Kadi ya DART ndani yake ina uwezo wa kuandika taarifa za makampuni zaidi ya 10 hivyo ni suala la muda tu kinachofanyika ni ku syncronize na huduma nyingine tu na mambo yanakwenda hakuna haja ya kubeba lundo la kadi wataalam wetu waliliona hilo, yetu ni multipurpose.
Kazi iendelee, Leo tarehe 22/4/2024 shehena kubwa ya Mageti Janja (smart gates) kwa ajili ya kufunga vituoni ili kufungamanisha na mfumo wa matumizi ya kadi janja (smart cards), inaendelea kushushwa pale Gerezani, watumiaji wa Mabasi Yaendayo Haraka muendelee kuwa na imani na Serikali yenu...
Maoni yanapokelewa na yanafanyiwa kazi ni kwa vile tu watanzania wengi hatupendi kuwa na subra wakati huu ambao serikali inatatua changamoto ya uchache wa Mabasi.
Ndugu zangu pamoja na matatizo yote ambayo mmeeleza kuna njia mbadala ya kukata tiketi kimtandao unatakiwa kupakua app ya mwendokasi kwenye simu yako ili ununue tiketi kidigitali wakati tunaendelea kukamilisha utaratibu wa kurudisha huduma ya kadi.
Pole sana kwa kadhia iliyokukuta wakati mwingine piga simu ya huduma kwa wateja bur 0800110147 ili hatua zichukuliwe kwa haraka, aidha usisahau kutaja muda na mahali ambapo tatizo husika limetokea.
Uchache wa Mabasi ndio unasababisha adha hii ,lakini maelekezo ya serikali ni kutafuta mtoa huduma mwingine ambaye atashindana na huyu wa sasa ili kuboresha huduma, maelekezo hayo yanafanyiwa kazi na baada ya muda mfupi mtaona matokeo.
Kukamilika kwa ruti kuna maanisha , mosi barabara na miundombinu mingine iwe imekamilika kwa asilimia mia moja na kukabidhiwa, hii inajumuisha pia vituo taa za kuongozea magari, taa za barabarani vituo mlishi n.k. , sambamba na hilo awe amepatikana mtoa huduma mwenye uwezo wa kuwa na idadi ya...
Serikali iko kazini na kama ulifuatilia juzi ziara ya Waziri Mchengerwa alitoa maagizo ya kuongeza watoa huduma zaidi ya mmoja ili kuleta ushindani huo ndio mwelekeo tuvute subra mambo mazuri yanakuja, hakuna mtu yeyote anayefurahia watanzania kuteseka kwa adha ya usafiri ni suala la muda tu.
kinachozungumziwa hapa ni daladala kupita kwenye njia maalum za BRT sio route za kawaida za njia za mitaani ambazo zimeainishwa na Mamlaka ya LATRA. habari hii ilisema daladala kuanza kutumia njia za mwendokasi ili kusaidia mabasi jambo ambalo sio sahihi. Umewahi kuona wapi daladala inapita...
Mfumo huu ulikuwepo awali lakini ilitokea changamoto ukaharibika ndiomaana hata utaratibu wa kutangaza vituo haupo, kwa sasa tuko kwenye hatua za kununua mfumo wa ITS inteligent transport system ambao utakuwa ukitumika kuongoza magari, kupanga ruti, sambamba na masuala yote yanayohusu vituo...
Hakuna taarifa iliyoeleza kuwa usafiri utaanza mwezi huu wa kumi isipokuwa kulikuwa na taarifa za mradi kukabidhiwa serikalini baada ya mkandarasi kumaliza ujenzi.
Hakuna ukweli katika jambo hilo, kwanza daladala uwezo wake ni mdogo katika kubeba abiria wengi, pili miundombinu ya vituo hairuhusu kushusha na kupakia abiria kwani daladala ni fupi na hazijatengenezwa kwa ajili ya BRT.
Mkandarasi ameshakabidjhiwa eneo la ujenzi na sasa ameanzakuandaa materials kwa ajili ya kuanza ujenzi mara moja, jana kama umefuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ya intsgram, facebook, na X(twitter) ya @dartmwendokasi utaona hata mfadhili Benki ya Dunia alikuwa saiti kuangalia maandalizi...
Oktoba hii tunakabidhiwa miundombinu ikiwa imekamilika kabisa, baada ya hapo utasikia kutoka kwetu kuwa ni lini tutaanza huduma endelea kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii ikiwemo JF.
Tunakoelekea ni kuzuri tutaanza na matumizi ya Gesi asilia na hatimaye kwenye matumizi ya magari ya kuchaji kwa umeme na hata solar, lengo ni kuelekea katika matumizi ya nishati ambazo hazichafui na kuharibu mazingira kama vile matumizi ya umeme.
Tunakushukuru sana kwa maoni yako ya kuboresha huduma zetu, mawazo yako ni mazuri sana na baadhi yake tumeshaanza kuyafanyia kazi ikiwemo utaratibu wa kuwa na Mabasi mahsusi yenye viyoyozi lakini pia kuwa na VIP buses, aidha tunaendelea na mchakato wa kuwa na sheria yetu ambayo itaturuhusu...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.