Ali Msham na Julius Nyerere

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,902
31,972

Ramadhani Matimbwa with Adam Kirumbi and 31 others.

November 20, 2015 ·
Mwl.Julius K. Nyerere akikabidhiwa meza ya ofisi yake ya TANU na wazee wa DSM! Mmoja ya walio ktk picha hii ndiyo alitengeneza meza hiyo.Je tunawajua wazee hawa?Na hapo ni wapi ktk DSM hii?Karibuni kwa michango yenu wana D'salaam.


LikeComment
Share

Zakaria Digosi, Rams Jacob Ruzohwama and 27 others like this.
1 share
Comments

5 of 17
View previous comments
Ramadhani Matimbwa Mungu awarehemu Wazee wetu hawa kwa kazi kubwa walizozifanya ktk harakati za kuikomboa nchi hii.Japo leo hawatajiki lakini Mwenyezi Mungu atawalipa inshallah! Tunashuhudia leo watu wananeemeka ktk CHAMA chetu bila jasho!
Like · Reply · 1 · November 23, 2015 at 11:06am

Like · Reply · November 23, 2015 at 11:11am
Sule Mavitu amin amin amin
Like · Reply · November 23, 2015 at 11:22am
Sule Mavitu wazee hao mola awalaze mahala pema
Like · Reply · November 23, 2015 at 11:23am
Mohamed Said Hizo samani zilitengenezwa na Bwana Ali Msham aliyekuwa na kiwanda chake Mtaa wa Kariakoo. Alifika ofisini kwa Nyerere New Street Makao Makuu ya TANU akamkuta Nyerere anafanya kazi katika meza ambayo Ali Mshama aliona haina hadhi ya rais wa TANU. Ndipo alipoamua kumtengenezea Nyerere samani mpya zitakazoendana na heshima yake na heshima ya TANU. Hii ilikuwa mwaka wa 1955. Wakati huo Ali Msham alikuwa amefungua tawi la TANU nyumbani kwake Mtaa wa Jaribu hapo Magomeni Mapipa. Hapo kwenye tawi la TANU nyumbani kwake ndipo ilipopigwa hiyo picha siku alipokaribishwa Nyerere kuja kupokea samani kwa ajili ya ofisi yake. Pamoja na samani Nyerere alipewa na saa ya ukutani na vitu vingine.Hawa wazee wengi wametangulia mbele ya haki. kwa hakika walikuwa wazalendo wa kweli na walijitolea hali na mali kupambana na ukoloni. Ali Msham ni huyo aliyesimama wa kwanza kulia na aliyekaa kwenye meza ni Julius Nyerere.
 
Pamoja na mambo mengine, inashangaza ukienda Butiama kwa Marehemu mpendwa wetu unalipa kiingilio mara mbili. Unatoa sh. 5,000/= kuingia makumbusho (upande wa serikali) unatoa sh. 5,000/= upande wa pili kuzuru kaburi la Baba wa Taifa. Alaf nguo alizovaa mara ya mwisho anaenda kwenye matibabu ziko upande wa serikali!
 
Picha nzuri na inaonesha jinsi Mwalimu alivyokuwa hana hila wala kudharau wengine hata kwa michango yao midogo waliyotoa. Viongozi waliofuata baada yake utu wao anaujua Mungu pekee!!
Allen,
Huo haukuwa mchango mdogo.
Ulikuwa mchango mkubwa sana.

Achilia mbali thamani ya samani.
Wakati ule kujinasibisha na TANU ilikuwa kujitafutia matatizo na wakoloni.

Ali Msham alijitolea chumba kimoja nyumbani kwake kiwe ofisi ya TANU.
Hakuishia hapo alimfungulia Mama Maria Nyerere kijiduka kidogo cha
kuuza mafuta ya taa.

Jioni nyakati za Maghrib ishaingia mtoto wa Ali Msham alikuwa ndiye
akimsindikiza Mama Maria nyumbani kwake Magomeni Majumba Sita.

Wakati ule Magomeni miembe mitupu na kiza kikiingia panatisha kwa
mwanamke kutembea peke yake.
 
Dah, mbona hawa watu hawasemwi kwenye historia kabisa, somewhere nyerere alikuwa selfish sana
"Selfishness" yake iko wapi? Wewe miaka 60 ijayo akitokea mtu akaweka picha ya Mtu aliyemlipia ada ya kwanza Magufuli wakati anakwenda shule utauliza mbona historia yake haijaandikwa?
 
Yote hayo ameshasahaulika na kupotezwa kama sii kudharauliwa... washapigwa deki na kugaragazwa hao !!!!
 
