari wana JF, ni matumaini yangu wote mko sawa, nadhani hii ni mara ya kwanza kupost hapa ubaoni ninaombeni msaada maana nimeshindwa hata kulala yaani.
Labda nielezee hivi, sisi ni wakristo, mzee alioa na kuzaa watoto 3 na bi mkubwa, huyu mama walichuma mali nyingi sana (nyumba, magari, viwanja na maduka kadhaa) na kwakweli maisha yalikuwa fresh.
Alipofariki bi mkubwa mzee akaoa tena ndipo kuzaa hawa wa3 wengine, ila kwa bahati mbaya mambo yalianza kuporomoka na vitu vingi sana vikauzwa kiasi kwamba alipoingia bi mdogo vilinunuliwa viwanja vipya viwili tuu lakini vingi vilivyokuwepo enzi za bi mkubwa viliuzwa. Zikiwemo nyumba na magari yaliuzwa pia.
Sasa ikatokea bi mdogo naye akafariki, ukapita mwaka naye mzee akafariki, na taratibu za usimamizi wa mirathi zikafanyika na kuchaguliwa kaka mkubwa kusimamia. Makubaliano ilikuwa tutaendelea kuishi pamoja kama familia ukizingatia asilimia kubwa walikuwa ni wanafunzi hivyo hatukutaka mambo ya kugawana.
Tumeishi hivyo toka hapo na sasa wote tuko mtaani baada ya kumaliza masomo.
Ishu inakuja kwa baadhi yetu maisha yamekuwa magumu, watoto wa bi mdogo wanaraise na kutaka mali zigawanywe.
Sasa swali langu ni jee, mgawanyo huo unakuwaje? Je mali zilizochumwa kipindi cha bi mkubwa zinabaki kwa watoto wa bi mkubwa au mali zote zinagawanywa sawa bila kuzingatia zilichumwa lini?
Sio mwandishi mzuri sana japo nimejitahidi kueleza, kama sijaeleweka pahala nitajibu kwa comments.
Ninatanguliza shukrani zangu kwenu