Rais Kusitisha Uzazi wa Mpango Kwa"Fyatueni Watoto wa Kutosha",Ni Yake au ni ya Wale Wazee wa..?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,582
113,799

Video Footage kwa hisani ya Millard Ayo wa AYO TV. (Full HD)

Wanabodi,

Swali.
Hii ni mada ya swali, Jee hii kauli ya rais wetu, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ya kusitisha uzazi wa mpango nchini Tanzania kwa Kauli ya "Fyatueni Watoto wa Kutosha nitawasomesha bure!" jee kauli hii imetoka kwake yeye binafsi kama rais wa Tanzania, akitutaka tufyatue watoto wa kutosha kufuatia kutoa elimu bure, au kauli hiyo imetoka kwake kama muumini au kwa kwa maelekezo kutoka kwa wale "Wazee ?!...(waliyemleta?)", ambako uzazi wa mpango haukubaliki, kwa hoja kuwa mpango wa Mungu kwa Wanadamu ni Zaeni muongezeke muijaze nchi yote?!.

Kauli Tata.
Hii sii mara ya kwanza kwa rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, kutoa kauli tata, rais ameendelea kutoa kauli tata, huku akishangiliwa na umati wa watu!, usually kauli hizo zinatolewa kwenye mikutano ya hadhara kwa lengo la ku gain popularity ambayo ndio a typical style ya ma populist leaders wote duniani, to win peoples hearts halafu baadae hakuna lolote kwenye utekelezaji!.

Kauli latest ni hii ya kusitisha uzazi wa mpango Tanzania, kwa kuwataka watu "wafyatue watoto wa kutosha", "nitawasomesha bure!", as if lengo la uzazi wa mpango na kudhibiti idadi wa watu, tatizo lilikuwa ni kulipia tuu ada ya shule!, hivyo kama elimu sasa inatolewa bure, hivyo sasa, hakuna tena hitaji la kudhibiti idadi ya watu!, kwa nini tuendelee kudhibiti idadi ya watu huku elimu ni bure?!.

Kumbe Tatizo la Ongezeko la Idadi ya Watu, Ufumbuzi ni Elimu Bure?!.
Kwa tangazo hili, rais hakupaswa kuishia kwenye nitawasomesha bure, bali nitawalisha bure, nitawavisha bure, nitawajengea makazi bora bure, ya kila familia kuwa na angalau watoto 6-10!, kisha awasiliane na wachumi wa kuhusu matokeo ya idadi kubwa ya watu, wampe projection za population growth ya Tanzania, vs economic growth, tujiridhishe Tanzania itakuwa na uchumi wa kubeba ongezeko hilo kubwa la idadi ya watu, ikiwa kula bure, huduma zote za jamii bure, ikiwemo, afya na elimu, watu hao hawahitaji ajira, what for, ardhi tunayo yenye rutuba na rasilimali tele, tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda, uchumi wa gesi na kuwa nchi ya uchumi wa kati, soon tutakuwa na uwezo wa kutoa kila kitu bure, na hata ikibidi hata kodi tutafuta, hivyo kwanini wasifanye kazi moja tuu ya kufyatua watoto wa kutosha, asubuhi, mchana, jioni na usiku kucha?!.

Jee Rais ni Mropokaji au Anasingiziwa Tuu?!.
Kuna watu humu waliwahi kusema rais Magufuli ni mropokaji, na kuna watu watafikiri, tamko hili pia ni uropokaji!, mimi sifikiri hivyo, japo ni kweli kuna mazingira fulani rais Magufuli huwa anazungumza kama ni mropokaji fulani kwa kujitolea kauli zake mwenyewe!, lakini niliposikia akizungumzia "ufyatuaji wa watoto" "nitawasomesha bure", ameisema kama kiutani utani akiielekeza kwa watani zake Wazaramo, akiwataka sasa kufanya kazi moja tuu, "kufyatua watoto", lakini huu sio ule ule uropokaji wake wa kawaida!, ....(Tafsiri ya uropokaji ni kutoa matamshi yoyote ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kina kuhusu athari za tamko husika)

