Barua ya wazi kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro

Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
3,281
2,423
Kwanza kabisa nianze kwa salam na kumshukuru Mungu kwa kuweza kutupa uhai pamoja na changamoto tunazo zipitia wananchi wa Tanzania.

Lakini pia naomba kukupongeza sana Mh. Mtatiro kwa kuteuliwa tena na Mh. Rais kua mkuu wa wilaya ya Shinyanga. Najua na kuamini utendaji kazi wako ndiyo msingi wa kuweza kuendelea kuwepo kwenye safu ya uongozi wa serikali hii ya awamu ya sita.

Mh. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga ndugu Mtatiro, hapo Shinyanga kuna watu wanapitia madhira yasiyo ya kawaida baada ya kunyimwa haki zao. Kwenye watu hao kuna wazee,wamama na vijana. Watu hao wameweza kuangaika sana kutafuta haki zao lakini kila wakati wamekau wakizungushwa na taasisi mbili ambazo ni kampuni ya Phantom, NSSF na shule ya sekondari Savannah Plains ambayo inamilikiwa na kampuni ya Phantom.

Nimewai kukutana na wamama pamoja na walimu ambao walifanya kazi katika Shule hiyo ya Savannah Plains na kuachishwa kazi au kumaliza mikataba yao lakini awakulipwa mafao ya hifadhi ya jamii. Kuna wamama ,wazee na walimu wamefanya pale miaka zaidi ya mitatu mpaka mitano lakini michango yao ya NSSF pamoja na kukatwa hiyo michango ilikua aipelekwi NSSF.

Watu hao walijaribu kwenda mpaka NSSF na mahakamani,mkuu wa mkoa, TAKUKURU lakini awakupata msaada kabisa wa kupata malipo yao jambo ambalo ni kinyume na taribu pampja na sheria za hifadhi ya jamii.

Mh.Mtatiro wewe kama mkuu wa wilaya mpya katika eneo ilo itakua busara sana kuwasaidia watu hao kupata haki zao. Kuna watu walimaliza mikata wengine kuachishwa kazi zaidi ya miaka minne sasa wengine mitano na wamefanya kazi zaidi ya miaka minne lakini waliwekewa kiasi cha michango ya miezi mitatu tu.

Watu hao maana yake wamepoteza ata haki ya kukopeshwa,kupata huduma kama ya matibabu au kujiajiri kwa kutumia hifadhi yao ya jamii.

Mwisho kabisa..Mh.Mtatiro matumaini ya hao watu sasa yapo mikononi mwako kama kiongozi makini .Najua unaweza kabisa kuwasaidia kupata haki zao maana umeweza kufanya hivyo toka ujawa ata mkuu wa wilaya,
MUNGU IBARIKA AFRIKA
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Kiongozi yeyote wa upinzani akipewa cheo serikalin hufikir kwamba "amehongwa" ili aachane na utetezi wa wananchi .

Hivyo hugeuka kuwa adui mkubwa wa wapenda haki na watetezi wa haki. Lengo la kufanya hivyo ni Ile kuendelea kuifaidi "hongo"

Mtatiro huyu sio Yule tuliyemfaham.

Usitegemee msaada wowote kutoka kwake.
 
Mimi nimemfikishia ujumbe mkuu
nimekuelewa ,lakini kama wao hawataki kuingia mtaani achana nao tafuta Hela ,ila kama msukuma mwezao/ mtanzania ujumbe umefika kalishakuwepo kasukuma kezenu hapo kama kakuu ka wilaya kakitokea chadema hakuwasaidia na nimwanasheria

Mtatiro nae mwanasheria/wakili atatoka kapa ishi sio mkuu wilaya ishu mfumo unaruhusu kutapeliwa maskini kwenye hilokundi
 
nimekuelewa ,lakini kama wao hawataki kuingia mtaani achana nao tafuta Hela ,ila kama msukuma mwezao/ mtanzania ujumbe umefika kalishakuwepo kasukuma kezenu hapo kama kakuu ka wilaya kakitokea chadema hakuwasaidia na nimwanasheria

Mtatiro nae mwanasheria/wakili atatoka kapa ishi sio mkuu wilaya ishu mfumo unaruhusu kutapeliwa maskini kwenye hilokundi
Sawa mkuu lakini atuwezi kuacha uovu huo ufumbiwe macho kamwe
 
Back
Top Bottom