A
Anonymous
Guest
Hospitali ya Mbagala Zakhem iliyopo Mbagala Dar es Salaam imekuwa kama ni sehemu ya kuwamaliza Watu, kuna mifano mingi tu kuhusu huduma zao kutokuwa na kiwango kizuri na hivyo kuwaathiri wengi.
Mfano kuna Mtoto wa ndugu yangu mwenye umri wa Mwaka Mmoja na Nusu, alikuwa anasumbuliwa na Degedege, pia Mtoto wa jirani yangu naye alikuwa anasumbuliwa na Upungufu wa Damu ingawa huyu ni mkubwa kama umri wa miaka 17 hivi.
Walipofikishwa hospitali hapo kupata huduma, Manesi na Madaktari hawapo care kabisa kwa kuwa wanajua mwisho wa Mwezi wataingiziwa tu kodi yetu ili wazitafune.
Ukijaribu kuwauliza kitu Watumishi wa hapo kuhusu huduma zao wanakwambia usiwafundishe kazi na wanakuwa wakali kuliko Simba mwenye njaa.