Harakati za kudai uhuru huwezi kufananisha na swala la ada,maana hata huyo nyerere kungekuwa na mtu kamlipia ada watu hawawezi kulalamika kwa kutomzungumzia huyo mfadhili wake wa ada,hapa swala ni harakati za kudai uhuru kuna watu hawatajwi kabisa kila jambo nyerere kitu ambacho sio kweli,nyerere hasingeweza kufanya chochote bila msaada wa hao watu.huo ndio ukweli hata kama hupendi kusikia habari za namna hiyo.
Kama huyo aliyetoa meza naye atajwe kwenye vitabu vya historia kwa nini? Lakini kwenye historia za ngazi ya chama cha TANU yupo na ndiyo maana hiyo picha ilipigwa. Kama Nyerere asingekuwepo hiyo Meza angempa nani?
 
Ukitaka kuwaweka kila mtu kwenye historia y ukombozi wa africa basi utaweka adi wanajeshi maafisa police na wanausalama wa taifa ambao wamefanya mengi.kikubwa historia itawasema kwa wakati wao watakopitajika kama hapa nyerer kapewa meza basi ndio lazima tumjue mhusika.lakini huwezi weka wote.tutavuruga maana nzima ..
 
Allen,
Huo haukuwa mchango mdogo.
Ulikuwa mchango mkubwa sana.

Achilia mbali thamani ya samani.
Wakati ule kujinasibisha na TANU ilikuwa kujitafutia matatizo na wakoloni.

Ali Msham alijitolea chumba kimoja nyumbani kwake kiwe ofisi ya TANU.
Hakuishia hapo alimfungulia Mama Maria Nyerere kijiduka kidogo cha
kuuza mafuta ya taa.

Jioni nyakati za Maghrib ishaingia mtoto wa Ali Msham alikuwa ndiye
akimsindikiza Mama Maria nyumbani kwake Magomeni Majumba Sita.

Wakati ule Magomeni miembe mitupu na kiza kikiingia panatisha kwa
mwanamke kutembea peke yake.
Mzee Mohamed Said nakubaliana kama Ofisi ilikuwa haina meza bora kama hiyo na Ally Mshamu (Bila shaka ni mmatumbi) akaitoa Meza hiyo bila shaka ulikuwa ni mchango mkubwa sana, lakini kwa Mwalimu mwenyewe kwenda kuipokea badala ya kumtuma mtu mwingine inaonesha ni jinsi gani alivyokuwa anathamini mchango wa kila mmoja. Lakini kwa wakati huo pia kama Mama maria alikuwa na duka hapo kwa Mshamu na lazima aende kulala kwake Magomeni Majumba sita si ajabu kwa mtoto wa Mshamu kumsindikiza bi mkubwa huyo.
 
Ukitaka kuwaweka kila mtu kwenye historia y ukombozi wa africa basi utaweka adi wanajeshi maafisa police na wanausalama wa taifa ambao wamefanya mengi.kikubwa historia itawasema kwa wakati wao watakopitajika kama hapa nyerer kapewa meza basi ndio lazima tumjue mhusika.lakini huwezi weka wote.tutavuruga maana nzima ..
Troojan,
Linawekwa jina la yeyote yule aliyehusika katika historia ya uhuru wa nchi yetu iwe awavyo.
Ali Msham hakutoa meza peke yake.

Ali Msham aliunga mkono harakati za uhuru kwa kufungua tawi la kwanza la TANU nyumbani
kwake Magomeni Mapipa.

Akiuza kadi na fedha akipeleka mwenyewe kwa Iddi Faizi Mafongo aliyekuwa Mweka Hazina
wa TANU New Street.

Hapana ubaya kuihifadhi historia hii.

Maofisa wa polisi waliosaidia TANU walikuwapo mmoja wapo alikuwa Hamza Aziz wakati ule
ofisa wa ngazi ya chini katika Jeshi la Polisi la Waingereza.

Hamza ni mdogo wake Dossa Aziz.
Huyu TANU walimtumia sana kupata mikakati ya Waingereza kuihujumu TANU.

Alikuwapo Amri Kweyamba na Kitwana Kondo katika Special Branch.
Huyu Amri Kweyamba aliwashughulisha sana wana TANU.

Mara kadhaa alivamia nyumba ya Ally Sykes Mtaa wa Kipata kutafuta makaratasi ya ''uchochezi,''
ambayo Ally akiyasambaza kuanzia Dar es Salaam, Morogoro nemda hadi mwisho wa reli Kigoma
na Mwanza.y of

Mimi nimeandika historia hii katika kitabu, ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes,'' (1998) na
haijavuruga chochote katika historia ya Tanganyika bali imeleta changamoto kubwa kwa wanahistoria
si wa Tanzania tu bali ulimwengu mzima.

Leo kitabu hiki kinasomeshwa kote wanakosomesha, African History na kipo Library of Congress,
Washington.
 
Back
Top Bottom