Tafiti mpya iliyofanywa na mamlaka ya kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya NACADA imeonesha kuwa watumiaji wa bangi wameogezeka maradufu katika kipindi cha miaka 5.
Kwa mujibu NACADA, mtu mmoja katika kila watu 53 walio na umri wa kati ya 15 - 65 ni mraibu wa bangi.
Wanaume wanaongoza kwa...
Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula leo amepokea ombi rasmi la kutaka kupiga marufuku matumizi ya mtandao wa TikTok, kwa madai kuwa mtandao huo unatumiwa vibaya na Vijana kueneza uchafu na anasa hasa nyakati za usiku.
Ombi hilo limewasilishwa na Afisa Mtendaji wa Kampuni ya Briget connect...
Rais William Ruto ameibua mjadala mitandaoni baada ya wataalam wa saa za mkononi kufichua kwamba alivaa saa kutoka kwa kampuni ya Jaeger Coultre yenye thamani ya Shilingi milioni 6.4 za Kenya ambazo ni sawa na milioni 111,565,761 pesa za Tanzania.
Serikali ya Rais William Ruto imemuagiza Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na familia yake kurejesha silaha zote wanazomiliki kama familia ya Kenyatta.
Familia hio inatarajiwa kurejesha jumla ya bunduki 28 wanazomiliki tangu enzi za babake mzazi Hayati Rais Jomo Kenyatta.
Baadhi ya raia wa Kenya katika mtandao wa Twitter wameonekana kukerwa na kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan juu ya athari ya maandamano yanayoendelea kushuhudiwa.
Rais Samia alisema kuwa Tanzania imekuwa ikipokea idadi kubwa ya wawekezaji tangu mwezi Juni kutokana na 'moto' mkubwa unaoshuhudiwa...
Hatimaye Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga amevunja ukimya baada ya kutojitokeza hadharani kushiriki maandamano.
Raila ameeleza kuwa alilazwa baada ya kuugua homa kali.
“Niko na homa mbaya sana ambayo ilinipiga na ikanilaza chini. Nimepata matibabu kutoka kwa daktari na sasa ninazidi kupata...
Wakenya kwenye mitandao ya kijamii wametoka rai kwa Inspekta Jenerali wa Polisi Japheth Koome kumkamata askari huyu aliyenaswa na kamera mara tu baada ya kumpiga risasi mtu mmoja kwenye maandamano ya Jumatano katika eneo la Mathare, kaunti ya Nairobi.
Baadhi ya watu katika mtandao wa twitter...
Mbunge wa Embakasi Mashariki Mheshimiwa Babu Owino angali bado anashikiliwa na polisi katika kituo cha Polisi cha Wanguru kilichoko kaunti ya Kirinyanga, Mke wake Fridah Ongili amethibitisha.
Owino ambaye ni mwandani wa karibu wa Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga alikamatwa Jumanne jioni katika...
Kiongozi wa zamani wa kundi haramu la Mungiki Maina Njenga alikamatwa nyumbani kwake eneo Kiserian usiku wa kuamkia Alhamisi. Aidha kakake Njoroge Njenga pamoja na msaidizi wake Ole lekishe walitiwa nguvuni usiku uo huo.
Kwa mujibu wa Mwanasheria wake Ndegwa Njiru, haijabainika wazi kituo cha...
Karibu utupie jicho yaliyomo kwenye kurasa za mbele ya magazeti leo Julai 20, 2023. Inasadikiwa wahariri wakuu wa magazeti walifikia makubaliano ya kutumia kichwa kimoja cha habari, kutoa rai kwa raia kudumisha umoja na amani.
Ikumbukwe maandamano yanatarajiwa kuendelea Leo na kesho.
Wizara ya elimu imetangaza kuwa masomo katika shule za kutwa zilizokuwa zimefungwa leo katika kaunti za Nairobi, Kisumu na Mombasa yatarejelewa kesho Alhamisi.
Awali Serikali ilitangaza kufunga shule hizo kutokana na vuguvugu la maandamano linaloshuhudiwa nchini lakini sasa imeeleza kuwa...
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga pamoja na Viongozi Wakuu wa Muungano wa Azimio akiwemo Martha Karua hawajulikani waliko.
Vilevile Wabunge kadhaa wa Muungano wa Azimio akiwemo Mheshimiwa Babu Owino wangali bado kujitokeza hadharani.
Haijabainika wazi iwapo ni mpango wa Raila kutojitokeza...
Serikali imewapokonya Waziri Mkuu wa zamani Raila Odinga na Makamu wa Rais wa zamani Kalonzo Musyoka walinzi dakika chache zilizopita.
Aidha Wabunge sita akiwemo Opiyo Wandayi vilevile wamepokonywa walinzi.
Kawaida Viongozi wa ngazi za juu serikalini wanapostaafu hupewa walinzi kwa ajili ya...
Idadi ya maiti Shakahola yafikia 403
Idadi ya maiti zilizofukuliwa katika msitu wa Shakahola imefikia 403 baada ya miili 12 kufukuliwa tena. Hayo yamethibitishwa na Kamishna wa ukanda wa pwani Rhoda Onyancha ambaye amesema shughuli ya kusaka miili inaendelea kwa ushirikiano mkubwa wa maafisa wa...
Kiongozi wa Upinzani Raila Odinga kupitia Ukurasa wake wa twitter amethibitisha kuwa vuguvugu la maandamano ya siku tatu mfululizo kuanzia Jumatano lingali bado lipo kwenye ratiba ya Muungano wa Azimio.
Maneno yake yanakuja dakika chache tu baada ya Mahakama kudinda kuweka zuio la maandamano...
Raila Odinga
Kiongozi Mkuu wa Upinzani Raila Odinga amesema kuwa anatarajia kukamatwa wakati wowote kuanzia sasa baada ya kuthibitisha kukamatwa kwa aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya jioni ya Alhamisi.
Aidha Raila ametangaza siku 5 za kuomboleza waandamanaji walioaga dunia...
Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amesema uharibifu uliotekelezwa na waandamanaji kwenye barabara maarufu ya 'Nairobi Expressway' utagharimu Serikali ya Kenya takriban milioni 700, sawa na bilioni 12 pesa za Tanzania.
Waziri Murkomen amesema haya baada ya kuzuru barabara hio kufanya...
Seneta wa kaunti ya Nairobi Edwin Sifuna kwenye mahojiano na televisheni ya Citizen amethibitisha maandamano sasa yatadumu kwa siku tatu mfululizo kila wiki; kuanzia Jumatatu mpaka Jumatano.
Tangazo hili linakuja huku taifa likikadiria hasara kubwa kufutia maandamano makubwa yaliyofanyika Jana...
Maandamano ya Jumatano yalishuhudia uharibifu mkubwa zaidi ikilinganishwa na ya hapo nyuma huku waandamanaji wakiharibu barabara maarufu ya Expressway, ambayo ilikuwa ndio mradi mkubwa zaidi na wa mwisho aliofanikisha Rais mstaafu Uhuru Kenyatta.
Barabara hio ambayo watumiaji wake hulazimika...
Watu watatu wameaga dunia eneo la Mlolongo kwenye barabara ya kuelekea Mombasa kufuatia vuguvugu la maandamano linaloshuhudiwa nchini.
Aidha waandamanaji wa eneo hilo leo wameharibu sehemu ya barabara ya Expressway iliyokuwa ndio mradi mkubwa wa mwisho wa Rais mstaafu Uhuru Kenyatta...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.