JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,227
- 5,265
Tunaomba ushauri wenu, kwa wale ambao specialists wa magonjwa haya ya ngozi. Tunauliza hivi kwa niaba ya watu wengi ambao wamekuwa wanahangaika kupata suluhu ya matatizo haya ya Mba, Fangasi na mabaka (hasa kwenye sehemu za siri, yakiwemo mapaja).
Shukrani
Tafadhari tunaomba ushauri wenu:
A. Kuhusu Fungus za sehemu za siri:
Zinatibiwa vipi au na dawa gani? Mdau anadai amefanya yafuatayo mpaka sasa:
1. Kunyoa muda wote
2. Kukausha vizuri kwa taulo baada ya kuoga
3. Kutumia gentriderm ya kupaka.
Na ameona kuwa akitumia gentriderm zinapona lakini baada kama ya wiki zinarudi.
B. Mabaka:
Je, kuna dawa ya mabaka ya usoni, mgongoni, kifuani na sehemu nyingine za mwili?
C.Mba:
Dawa ya mba please? (Tunafahamu kuna mjadala juu ya MBA tu hapa => Ujue ugonjwa wa Mba na Tiba yake
NB:
Kwa kila moja ya dawa utajazo hapo juu tuambie kama mtoto anaweza kutumia, na kama hawezi; ni umri gani unashauriwa?
Je, kwa magonjwa hayo kuna dawa za mitishamba pia, ni zipi, zinatumikaje na dosage yake ikoje.
===
BAADHI YA WADAU WALIOULIZA KUHUSU TATIZO HILI
---GOOD DAY ALL,
Habari ya week end members. Ninaomba kujuzwa dawa na matibabu ya tatizo la fungus (any kind of fungus) au kama kuna specialist wa hili eneo mnijulishe.
Binafsi ninatatizo la fungus ambao nikitumia dawa wanapotea wote na it takes about a month or two tatizo linajirudia. Nimetumia dawa nyingi na mara nyingi tu.
Msaada jamani.
---Wanajamvi heshima kwenu,
Mimi nilisumbuliwa na fangas kwa muda mrefu sana kwenye sehemu za siri, lakini namshukuru mungu nimepona ila wakati naumwa mapaja yangu yalibadilika na kuwa meusi sana mpaka yanakawa yanatisha sana ila kadri siku zinavyosonga yanaanza kubadilika.
Sasa, naja kwenu JF Doctors kwa ushauri wenu kuwa nawezaje kupata dawa ya kupaka ya kuweza kuondoa huo weusi?
Nitashukuru sana wandugu endapo nitafanikiwa kwa hili
---Habari JF DOCTORS,
Nisaidieni kwa mda sasa nimekuwa nikisumbuliwa na ugonjwa wa fangasi ya makende kiasi kwamba yakianza kuwasha ni shidaa yanawaka ka moto vile.
Nshajaribu sabuni za rungu, protector, na detal ya maji lakn sijapona.
Jamani, msaada kwa anayejua dawa ya hili tatizo manake linanikosesha raha kwakweli.
Wadau habari za leo, nina kabiliwa na changamoto ya muda mrefu ya fangasi sehemu za siri hasa kwenye corodani, nimetumia dawa za kumeza na kupaka lakini tatizo halijakoma. Je, kuna dawa nyingine ambayo naweza kutumia ili nipone maana zinawasha na kuleta harufu sio nzuri...
Nawasilisha
===
MASWALI MUHIMU:
===Wataalam naomba kuuliza maswali saba (7) ambayo kwa muda mrefu nimetafuta MAJIBU YA UHAKIKA bila mafaniko.
Naamini wataalamu wetu wa JF mtanisaidia:-
1. Je kitaalamu kuna aina ngapi za fangus? Aina hizi zinatambulika kwa dalili tofauti?
2. Naomba kufahamishwa kama matibabu yake hutofautiana kwa mwanamke na mwanamume.
3. Je, mikorogo kwa wakina-dada huweza kusababisha mashambulizi ya fangus?
4. Dawa za Fangus (tube ama unga) zipatikanazo kwenye Pharmacy zetu zaweza kutumiwa popote penye fangus? Eg hata ukeni/uumeni? na jinsia yoyote?
