CWT: Mkurugenzi wa jiji la Mwanza alipika takwimu za wanafunzi hewa na kufukuzisha walimu 62

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,969
Chama cha Walimu Mkoa wa Mwanza kimesema kuwa Mkurugenzi wa jiji la Mwanza alipika takwimu za wanafunzi hewa kwa makusudi kisha kufukuzisha walimu wakuu 62 wilaya ya Nyamagana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella amesema ameunda kamati ya kuchunguza tuhuma hizo.

  • Thanks
Reactions: BAK
Siwezi kushangaa iwapo hili ni la kweli.

Ona mwenzake wa Misungwi na kioja chake cha kumpigisha deki darasa mwalimu eti kisa tu kakuta darasa ni chafu!!

They are too defensive to the extent that they look foolish & stupid!!
 
watanzania wote kila mahala watawajibika kuwalipa fidia waalimu hao kwa.kudhalilishwa,badala ya kununua madawa na mengineyo,itabidi taifa lilipe mabilioni ya fidia kwa uamuzi wa mtu mmoja tu ambao kwanza hakuwa kaufanyia utafiti,mbaya zaidi yeye mwenyewe ni mwanasheria,hakuwapa hata haki ya kuwasikiliza
 
Tatizo la viongozi wateule wakitaka waandikwe kwenye media kick yao ni walimu....kwa hiyo viongozi wanatembelea nyota za walimu kutimiza ndoto zao
 
Na atumbuliwe tu, pia mkuu wa kaya aache kufurahia takwimu bila kufanya uchunguzi
 
Hata halmashauri ya Ruangwa kuna watu wanataka kutembelea nyota za waalimu. siku si nyingi mtasikia bado nafuatilia kuna figisu figisu zinafanywa na waliopewa dhamana idara ya msingi. TUTAUWEKA HADHARANI UOVU WAO DHIDI YA WALIMU ILI WAPATE HIYO KIKI WANAYOITAFUTA.
 
Tusiongee tusiyo yajua asee yaliyoko mwanza kuhusu wanafunzi ni zaidi ya masinema hao wakuu wa shule wanatapa tapa na wachache walio waingiza wenzao mkenge ndo watawaponza kuna scenario nyingi mfano.
Kuna shuke toks mwaka jana mwezi wa 8 mpaka leo idadi ya wanafunzi haijawah pungua wala kuongezeka so inamaana watu hawajamaliza darasa la saba wala hawajaandikisha darasa la kwanza,
Sasa wana tafuta namna ya kukwepa kila siku wapo maofisin wakiruka ruka kupika data watanyooshwa tu hakuna namna
 
Tatizo la viongozi wateule wakitaka waandikwe kwenye media kick yao ni walimu....kwa hiyo viongozi wanatembelea nyota za walimu kutimiza ndoto zao

Hivi sijui kwanini bado Rais hajawashtukia hadi sasa
 
Tusiongee tusiyo yajua asee yaliyoko mwanza kuhusu wanafunzi ni zaidi ya masinema hao wakuu wa shule wanatapa tapa na wachache walio waingiza wenzao mkenge ndo watawaponza kuna scenario nyingi mfano.
Kuna shuke toks mwaka jana mwezi wa 8 mpaka leo idadi ya wanafunzi haijawah pungua wala kuongezeka so inamaana watu hawajamaliza darasa la saba wala hawajaandikisha darasa la kwanza,
Sasa wana tafuta namna ya kukwepa kila siku wapo maofisin wakiruka ruka kupika data watanyooshwa tu hakuna namna

Tusubiri uchunguzi ufanyike yawezekana kuna mengi zaidi tukayasikia
 
Binadamu kwa asili ana pande mbili kama viumbe vyote vilivyoumbwa, yaani negative na positive.
Naamini awamu hii lakini kama binadamu kuna waziri mmoja na rc mmoja ambao wananipa mashaka na kudhani kuwa kama mkulu 'ameghafirika' ameweza kuwaamini basi tutakuwa tunajidanganya kutegemea ya maana!
 
Back
Top Bottom