Fursa zinazopatika kipindi cha mavuno ya ufuta maeneo ya Kilwa kuanzia May mpaka Agosti kila mwaka

Jul 14, 2021
34
35
Habari, hii taarifa nilishawahi kuandika siku 3 au 4 zilizopita sasa baada ya watu wengi kutoelewa na kuhisi vibaya nimerudi kuweka KILA kitu wazi fursa zinazopatika kwenye msimu huu wa mavuno ya zao la ufuta.

1. Unaweza kununua ufuta Kwa wakulima na ww ukauza kwenye vyama vya msingi na ukapata faida. Kwa mfano msimu wa kilimo (2021-2022) Bei ya ufuta kwa wakulima ilikuwa kilo moja kati ya Tsh. 1500 mpaka Tsh. 2500, kwenye vyama vya msingi ilikuwa kilo moja kati ya 2800 mpaka 3600.

Msimu wa (2022-2023) yaani msimu mwaka jana, bei kwa wakulima ilikuwa kilo moja kati ya Tsh. 2000 mpaka Tsh. 3000, bei ya vya msingi kwa kilo moja ilikuwa kati ya Tsh. 3500 mpaka 4000.

Unaweza kujiuliza kwanini mkulima auze bei ya chini wakati kwenye vya msingi bei iko juu, sasa mfumo uko hivi;

Vya vya msingi vinakusanya ufuta halafu watangaza tarehe ya mnada kwa matajiri wakubwa ambao wanapeleka ufuta nje ya nchi, atakae fika bei juu ndio anauziwa. Sasa basi huu mchakato unaweza kuchukua wiki hadi wiki 2.

Sasa baadhi ya wakulima wanaona kuchelewa huo mzinguko, wengine wanauza ili kupata pesa ya gharama ya uendeshaji. Mfano mkulima aweza kupata tani 3 au 2 analazimika kuuza walau kilo 300 ili apate pesa ya usafilisha wa mzigo wake kupeleka kwenye magala ya vyama vya msingi.

Pia baadhi ya wakulima hawapeleki kwenye vyama vya msingi kwa sababu hana account ya bank, maana vyama vya msingi vinafanya malipo ya mazao ya mkulima kupitia bank.

Fursa nyengine kwenye hiki kipindi cha ufuta ni biashara ya fedha mtandao, yaani hiki kipindi cha ufuta mawakala TiGO-Pesa, Airtel Money, HaloPesa, ila wakala wa NMB ndio utaishiwa hela, maana wakulima walio na account ya bank 90% ni NMB.

Ukiacha na hayo kipindi hiki cha ufuta biashara ya vyombo inatembea sana, maana hiki kipindi wakulima wanakuwa na hela. Akina mama wanapenda sana kununua vyombo, nguo zinauzika pia.

Kwangu mimi hiki kipindi ni kidogo sana ila kipo vizuri sana kwa mjasiliamali. Wewe Mtanzania unaweza kuifuata hii fursa

From kilwa.
 
Ufuta Ni big deal ambalo Ni Kama wengi hawajafungua macho mfano mwaka huu huku songwe ufuta ulifika Hadi 85000 kwa kilo 20
 
Screenshot_20240522-062300.png
 
Wiki ijayo nakuja kupiga kambi huko nije kusumbuana na wale niliowakopesha shiling 1000 kwa kilo maarufu kula maua,najua kutakuwa na ugumu mno mtu kukulipa kilo zote za ufuta kutokana na huu mnada unaopigwa mikoa ya wenzetu bei kuwa juu mno
 
Wiki ijayo nakuja kupiga kambi huko nije kusumbuana na wale niliowakopesha shiling 1000 kwa kilo maarufu kula maua,najua kutakuwa na ugumu mno mtu kukulipa kilo zote za ufuta kutokana na huu mnada unaopigwa mikoa ya wenzetu bei kuwa juu mno
Aaah biashara ya kukopesha inafaida ila inachangamoto sana, ya kupitia kudai, wapi ndugu yangu ulikopesha
 
Back
Top Bottom