5. Mwanamke akitumia ya unga/au ya kupaka pana madhara gani kama itaingia mpaka ukeni? Kuna angalizo lolote?
6. Vagina PH inaweza kwa namna yoyote kusababisha fangus kwa mama na dada zetu?
7. Mtu aliyetumia hizi tube almost zote na nyingi kati ya Pawder anashauriwa atumie dawa gani? (Kuna vidonge au sindano?) ambavyo ni effective zaidi?
Majibu yako yatasaidia wengi, hivyo kwa niaba yao na mimi mwenyewe, naomba kutanguliza shukurani kwa wataalam wetu.
UFAFANUZI WA KINA WA TATIZO HILI
Fangasi sehemu za siri kwa WanawakeInapotokea wale wadudu wanaomlinda kuwa wengi sana ukeni badala ya kulinda mwili hugeuka na kuanza kushambulia na mwisho dalili hujitokeza na ndipo hapo tiba huwa inahitajika haraka sana ili kuzuia madhara mengine.
Kuna baadhi ya sababu zinazo sababisha fangasi kutokea ukeni na sababu hizo ni kama ifuatavyo:
Kutumia dawa za antibayotiki mara kwa mara na kwa muda mrefu, husababisha fangasi kwani dawa hizo huua wadudu wote wanaolinda mwili na kuacha uke ukiwa hauna kinga. Dawa za antibayotiki ni kama, Ampicillini, Amoxylline, Ciproflaxine, Doxylline, Erythromycine, Gentamcycine na nyingine nyingi hivyo basi, jamii isitumie ovyo dawa za antibayotiki bila ushauri wa daktari.
Sababu nyingine ni unene kupita kiasi. Mtu akinenepa anaweza kupata fangasi kwasababu unene husababisha jasho sehemu za siri nakuongeza unyevunyevu sehemu hizo pia michubuko kutokana na kubanwa na nguo ya ndani. Sababu zingine ni utumiaji wa dawa ya jamii ya steroid, dawa hizi ni kama Prednisoline, Hydrocortisone Dexameltasone na nyingine nyingi. Hizi nazo hupunguza kinga ya mwili na kusababisha fangasi kuzaliana kwa wingi.
Pia kuna magonjwa yanayosababisha kupungua kwa kinga nayo ni kisukari, Ukimwi na magonjwa mengine yanayopunguza kinga ya mwili na kusababisha magonjwa nyemelezi.
Kuwepo na joto kupita kiasi na kuvaa nguo za ndani ambazo hazijakauka pia husababisha fangasi sehemu za siri.
Sababu ni nyingi na hatuwezi kuzitaja zote.
Dalili
Dalili hutofautiana kutokana na mtu na mwingine ila dalili kubwa ni kutokwa na majimaji meupe wakati mwingine kama mgando wenye rangi ya njano ukiwa umeambatana na muwasho sehemu za ndani au kwenye mashavu ya sehemu za nje za siri.
Nje ya sehemu hizi za siri hutokea wekundu na maumivu wakati wa kukojoa au wakati wa tendo la ndoa.
Pia mgonjwa atajikuta akikojoa mara kwa mara. Tiba na ushauri Fangasi hutibika vizuri nakupona ila ni vizuri ukaenda hospitali na kufanyiwa kipimo cha mkojo ambapo chembechembe za yeast huonwa vizuri kwenye darubini. Lakini pia wapo ambao wanatambua kabsa kuwa wanasumbuliwa na fangas tena sugu.
Baada ya kupima ukigundulika una fangasi sehemu za siri au sehem nyingineyo mwilini wasiliana nasi tukupatie tiba yenye uhakika.
Fangasi Sehemu za siri kwa upande wa Wanaume
Watu wengi wanaamini kuwashwa sehemu za siri kunasababishwa na fangasi tu, ndiyo maana nimepata maswali ya wasomaji juu ya matibabu na jinsi ya kujikinga na fangasi kwa kuwa wanaamini muwasho unaowasumbua kwa muda mrefu ni matokeo ya maambukizi ya fangasi.Watu wanapaswa kufahamu kuwashwa sehemu za siri kunaweza kuwa dalili ya maradhi fulani ndani ya mwili wako pengine isiwe ni fangasi na ikawa ni mzio (allergy) tu.
