Wakuu, nawaaga kwa muda. Naelekea Tandika kwenye kukabidhi kadi kwa viongozi wa CCM wamemua kujivua gamba na gwanda, nimeitwa huko na M4C ya eneo lao inayofanya kazi ya ujenzi wa chama kuanzia kwenye misingi mpaka matawi. Nikimaliza jioni baada ya mkutano wa hadhara nitarejea baada ya mkutano...
Wavuti iko kwenye matengenezo kwa ajili ya kuzinduliwa upya kwa mwonekano tofauti, matengenezo hayo yanaendelea kwa muda mrefu sasa. Wanachama wataalamu wa IT na ubunifu wakiwasiliana nasi kupitia info@chadema.tz na nakala chademahabari@gmail.com baada ya hatua mbili tatu za uhakiki wanaweza...
Hili suala nilishalitolea maelezo toka mwanzo na Dr Slaa alishaelekeza marekebisho kwenye orodha kwamba katiba ya 2004 haiko kwenye orodha hiyo. Kwa hiyo kufanyia rejea kitu kilichofanyiwa marekebisho ni kutaka tu kuhamisha mjadala. Dr Slaa alizungumzia suala la rebranding ya chama, kwenye dhana...
Wala hakuna ulazima wa minutes za vikao hapa, sisi tumeandika katiba mpya mwaka 2006. Ushahidi kwamba hakuna kipengele cha ukomo wa vipindi viwili ni rasimu iliyopitishwa na wajumbe mwaka 2006. Atuletee mtu hapa kwamba katiba ilipitishwa ikiwa na ukomo wa vipindi halafu baadaye kifungu...
Naomba nikukumbushe maneno ya Nyerere kwamba ukiona mtu anakimbilia kwenye ukabila ujue umefilisika kwa hoja. Baba yangu Mzee John Dalali ni msukuma, mama yangu Lucia Mduma ni mpare; unaweza kuamua mimi ni kabila gani. Suala la msingi hapa sio kabila la mtoa hoja, bali hoja yenyewe. Jenga hoja...
Uchaguzi ngazi za majimbo, wilaya, mikoa na taifa haujafanyika kwa chama wala kwa jumuiya. Kikatiba, chama kinaanzia ngazi ya msingi halafu tawi, ili ngazi za mbele zifanye uchaguzi lazima ngazi ya chini si chini ya 50 ziwe zimekamilisha uchaguzi. Maeneo yaliyofanya chaguzi ni ngazi hiyo ya...
Pasco, Pamoja na marekebisho niliyoeleza kuhusu majibu ya Dr Slaa kwamba katiba ya 2004 iondolewe kwenye orodha kama nilivyochangia hapo awali. Katiba ya mwaka 2004 haiwezi kuwa ushahidi wa hayo madai yasiyokuwa ya kweli. Katiba ya mwaka 2004 mimi ninayo hapa nilipo, kwenye kifungu cha 6.3.2...
Pasco nimesoma mjadala ulioanzisha na majibu ya Dr Slaa. Kabla ya kusoma mjadala huu, niliitikia mwito wa Mtoi kwenye Jukwaa la Wanamabadiliko na nikaandika kwa kirefu kuhusu suala hili ambalo mimi nilishiriki kwa karibu sana nikiwa sehemu ya timu zote tatu zilizohusika na mchakato wa kukusanya...
Niweke tu kumbukumbu sahihi. Sijawahi kuhojiwa wakati wowote ule na maafisa wa polisi kuhusu Deus Mallya, ni kweli kwamba kwenye mkutano na wanahabari niliwahi kuulizwa swali iwapo Deus ni mtumishi au afisa wa makao makuu ya chama. Nilikana kwa sababu hakuwahi kuwa mtumishi wa makao makuu ya...
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM...
Shardcole,
Nashukuru. Naomba urudie tena kusoma katikati ya mstari mchango wangu wa kwanza utabaini kuwa kabla hata ya tuhuma na shutuma za sasa kutolewa JF tayari chama kilishaanza kuchukua hatua kuhusu baadhi ya wanachama kuchafua viongozi kwenye mitandao ya kijamii na njia nyingine za...
Mag,
Shukrani. Kwa maana rahisi mgogoro ni mchakato ambao kila upande una matakwa yake na unaona upande mwingine unakwenda kinyume na matakwa hayo na kufanya vitendo vya kuhujumiana; mgogoro ni kipeo cha kutokuelewana na kutokubaliana kwa kiwango cha kukabiliana. Migogoro mara nyingi huwa na...
Jorojik,
Asante, sio kila kitu lazima wasemaji wa chama tuingie kutoa ufafanuzi. Zingine ni propaganda za kijivu ambazo hata nyinyi mnaweza kuzitolea majibu.
Ikiwa kila uzushi na upuuzi unaoandikwa mtatulazimisha viongozi tuingie na kuutolea majibu mtakuwa mmefanikisha malengo yao ya kututoa...
Mtizamo,
Asante kwa mtizamo wako. Hata hivyo zingatia kwamba chama kufanya maamuzi yake kwa kuzingatia katiba na kanuni na suala la vikao vya maamuzi ni muhimu kuzingatiwa. Kumbuka kwamba siku chache zilizopita tulikuwa kwenye kikao cha kamati kuu, kikao kingine pengine ni mpaka mwezi Januari...
Avanti, asante kwa maoni yako hata hivyo zingatia kuwa 'press' yangu ipi? Ikiwa wewe kweli ni mwanachama wa CHADEMA na una malalamiko dhidi ya kadi ya Dr Slaa andika rasmi kwa chama. Kabla ya kuandika malalamiko hayo usome kwanza katiba ya CHADEMA, katiba ya CCM na sheria ya vyama vya siasa. Dr...
Tangu wanachama wachache wa CHADEMA walipoanza kutuhumiana na kushutumiana kupitia JF watoa maoni mbalimbali mmetoa mwito kwa chama kuchukua hatua na wengine mmehitaji majibu kutoka viongozi wengine na kwangu kuhusu hali hiyo iliyojitokeza.
Ifahamike tu kuwa mara baada ya tuhuma na shutuma hizo...
Nape,
Walatini wanamsemo ambao kwa kiswahili rahisi humaanisha maandiko hubaki, mlichokifanya Mwanza wewe na viongozi wengine wa chama chako kiliandikwa, mfano: CCM yabuni mbinu mpya kwa hiyo unataka kusema kwamba magazeti yaliwasilisha maneno? Na sio magazeti tu, baadhi ya vituo vya...
Nape nashukuru kwa majibu yako na majibu kama haya haya yaliyotolewa na Naibu Katibu Mkuu wenu Mwigulu Nchemba, naona ni vyema nijielekeze kwenye hoja zako na niachane na vioja vingine. Ikiwa majibu haya ni msimamo pia wa Mwenyekiti wenu Kikwete na Katibu Mkuu Kinana, hakika mnadhihirisha kauli...
Bwana Kimbunga Nakushukuru sana kwa maoni yako, nakushauri uanze kwanza kukusanya saini za watanzania siku ya uhuru tarehe 9 Disemba 2012 tunaposheherekea miaka 51 ya Uhuru bila ya maji katika majimbo mbalimbali nchini (Ubungo likiwa na afadhali kuliko majimbo mengi nchini na hata baadhi ya...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.