Kusitisha Uzazi wa Mpango ni Uropokaji au ni Kauli Thabiti?!.
Rais aliposema "nasitisha uzazi wa mpango kwa kipindi chote cha mimi kuwepo madarakani, halafu uzazi huo utaendelea baada ya mimi kuondoka!", ndipo nikashituka na kuyakumbuka maneno fulani niliwahi kudokezwa kumhusu Magufuli, alitokea wapi na ikawaje akawa ndio yeye rais wa Tanzania!. (Uthibitisho wa tamko hili kama ni thabiti au ni uropokaji tutaupata soon kupitia taarifa ya Mashirika ya Kimataifa yanajihusisha na idadi ya watu, Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, Shirika la Afya, WHO, UMATI, Pupolation Services Intenarnation (PSI) na ufafanuzi wa kauli hiyo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa sababu kuna international instruments Tanzania tumeridhia kama nchi, kuhusu uzazi wa mpango, haiwezekani leo, mtu akaibuka tuu, (hata akiwa ni rais wa nchi). halafu akasema ghafla tuu, Tanzania tumesitisha uzazi wa mpango!).

Why ni Magufuli Ndiye Rais Wetu, na Siye Mtu Mwingine Yeyote?!.
Niliposikia why ni Magufuli, nilipandisha uzi huu humu jukwaaniMgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ..., ila hizo sababu sikuzitaja kwa sababu nilikuwa siamini!, lakini kwa tangazo hili la kusitisha uzazi wa mpango Tanzania!, nimeanza kuamini, inawezekana kabisa, hayo niliyoyasikia kumhusu Magufuli ni kweli!. Na kama ni kweli, wele mliokuwa ukisubiria mahakama ya kadhi, na Tanzania ijiunge na OIC, mtasubiri sana!.

Kule nyuma niliwahi kuanzisha uzi, nikiuliza "hivi rais wa Tanzania akiwa Mkristu, ni lazima awe Mkatoliki?!, mode waliufuta uzi huo, kuwa ni udini!. Kisha nikauliza,
Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika ...
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...

Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano ...
Nguvu ya shirika la Kijasusi la kanisa Katoliki duniani na ...
na kuuliza, sikupata majibu, lakini sasa majibu yanaanza kujitokeza!.

Upande Mwingine.
Huu kuhusu kauli hii ni ya nani ni upande mmoja, upande mwingine, mimi binafsi, naiunga mkono kauli hii ya rais ya kufyatua watoto wa kutosha, kwa sababu ninaiishi!.

Pamoja na kutofautiana na Rais wangu, Magufuli kwenye utekelezaji wa baadhi ya kauli zake haswa zile za tumbua tumbua, lakini hili la kufyatua watoto wa kutosha, naliunga mkono!.

Familia za watoto wawili ni familia za kizungu, sisi sio wazungu!, familia za Kiafrika ni kuanzia watoto 4, 6 8 hadi10!, mimi tayari ninao 8, bado wawili!.

Ila katika hili la kufyaytua watoto wa kutosha, kuna kitu rais Magufuli, hakukisema kuhusu ufyatuaji huu!, alipaswa awaambie wababa, wasiwachoshe wamama kwa kuwafyatulisha watoto kibao, watawazeesha bure!, bali kufuatia Tanzania kuwa na idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume, kwenye ufyatuaji huu wa watoto wa kutosha, rais pia alipaswa kusema mpachikaji ndie aendelee kuwa mmoja lakini wafyatuaji wasaidiane, wengine hii ndio asili yetu, wafyatuaji wanakuwa wengi wa kutosha ili kutowachosa na wakati huo huo, kusaidia kubalance ziada ya wanawake waliozidi!.

Hivyo namshauri rais Magufuli, aibadili ile sheria yetu ya ndoa ya mwaka 1971, tukiondoe kile kipengele cha mila za kizungu cha mke mmoja, tubakize kile cha wake wengi, ila wale wanaopenda ndoa ya mke mmoja, iwe ni kwa ridhaa yao na mapenzi yao tuu na lisiwe ni takwa la kisheria!, ili Watanzania wengine wote tupatiwe fursa kama za wenzetu ambao mwisho ni wake 4, sisi sheria isiweke mwisho wa idadi ili tuwe na wafyatuaji wa kutosha.

