Kampuni ya AQUA iliyoleta ukakasi ishu ya Dangote ni ya nani?

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
618
1,816
Katika kile kilichoelezwa leo na mh. rais juu ya kizungumkuti na maneno maneno kuhusu kusitisha uzalishaji wa kiwanda cha DANGOTE, ilitajwa kampuni ya AQUA kuwa ni wapiga deal ambao walijiingiza kati kati (Udalali) ili kufanikisha upatikanaji wa gesi ya ethene kutoka TPDC..Nilitaka kufahamu hasa kampuni hii ni ya nani ili watanzania tuijue (Hizi ni zama za kuwaanika wapiga deal wote).

Nimejaribu kupita pita na kukutana na hii kampuni inayojiita AQUA WELL DRILLING COMPANY LIMITED yenye usajili namba SPC2/0082/11/2006 ikiongozwa na MASOUD KHALFAN na yenye makazi yake jijini DAR..Ndio hii au kuna nyingine?

Ombi langu wakuu kama ni hii tupeane undani au kama kuna mtu anaifahamu nyingine basi tujuzane maana hakuna namna zaidi ya KUWAUMBUA na KUWAANIKA licha ya kuambiwa na mh, rais itafutiliwa mbali..
 
AQUA power ni kampuni ya kuzalisha umeme.

Nadhani ndo wamepewa tenda baada ya majenereta yaliyokuwa yakitumika mwanzo kuingizia hasara kampuni na inasemekena project iko kwenye hatua nzuri. Soon Dangote atapata umeme toka kwa hawa jamaa kabla ya mwezi Aprili 2017 yapata Megawati 30

Hawa jamaa kama sikosei nadhani ndo wanaozalisha umeme wa Lindi na Mtwara kama megawatt 18 hivi
 
Watu inaonyesha tupo mbali sana na dunia ya kibepari. Kwa kifupi ni kuwa, hakuna uwekezaji wowote unaofanyika bila udalali. Miji kama New York , London, Singapore , Hong Kong ndipo makampuni makubwa ya udalali yalipo. Ndiyo yanayoaminiwa na wawekezaji wakubwa kutoa taarifa na sifa za uwekezaji katika nchi mbalimbali. Investor kabla hajaenda nchi anayotaka kuwekeza anapita kwenye haya makampuni anakuwa fed up na taarifa za kutosha juu ya nchi husika. Hayo makampuni ya udalali yakishakuweka kwenye "yellow light" ujue una kazi kubwa kupata uwekezaji.

Na wao wanakusanya taarifa kupitia kwa kampuni za madalali katika nchi husika na ndio maana hizo kampuni zinakuwa middle men kati ya mwekezaji na Serikali. You can't (or very difficult to avoid). Sawa tu kama mfumo wa kutafuta nyumba au viwanja au chumba ulivyo katika maeneo ya mijini. Dalali anaweza ku-spot nyumba yako kuwa haifai, na kuipa sifa zote mbaya kama anajua hatafaidika kwa kumleta mpangaji.

Sisemi kuwa hiyo nyumba haitapata mpangaji/nchi kukosa uwekezaji! lakini mpangaji (sawa na mwekezaji) wanapenda kupata taarifa kutoka kwa watu wa kati/madalali wakiamini ni sahihi zaidi kuliko kutoka kwa mhusika mwenyewe. Hivyo basi, serikali inabidi iwe makini kidogo ku-deal na hawa madalali.Kwa mataifa makubwa, wenyewe wamekuwa wakianzisha kampuni za udalali na kufungua ofisi katika nchi zilizoendelea ili kuepuka "kupigwa" na madalali.

Hatua ni nzuri kupunguza ulanguzi wa kidalali ila tusijisahau kujua madalali ni watu wa namna gani.
 
Mwambie raisi wako aache kudharilisha nchi kama alijuwa kuna kampuni hiyo kwa nini alikuwa anataka mpaka Forbes waandike baada ya Dangote kulalamika its bad move for our country huwezi kuongoza nchi kwa utapelitapeli hivi ukiwa raisi hufunzwi namna ya kukabiliana na matatizo I am tired and sick
 
Back
Top Bottom