Kwanini maisha ya Ulaya yana stress pressure fatigue kuliko mtu anayeishi Tanzania?

Covax

JF-Expert Member
Feb 15, 2021
6,488
22,136
Kwanini ukiishi nchi za wenzetu zilioendelea zenye ajira nyingi, maisha mazuri safi good hygiene medical care nzuri nk. Lakini stress miongoni mwa watu ziko high mpaka kusababisha high blood pressure, Ulaya kutembea na kifaa cha kupima mapigo ya moyo ni sehemu ya maisha ya kila siku, hyper stress mpaka watu wanaamua kujiua(sucide).

Watu wanakata tamaa na maisha rehabilitation houses ni nyingi, psychiatrist ni wengi kwasababu idadi ya watu wanaochanganyikiwa ni wengi kila siku hususani wale ambao wamekaa kwa muda mrefu 10. 20 30 40, kama wamechanganyikiwa hivi..........

Mimi nafikiri Uchumi wa wenzetu hauruhusu mtu kuendelea bila kufanya savings kwa kujinyima, mtu anaingia miaka 60, haoni jipya zaidi ya hand to mouth income, lazima apate stress na high blood pressure imuue mapema ndo utasikia amekufa kwa heart attack.......

Wakati hapa watu wanadunda bila ajira na wana vitambi na pressure hawana siku nzima unajadilli mechi ya Simba na Yanga siku zinaenda, hana shida yoyote, shida zingine ni za kujitafutia, msitamani kwenda Ulaya kuishi.
 
Tanzania ni nchi ya 135/145 kwa furaha duniani. Yani tupo top ten kutoka chini. Hizo nchi za Europe ulizotaja ni Ukraine na ugiriki pekee ambazo watu wake hawana furaha.
Unaposema Ulaya kuna stress kuliko Tz unatumia data zipi?
Mkuu tofoutisha neno stress na furaha, furaha sio opposite ya stress, unaweza ukawa na furaha ila ukawa na stress.
 
endelea kujipa moyo kwa sababu una uhakika wa kula vyakula vya mifugo (ugali kwa dagaa) na unatoka kitambi kabisa, Mungu aturehemu siye watanzania tunajisifia umaskini na udumazi wa akili.
Mkuu acha dharau kwani Ulaya wanakula nini kama sio ngano kwa 80% ni maamuzi tu ya mtu kwa amua atakula nini, ila hao watu wanaishi bila stress.
 
Raha ya huku bongo kuna pesa ya upigaji, rushwa, ujanja, utapeli, udalali unaweza kumfanya mtu kuishi kuliko Ulaya ambapo mambo haya si sana. Huko Ulaya asiyefanya kazi na asile ingawa zipo posho za wasiojiweza kiuchumi.

Pia hapa kwetu ipo pesa ya kufahamiana na undugu unaweza upewe na hata kukopeshana sisi kwa sisi bila kwenda benki maisha yanakwenda,ulaya sahau. Aidha watu huponea Michango mingi ya harusi na misiba. mambo km haya kwa wenzetu hayapo. ingawaje dhana hii haijafanyiwa utafiti kubaini assumption yako
 
Kwanini uki ishi nchi za wenzetu zilio endelea zenye ajira nyingi maisha mazuri safi good hygiene medical care nzuri nk. Lakini stress miogoni mwa wstu ziko high mpaka kusababisha high blood pressure, Ulaya kutembea na kifa cha kupima mapingo ya mwayo ni sehemu ya maisha ya kila siku, hyper stress mpaka watu wana amua kujiua(sucide) watu wanakata tamaa na maisha rehabilitation houses ni nyingi psychiatrist ni wengi kwasbb idadi ya watu wanao changanyikiwa ni wengi kila siku hususani wale ambao wamekaa kwa mda mrefu 10. 20 30 40, kama wame changanyikiwa hivi..........

Mimi nafikiri Uchumi wa wenzetu hauruhusu mtu kuendelea bila kufanya savings kwa kujinyima mtu anaingia miaka 60, haoni jimpya zaidi ya hand to mouth income, lazima apate stress na high blood pressure imue mapema ndo utasikia amekufa kwa heart attack.......

Wakati hapa watu wana dunda bila ajira na wana vitabi na pressure hawana siku nzima unajadilli mechi ya simba na Yanga siku zinaenda hana shida yoyote, shida zingine ni zakujitafutia msitamani kwenda Ulaya kuishi.
Endelea na ndoto zako za alinacha!
 
Back
Top Bottom