Kitu ambacho rais angesisitiza katika ufyatuaji huu, lengo liwe ni ufyatuaji wa watoto, sio ile burudani au starehe ya ufyatuaji, ili hao watoto watakaofyatuliwa, wawe ni wale waliokusudiwa kufyatuliwa, ambao wazazi wao wana uwezo wa kuwalisha, kuwatunza, kuwalaza mahali pazuri, kuwasomesha elimu nzuri, na sio wale wanaotokea kwa bahati mbaya katika starehe na burudani za ufyatuaji, huku wengine wakitelekezwa na kuja kuwa watoto wa mitaani.

Jumamosi Njema!.

Paskali.
Update 1.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu aliikanusa kauli hii ya rais kwa kusema ilikuwa ni ya utani tuu, akiwatania watani zake Wazaramo.

P.
Update 2.
Rais Magufuli hapa amerudia msimamo wake kuhusu uzazi wa mpango

Jee Waziri Ummy atameza tuu kauli yake na sera yake ya afya?, au ataibuka na kuifafanua na hii, maana this time hajataji kuhusu watani zake!, asije kuibuka na kusema alikuwa akimaanisha kwa Wasukuma tuu!.

P.
 
Aaah inachosha siasa za kibongo,fisadi mpaka mhariri anamwagiwa tindikali,mwandishi anakatwa mapanga,mimi nimewacha kuwaamini,kipindi cha kampeni ya uzazi wa mpango bado watu walizaliana tu kila mmoja na maamuzi,nendeni mkazaane muijaze dunia!
 
Kinachonifurahisha ni hilo neno "kufyatua". Mkuu Pasco, hatukatai dhana ya kuzaliana kwa kuwa wengi wetu tumezaliwa katika familia zenye watoto zaidi ya watano, ila hilo neno lililotumika katika kusherehesha dhana ya kuongeza uzazi, yaani "kufyatua". Hao watoto wamekuwa matofali au viumbe? Kwa kweli hiyo lugha iliyotumika haiakisi uungwana wa tendo la uumbaji.
Tunajua hivi sasa idadi kubwa ya watu ni mtaji na ndio maana China na India zinajivunia kuwa na mtaji mkubwa wa soko la bidhaa. Hivyo sio vibaya kwa Rais kusisitiza ongezeko la watu ili tutengeneze soko kubwa la bidhaa zitakazozalishwa kutoka katika viwanda tutakavyovijenga. Ila tutumie uungwana katika kusisitiza hiyo dhana ya kuongeza idadi ya watu.
 
Watoto wa Tanzania wanafyatuliwa kama matofali!!! Hawahitaji KULA, kuvaa na Malazi.

Juzi Rais kasema hatawapa chakula ..... Leo anawataka wasitishe majina wafyatue, yeye atawasomesha.

Cha kushangaza na kufedhehesha, anazungumza as if he is doing us a faver. Poor Tanzania!!
 
Wanabodi,

Swali.
Hii ni mada ya swali, Jee hii kauli ya rais wetu, Mhe. Dr. John Pombe Joseph Magufuli, ya kusitisha uzazi wa mpango nchini Tanzania kwa Kauli ya "Fyatueni Watoto wa Kutosha!" jee kauli hii imetoka kwake yeye binafsi kama rais wa Tanzania, akitutaka tufyatue watoto wa kutosha kufuatia kutoa elimu bure, au kauli hiyo imetoka kwake kama muumini au kwa kwa maelekezo kutoka kwa wale "Wazee wa Kule?!...(waliyemleta?) ambako uzazi wa mpango haukubaliki, kwa hoja kuwa mpango wa Mungu kwa Wanadamu ni Zaeni muongezeke muijaze nchi yote?!.