Mara nyingi muwasho sehemu za siri unaosababishwa na kitu huisha wenyewe kitu hicho kikiondolewa. Kuondolewa kwa kitu hicho kunatia ndani matibabu sahihi na kuendelea na njia bora za kujikinga kutopata maambukizi tena. Vitu vingine vinavyosababisha muwasho huhitaji matibabu ya hali ya juu zaidi. Ikiwa unawashwa kwa muda mrefu ni vyema kuzungumza na daktari. Kukaa na ugonjwa kwa muda mrefu kunaweza sababisha ugonjwa kusambaa mwilini na kuongeza hatari ya kifo.
Nini husababisha Muwasho Sehemu za Siri za Mwanaume?
Kuwashwa uume au sehemu zingine za siri za mwanaume husababishwa na sababu zile zile zinazosababisha muwasho sehemu nyingine za mwili.
Maradhi ya fangasi husababisha muwasho kwa wanaume wengi, sababu nyingine ni kama ugonjwa wa upele (scabies), kuwepo kwa chawa, mzio na maambukizi mengine ya bakteria. Maambukizi hasa ya magonjwa ya zinaa ndio chanzo kikuu cha kuwashwa uume.
Fangasi sehemu za siri za mwanaume ni nini?
Maradhi ya fangasi (Candidiasis) husababishwa na vimelea viitwavyo Candida albicans. Vimelea hivi hushambulia jinsia zote ingawa hushambulia sana jinsia ya kike kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu kitu kinachosababia wao kuathiriwa zaidi.
Watu wengi wana vimelea hivi katika miili yao kwa kiwango kidogo sana. Kinga ya mwili ikisaidiwa na bakteria walinzi wa mwili huweza kupambana na vimelea hivi.
Mwanaume anapataje fangasi sehemu za siri?
Mtu anapokunywa dawa za kuua bakteria kutokana na ugonjwa mwingine wa bakteria kama kuhara damu, husababisha bakteria walinzi wa mwili kufa, hivyo kuongeza hatari ya mwili kushambuliwa na ugonjwa wa fangasi.
Ikiwa kinga yako ya mwili itashuka kutokana na maradhi kama VVU/UKIMWI au lishe duni pia mwili wako utakuwa katika hatari zaidi ya kupata maradhi ya fangasi.
Hata hivyo, maradhi ya fangasi yanaweza kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine kwa kuchangia nguo au vifaa vya kuogea na kujamiana na mtu mwenye ugonjwa wa fangasi.
Wanaume wengi wanaosumbuliwa na fangasi sehemu za siri huishi maeneo yenye joto sana kama Pwani, Lindi, Mtwara, Tanga na Dar es salaam.
Kuishi sehemu yenye joto pamoja na kuvaa nguo za kubana hasa zisizo tengenezwa na pamba kwa asilimia 100 kunafanya sehemu za siri kuwa na unyevunyevu, hivyo kutengeneza mazingira mazuri kwa fangasi kuzaliana na kuongezeka.
Dalili za fangasi sehemu za siri za mwanaume ni zipi?
Sehemu za siri za mwanaume hata ndani ya uume, korodani, eneo katikati ya makalio na kuzunguka korodani hadi kwenye mapaja huathirika na ugonjwa wa fangasi.
Kichwa cha uume hubadilika na kuwa chekundu na kuwasha. Ngozi inayozunguka sehemu za siri huwasha, kukakamaa na kutoa majimaji ambayo hutoa harufu mbaya.
Matibabu ya fangasi sehemu za siri za mwanaume ni yapi?
Ikiwa una dalili za ugonjwa wa fangasi ni vyema kufika kwa daktari kwa ajili ya matibabu na ushauri zaidi.
Kutumia dawa bila ushauri wa daktari kunaweza sababisha kutopona kabisa, kutopona vizuri au ugonjwa kujirudia baada ya siku chache, pia vimelea vinaweza kujenga usugu wa dawa.
Kumwona daktari kutasaidia kujua kama una maradhi mengine yanayosababisha upate fangasi sehemu za siri.
Ugonjwa wa fangasi usipotibiwa husambaa kwenye damu na kusababisha madhara makubwa mwilini kama kwenye ubongo na mapafu.
