Mzalendo120
JF-Expert Member
- Jul 2, 2022
- 1,603
- 2,089
Eti mbunge huyo wa Bunda vijijini Boniface Mwita Getere anasema wanachuo wasipewe boom kwani wanafunzi wanaopewa boom hawana nidhamu, niwalevi, na hawasomi.
Anadai eti walipiwe karo tu kuhusu matumizi watalipiwa na wazazi wao. Sasa hajajua kama hakuna wazazi ambao hawana uhakika wa kula? Hajajua kama huo ni mkopo sio msaada? Hajajua kama bado boom nikidogo wanavyuo wanaomba waongezewe?
Hivi amesoma chuo huyo mbunge au amesoma shule za bweni? Au anataka wanachuo wachemshiwe mihogo na chai rangi kama wanafunzi wa boarding? Mbona wapo wanafunzi ambao wanawasaidia ndugu zao kwa hilo boom, je mbona hajawatambua? Ameonesha chuki kubwa kwa watanzania wenzake
Je, hakuna wabunge walevi? Hakuna wabunge ambao hawana nidhamu? Hakuna wabunge ambao wanasinziatu kwa mujibu wa aliyekua RC wa DSM kipindi cha nyuma? Mbona tunaona wabunge marakadhaa wakinyamazishwa waache kelele bungeni? Hawaoni kama wanaonekana na wananchi?
Nimara ngapi wanapitisha miswada inakua sheria mfano mambo ya tozo na muda kidogo wakaondoa? Sio kama walichemka? Mbona hawajawahi kutuomba radhi?
Kwani yeye hela anazolipwa kama mbunge hakuna ziada? Mbunge huyo amejiaibisha, ameishusha hadhi yake na amewavua ngua wapigakura wake. Nashawishika kusema hafai tena kurudi bungeni.
Maelezo kidogo ya muwakilishi wa wananchi wa Bunda vijijini hayo hapo chini
Pia soma Mbunge Getere: Boom lifutwe, wanafunzi wanatumia kulewea