Kauli Tata.
Rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli, ameendelea kutoa kauli tata, huku akishangiliwa na umati wa watu!, usually kauli hizo zinatolewa kwenye mikutano ya hadhara kwa lengo la ku gain popularity ambayo ndio a typical style ya ma populist leaders wote duniani, to win peoples hearts!.

Kauli latest ni hii ya kusitisha uzazi wa mpango Tanzania, kwa kuwataka watu "wafyatue watoto wa kutosha", "nitawasomesha bure!", as if lengo la uzazi wa mpango na kudhibiti idadi wa watu, tatizo lilikuwa ni kulipia shule tuu!, hivyo kama elimu sasa inatolewa bure, hivyo sasa, hakuna tena hitaji la kudhibiti idadi ya watu!, kwa nini tuendelee kudhibiti idadi ya watu huku elimu ni bure?!.

Kumbe Tatizo la Ongezeko la Idadi ya Watu, Ufumbuzi ni Elimu Bure?!.
Kwa tangazo hili, rais hakupaswa kuishia kwenye nitawasomesha bure, bali nitawalisha bure, nitawavisha bure, nitawajengea makazi bora bure, ya kila familia kuwa na angalau watoto 6-10!, kisha awasiliane na wachumi wa kuhusu matokeo ya idadi kubwa ya watu, wampe projection za population growth ya Tanzania, vs economic growth, tujiridhishe Tanzania itakuwa na uchumi wa kubeba ongezeko hilo kubwa la idadi ya watu, ikiwa kula bure, huduma zote za jamii bure, ikiwemo, afya na elimu, watu hao hawahitaji ajira, what for, ardhi tunayo yenye rutuba na rasilimali tele, tunakwenda kwenye uchumi wa viwanda, uchumi wa gesi na kuwa nchi ya uchumi wa kati, soon tutakuwa na uwezo wa kutoa kila kitu bure, na hata ikibidi hata kodi tutafuta, hivyo kwanini wasifanye kazi moja tuu ya kufyatua watoto wa kutosha, asubuhi, mchana, jioni na usiku kucha?!.

Jee Rais ni Mropokaji au Anasingiziwa Tuu?!.
Kuna watu humu waliwahi kusema rais ni mropokaji, na kuna watu watafikiri, tamko hili ni uropokaji!, mimi sifikiri hivyo, japo ni kweli kuna mazingira fulani rais huwa ni mropokaji tuu kwa kujitolea kauli zake mwenyewe!, hivyo niliposikia akizungumzia "ufyatuaji wa watoto" "nitawasomesha bure", nikajua huu ni ule ule uropokaji wake wa kawaida!, lakini ....(Tafsiri ya uropokaji ni kutoa matamshi yoyote ambayo hayajafanyiwa utafiti wa kina kuhusu athari za tamko husika)

Kusitisha Uzazi wa Mpango ni Uropokaji au ni Kauli Thabiti?!.
Rais aliposema "nasitisha uzazi wa mpango kwa kipindi chote cha mimi kuwepo madarakani, halafu uzazi huo utaendelea baada ya mimi kuondoka!", ndipo nikashituka na kuyakumbuka maneno fulani niliwahi kudokezwa kumhusu Magufuli, alitokea wapi na ikawaje akawa ndio yeye rais wa Tanzania!. (Uthibitisho wa tamko hili kama ni thabiti au ni uropokaji tutaupata soon kupitia taarifa ya Mashirika ya Kimataifa yanajihusisha na idadi ya watu, Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu, UNFPA, Shirika la Afya, WHO, UMATI, Pupolation Services Intenarnation (PSI) na ufafanuzi wa kauli hiyo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kwa sababu kuna international instruments Tanzania tumeridhia kama nchi, kuhusu uzazi wa mpango, haiwezekani leo, mtu akaibuka tuu, (hata akiwa ni rais wa nchi). halafu akasema ghafla tuu, Tanzania tumesitisha uzazi wa mpango!).