Mwanaume atajikinga vipi na fangasi sehemu za siri?
Ili kusaidia kuepuka kupatwa na fangasi sehemu za siri ni vyema kuosha vizuri uume, na kwa wale ambao hawajatahiriwa wanapaswa kuosha kwa umakini zaidi hadi sehemu za ndani za govi.
Ziweke sehemu zako za siri pamoja na ndani makalio katika hali ya usafi na ukavu, kwa maana unyevunyevu unaweza sababisha maambukizi.
Matumizi ya poda maalumu yanaruhusiwa hasa kipindi cha joto kali ili kuzuia unyevunyevu.
Vaa nguo isiyobana sana, iliyotengenezwa kwa vitu asilia kama pamba. Badili nguo ya ndani (chupi) angalau kila siku na vaa kondomu kila unapofanya ngono na mwanamke usiyejua hali yake kiafya kwa ujumla.
===
BAADHI YA WATU WALIONUFAIKA NA USHAURI WA WADAU:
---Wadau,
Napenda kutanguliza shukrani za dhati kwenu nyote nimepona ugonjwa wa fungus wa mwili niliokuwa nao kwa muda takribani miaka 12.
Nimetibiwa hospital ya masista Kawe unashukia kituo kinaitwa Kanisani kama ukipanda daladala.
Jaribu nawe kama una tatizo kama langu thanks so much JF
---Ushuhuda: Ndimu dawa nzuri ya fangasi
Salaam wadau,
Kwa kweli JF imekuwa na msaada mkubwa sana kwangu binafsi. Nimejifunza vingi hapa.
Mojawapo ya mambo mazuri niliyojifunza hapa ni dawa ya kutibu fungus za sehemu za siri za wanaume. Sehemu iliyojibana kati ya mapaja na mfuko wa korodani. Niseme ukweli nimwtumia dawa nyingi sana lakini tatizo likawa linapona na kurudi.
Nilipoingia hapa kutafuta dawa nikakutana na maoni ya watu wakisema ndimu au limao ni dawa pia. Ukweli nilipoitumia ilinichukua siku 7 tu kupona. Ni sawa na ndimu 7 tu nilizonunua kwa bei ya sh 100 kila moja. Napata kipande asubuhi na kipande jioni.
Hakuna muwasho tena, hakuna kunuka tena, hakuna kubadilika rangi ya makende wala kutokuwa na confidence siku ukiwa faragha na mwenza.
Jamani nashauri dawa ya bure kabisa unapona. Si gharama na ni rahisi kutumia na inapatikana kila mahali. Sasa nimejiweke ulinzi wa kupaka kila week angalau mara 2 kuhakikisha hazirudi tena kabisa.
Zingatia: usafi ni muhimu sana na epuka unyevu nyevu wa aina yoyote. Ikiwezekana anika taulo lako juani kila baada ya kuoga. Au tumia taulo kavu muda wote.
Kama unatatizo la Fangasi za Muda mrefu au Muda mfupi kwenye Nyeti zako (Corodani, Mapaja, na Jogoo) basi dawa yako ni hii 👇
Kanunue Vidonge vya Vitamin B Complex (Vit. BCO) then kwa siku 3 za mwanzo kunywa Viwili asubuhi na Viwili jioni (2×2).
Baadae kwa Muda wa Siku 14 kunya Vidonge 2 kwa siku.
Kama hajijapona endelea wiki moja zaidi, kama zimepona na kuisha basi sitisha kwa siku 30 ikisha kunywa tena siku 7 kwa Vidonge 2 kwa siku.
Fanya hilo zoezi kwa Muda wa wastani wa miezi 6 utakuja kunishukuru.
ANGALIZO:
Usisahau kuleta Mrejesho hapa.
- Hii dawa haijatengenezwa kwa ajili ya Kutibu Fangasi, lakini matokeo ya Wanywaji wake yameonesha inatibu Fangasi kwa ufanisi Mkubwa zaidi kuliko zile dawa zenyewe za Fangasi.
- Epuka kuvaa Boksa/Chupi za kubana hasa kama unaishi maeneo yenye Joto kama Dar au Zanzibar.
- Usafi wa kila siku unahitajika.