Hivi historia ya Tanzania inafundishwa drs/kidato gani?

nasaluka

Senior Member
Jun 20, 2015
149
184
Nimejaribu kufanya utafiti mdogo juu ya historia ya tz hasa inayohusu harakati za uhuru na muungano sijaona inapatikana drs/kidato cha ngapi katika mitaala ya tz.

Swali langu linatokana na kiu ya kutaka kujua watoto wetu wanarithishwa nini huko mashuleni.?
 
Nasaluka,
Wala usiitabishe akili yako kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika
na historia ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964.

Hatajapata ujasiri wa kuandika historia ya kweli ya Tanzania sasa
zaidi ya miaka 50.

Nimesoma historia ya uhuru wa Tanganyika Chuo Kikuu Cha
Dar es Salaam.

Kila siku nilikuwa nagongana na mwalimu wangu kwa kumueleza
kuwa hilo silo hili silo.

Nikamfahamisha kuwa naitoa makosa historia hiyo kwa kuwa wazee
wangu ndiyo walioasisi hizo harakati za uhuru na hapa sioni kutajwa.
Ingia hapa:
Mohamed Said: KUTOKA JF: BABU YANGU SALUM ABDALLAH

Nikawa katika semina wakati mwingine naachiwa nieleze historia ya
TANU na mambo yalivyokuwa.

Mwisho wa yote kwa kuchelea historia ya kweli isije kupotea nikaandika
kitabu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924-1968) The
Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in
Tanganyika,'' Minerva, London 1998.

Kuhusu historia ya Mapinduzi ya Zanzibar, kitabu kilichoeleza ukweli ni
cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' USA,
2010.
Ingia hapa:
Free Downloading ya Kitabu
 
Nimekupata mzee wangu
 
Ni kweli,ila maalimu Mohamed Said amefunua mengi katika,Maisha na nyakati za Abdulwahd Sykes.
Balibaba...
Watu wameshaanza kuandika historia hii.
Dr. Harith Ghassany kaandika historia ya Zanzibar.

Ali Muhsin Barwani kaandika kumbukumbu zake, ''Conflicts and Harmony
in Zanzibar,'' na humo kaeleza mengi kuhusu Zanzibar na mapinduzi.

Aman Thani kaandika kitabu, ''Ukweli ni Huu,'' na kaacha mihadhara katika
DVD halikadhalika Ali Muhsin kafanya hivyo pia.

Prof. Ibrahim Noor Sharif kaandika kitabu muhimu sana, ''Propaganda za Udini
Tanzania.''

Kitabu hiki kimerekebisha mengi katika uongo uliokuwa umezagaa kuhusu utumwa
Zanzibar na kwengineko duniani.

Ingia hapo chini:

Tatizo lilibakia ni kwa watafiti wa Tanzania Bara, wao wameridhishwa na hii
historia inayosomeshwa enzi na enzi.
 
Nimejaribu kufanya utafiti mdogo juu ya historia ya tz hasa inayohusu harakati za uhuru na muungano sijaona inapatikana drs/kidato cha ngapi katika mitaala ya tz.

Swali langu linatokana na kiu ya kutaka kujua watoto wetu wanarithishwa nini huko mashuleni.?
Kama shule uliyosoma hukufundishwa historia ya Tanganyika na baadaye Tanzania kuna mawili. Moja inawezekana ulikuwa mtoro wa kukubuhu hivyo ulipitwa na vipindi na pili inawezekana ulipofundishwa yaliingilia sikio la kulia na kutokea kushoto.
Nenda maktaba ya taifa ujikumbushe. Ila Tanganyika ilipata uhuru 1961. Anzia hapo kuja mbele au kurudi nyuma ujuwr vita ya majimaji ilipiganwa lini, akina Mkwawa, Kinjekitile Ngwale, Kimweri, Mirambo walifanya nini.
 
Mengi kati ya uliyofundishwa wakati huo ni historia iliyopotoshwa.Ukiulizwa Damu ya Msanii Duly Sykes utasema ni mzaramo wa Mzenga maana ukoo wake hautajwi popote,Dr Vedasto Kyaruzi huwezi jua alikuwa ni nani.Wengi mnajua kwamba historia ya uhuru inaanza na Nyerere inaisha na Nyerere.Anachoulizia mleta mada,ni historia halisi ambayo haijapotoshwa kuwahalalisha watawala waleo.Historia muijuayo ni ya kwamba ZNP kilikuwa chama cha waarabu na kwamba ASP walikuwa hawamtambui sultan wakati hata ASP kama wangeshinda uchaguzi wa 1963,sultan angebaki.
 
