Tujifunze Kukataliwa!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
4,005
7,675
Hakuna kitu kigumu kukipokea kama kukataliwa na Yule unayempenda au unaye tarajia kuwa nae ktk Maisha ya kimapenzi.

Tujue Kwanza kukataliwa ni haki ya yule anayetukataa,ana Uhuru na uamuzi wa kufanya hivyo,kwakuwa naye ana vigezo vyake vinavyo mfanya amchague mtu Fulani,kwahiyo tusipokuwa na vigezo hatuna haki ya kupendwa na mtu huyo,tukubali ukweli na kusonga mbele.

Kukataliwa ni sehemu ya Maisha ya kila siku,wewe sio wa Kwanza kukataliwa,usijione hauna thamani kwakuwa Tu eti umekataliwa,tambua kwamba haujakizi Tu vigezo vya huyo umpendaye lkn haimaanishi kuwa ndiyo hauna thamani laa! Thamani IPO pale pale Ila Tu haujakutana na Yule ambaye anaijua thamani yako,so IPO siku utampata Yule ambaye anaijua thamani yako na mtainjoy mahusiano yenu.

Kukataliwa usikuchukulie upande wa negative Tu bali chukulia upande wa positive pia Kwa faida yako,je unajuaje kama huyo aliye kukataa alikuwa mtu sahihi kwako? Je Una uwakika gani kwamba angekupa furaha ambayo ungeitamani? Kwahiyo kukataliwa wakati mwingine ni faida kwako kuepukana na mtu ambaye angekuwa sababu ya maumivu yako au mateso yako,umekataliwa huenda kuna mtu mwingine ambaye unatakiwa ukutane na ambaye atakuwa ulimwengu wako,atakuwa nuru yako na atakuwa pumziko lako.

Na kitu kingine ambacho watu hawajui ni kuwa,wanaotukataa ndio huenda wamekula hasara! Ndiyo narudia tena wamekula hasara,unajua Kwa nini? Kwasababu wanakosa Yale mazuri ambayo wangepata kutoka kwetu,wanakosa utulivu ambao wangeupata kutoka kwetu na wanakosa MAHABA ambayo wangepata kutoka kwetu,kwahiyo wakati mwingine badala ya kuumia na kukosa Raha inatakiwa tuwaonee huruma Tu.

Ni hayo Tu.
 
Kubali kuwa vitu fulani huna na usonge mbele na ujifunze kuridhika kwa ulichonacho

Kusonga mbele bila manung'uniko ni sehemu mojawapo ya kujijali

Zamani nilikuwa sikubali aisee, ila tangu niujue ukweli narelax na maisha yanasonga

sio kila kitu ni cha kulazimisha, vingine jifunze tu upate somo
Kweli kabisa mkuu,na huko ndio kujitambua na huko ndio kukua na huko ndio kujielewa,..... Kwa namna hii wala hautapata tabu ktk Maisha,ni kujifunza kuyaangali mambo ktk mtazamo chanya
 
Nakumbuka nkiwa foolish age kuna manzi alinipiga za mbavu daah ili uma but courage bhana nkamwambia "Nashukuru sana kwa Jibu lako" akaniuliza "why" nkamwambia umeniepusha na mengi... ilikuwa mtafutano ooh soo hutaki tena, was just kidding... Haha haha haha
Unajua y alipagawa? Ulimuonyesha wewe ni mtu tofauti Sana ndiyo maana akashangaa reaction yako
 
Back
Top Bottom