DOKEZO Moshi: Watumishi wa Mkataba Hospitali ya KCMC, tunakatwa fedha ya Bima ya NHIF lakini hatunufaiki na huduma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Mimi ni miongoni mwa Wafanyakazi wa Hospitali ya Rufaa ya KCMC, Kitengo cha utafiti KILIMANJARO CLINICAL RESEARCH INSTITUTE (KCRI).

Katika kitengo hiki Waajiriwa wengi ni wale wa mkataba, kwani wao huwa wanaajiriwa kutokana na miradi iliyopo, hivyo pindi miradi inapoisha huwa mikataba yao pia huisha.

Sasa yapata mwezi wa tatu au wanne hatupati huduma za matibabu kupitia Bima za NHIF.

Tumejaribu kufuatilia kwa muda sasa lakini majibu tunayopewa yanakuwa ya kukatisha tamaa, kila siku ni stori zilezile za “linafuatiliwa” “linafanyiwa kazi” lakini siku zinazidi kwenda, mishahara inakatwa fedha kwa ajili ya bima lakini hakuna huduma ya Bima inapotokea wanahitaji huduma hiyo.

Tunateseka, wengi wetu ni Watoto kutoka familia duni na Wazazi wetu ndio hufaidika na bima hizo kupitia sisi.

Inapotokea huduma haipatikani kidogo inakuwa ni changamoto sana kwenye kutoa cash, kwani huo mwisho wa mwezi wenyewe unajikuta una madeni kila mahali.
 
KCMC vile mko ndani ya hosp, mna uhakika wa matibabu.

I wish mngekuwa huku mtaani mlipie hiyo huduma sijui ingekuwaje.

Hope kila kitu kitakuwa sawa. jipeni muda.
 
𝐇𝐚𝐭𝐚 𝐰𝐚𝐭𝐮𝐦𝐢𝐬𝐡𝐢 𝐰𝐚 𝐬𝐞𝐫𝐢𝐤𝐚𝐥𝐢 𝐩𝐢𝐚 𝐭𝐮𝐧𝐚𝐩𝐚𝐭𝐚 𝐛𝐚𝐚𝐝𝐡𝐢 𝐲𝐚 𝐡𝐮𝐝𝐮𝐦𝐚.
𝐍𝐇𝐈𝐅 𝐢𝐦𝐞𝐤𝐮𝐰𝐚 𝐤𝐞𝐫𝐨 𝐭𝐚𝐧𝐠𝐮 𝐰𝐚𝐛𝐚𝐝𝐢𝐥𝐢𝐬𝐡𝐞 𝐊𝐢𝐭𝐢𝐭𝐚 𝐜𝐡𝐚 𝐌𝐚𝐟𝐚𝐨.

𝐈𝐦𝐚𝐠𝐢𝐧𝐞 𝐮𝐧𝐚𝐞𝐧𝐝𝐚 𝐤𝐮𝐧𝐮𝐧𝐮𝐚 𝐆𝐥𝐨𝐯𝐞𝐬 𝐧𝐚 𝐛𝐨𝐦𝐛𝐚 𝐥𝐚 𝐬𝐢𝐧𝐝𝐚𝐧𝐨 🙂🙂
𝐍𝐈 𝐇𝐔𝐙𝐔𝐍𝐈
 
Back
Top Bottom