Kama shule uliyosoma hukufundishwa historia ya Tanganyika na baadaye Tanzania kuna mawili. Moja inawezekana ulikuwa mtoro wa kukubuhu hivyo ulipitwa na vipindi na pili inawezekana ulipofundishwa yaliingilia sikio la kulia na kutokea kushoto.
Nenda maktaba ya taifa ujikumbushe. Ila Tanganyika ilipata uhuru 1961. Anzia hapo kuja mbele au kurudi nyuma ujuwr vita ya majimaji ilipiganwa lini, akina Mkwawa, Kinjekitile Ngwale, Kimweri, Mirambo walifanya nini.
Maliambwiga,
Kinachoulizwa ni historia kwa maana yake halisi kuwajua watu walioifanya hiyo
historia.

Haitoshi kujua kuwa uhuru ulipatikana mwaka wa 1961.
Muhimu ni kujua historia ya mashujaa wa uhuru huo.

Kujua Vita vya Maji Maji bila kuwafahamu mashujaa wake bado historia haijakaa
sawa.

Historia ya uhuru wa Tanganyika na historia ya Mapinduzi ya Zanzibar zilikuwa kwa
kweli zimevurugwa hadi pale walipotokea watafiti wakaandika.

Lakini muhimu ni pale wahusika wenyewe walipoamua kuandika historia hizo wao
wenyewe au kwa kutoa ushirikiano wa dhati kwa watafiti wa historia.

Picha hiyo hapo chini ni ya Mwandishi na Dr. Harith Ghassany.

Mwandishi aliweza kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa msaada
wa Nyaraka za Sykes na mahojiano.

Dr. Harith Ghassany ameandika historia ya Zanzibar kwa utafiti aliofanya Marekani,
Uingereza na Arabuni na kwa kufanya mahojiano na Wazanzibari wenyewe.

fm4WIXMyQUJfGlF7PsmD49H4lP0LKOMX8DxDgAslXvtsBOyaArHb1wzDOn7D-42mtcOMm4lcRyx-q3qb1eB-uOBbvxteLs-HogrqXAY3UNw_CBSGJOuAn3rhLoJNiERCadfqHDggTgUuG9Gq4vciPEW_KLiKpVtL1YiwK9_tH8azQ1ZE6ZMIxfpuPJiYBhc_CgLhlgG3WJgoFQubo3wXk3kRh96nhLWWKSfuH87OHgFPehZqwlB8Jxnxomo0l-ve1x--vJz6a8-SA7eJ2SmaqMgs1SUIvPb2p1g-p-9-l8676ULFVtF2hvPbLwd4hhjUvIMXKg6MEiE0JZylV025h2GfiTLTPuW6CHe5BLzRnxuI5ZRHl_YsYmxVmEkQlP9CtRQrhYnjgbX9wSHpmVkR6m_5rjUfMSd-1f5IizJ8xepdm4v9gWocOp5fH9y7n8d0re2-pjmc2FLsbpt3C8J_OvFLADGABXwn5XsjpnJe_ZOqFIWZz19g3iOL4UJFnJQ86CSKsbdidlYsjolYVu5eLUEtkkk70iszTjN-Af8sKJBGvbKjICQajFwlH0asP6CfWZrCwv5cPBDNaIWjT1k9zbOlMWmc3R_Qkm1g911CVf7n9QdFdA=w480-h360-no

Mwandishi na Dr. Harith Ghassany Muscat Oman 2015
 
kuificha historia halisi ya taifa hili ni kuwanyima haki yao wananchi wengi tunaelezwa juu juu tu,wakati mengi yanafanywa siri!ni kwa hofu ya nani?
 
Naona hapa tunataka kupotosha sasa sio kweli kua Historia yetu aifundishwi bhana .. Kuanzia darasa la 4, 5, 6, 7 watoto wanafundishwa mada kuhusu Tanganyika.. Form 2 na F4 mada zipo kuhusu uhuru na mapinduzi... Sasa tatizo mnataka mtoto aisome Tanzania tu nakuwataja babu zenu ndo mtarizika au... Ata hao wanao andika lazma wataacha mengine tena ya muhumu.. Writing History is more subjective than reading History
 
Back
Top Bottom