Why ni Magufuli Ndiye Rais Wetu, na Siye Mtu Mwingine Yeyote?!.
Niliposikia why ni Magufuli, nilipandisha uzi huu humu jukwaani Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe ..., ila hizo sababu sikuzitaja kwa sababu nilikuwa siamini!, lakini kwa tangazo hili la kusitisha uzazi wa mpango Tanzania!, nimeanza kuamini, inawezekana kabisa, hayo niliyoyasikia kumhusu Magufuli ni kweli!. Na kama ni kweli, wele mliokuwa ukisubiria mahakama ya kadhi, na Tanzania ijiunge na OIC, mtasubiri sana!.

Kule nyuma niliwahi kuanzisha uzi, nikiuliza "hivi rais wa Tanzania akiwa Mkristu, ni lazima awe Mkatoliki?!, mode waliufuta uzi huo, kuwa ni udini!. Kisha nikauliza,

Kete ya Dhana ya 'Zamu za Kupokezana' ina turufu yoyote katika ...
Sumu ya Siasa za Udini, Ukanda na Ukabila, "Is It Real? au ni ...

Japo hakuna kupokezana: Kiukweli, kihaki, kihalali na ki-Muungano ...
Nguvu ya shirika la Kijasusi la kanisa Katoliki duniani na ...
na kuuliza, sikupata majibu, lakini sasa majibu yanaanza kujitokeza!.

Upande Mwingine.
Huu kuhusu kauli hii ni ya nani ni upande mmoja, upande mwingine, mimi binafsi, naiunga mkono kauli hii ya rais ya kufyatua watoto wa kutosha, kwa sababu ninaiishi!.

Pamoja na kutofautiana na Rais wangu, Magufuli kwenye utekelezaji wa baadhi ya kauli zake haswa zile za tumbua tumbua, lakini hili la kufyatua watoto wa kutosha, naliunga mkono!.

Familia za watoto wawili ni familia za kizungu, sisi sio wazungu!, familia za Kiafrika ni kuanzia watoto 6-10!, mimi tayari ninao 8, bado wawili!.

Ila katika hili la kufyaytua watoto wa kutosha, kuna kitu rais, hakukisema kuhusu ufyatuaji huu!, alipaswa awaambie wababa, wasiwachoshe wamama kwa kuwafyatulisha watoto kibao, watawazeesha bure!, bali kufuatia Tanzania kuwa na idadi kubwa ya wanawake kuliko wanaume, kwenye ufyatuaji huu wa watoto wa kutosha, wafyatuaji wasaidiane, wengine hii ndio asili yetu, wafyatuaji wanakuwa wengi wa kutosha ili kutowachosa na wakati huo huo, kusaidia kubalance ziada ya wanawake waliozidi!.

Hivyo namshauri rais Magufuli, abaibadili ile sheria yetu ya ndoa ya mwaka 1971, tukiondoe kile kipengele cha mila za kizungu cha mke mmoja, tubakize kile cha wake wengi, ila wale wanaopenda ndoa ya mke mmoja, iwe ni kwa ridhaa yao na mapenzi yao!, ili Watanzania wengine wote tupatiwe fursa kama za wenzetu mwisho 4!.

Kitu ambacho rais angesisitiza katika ufyatuaji huu, lengo liwe ni ufyatuaji wa watoto, sio ile burudani au starehe ya ufyatuaji, ili hao watoto, wawe ni wale waliokusudiwa kufyatuliwa, na sio wale wanaotokea kwa bahati mbaya katika starehe na burudani za ufyatuaji.

Jumamosi Njema!.

Pasco

Hivi Magufuli ana watoto wangapi!!?
 
Kinachonifurahisha ni hilo neno "kufyatua". Mkuu Pasco, hatukatai dhana ya kuzaliana kwa kuwa wengi wetu tumezaliwa katika familia zenye watoto zaidi ya watano, ila hilo neno lililotumika katika kusherehesha dhana ya kuongeza uzazi, yaani "kufyatua". Hao watoto wamekuwa matofali au viumbe? Kwa kweli hiyo lugha iliyotumika haiakisi uungwana wa tendo la uumbaji.
Tunajua hivi sasa idadi kubwa ya watu ni mtaji na ndio maana China na India zinajivunia kuwa na mtaji mkubwa wa soko la bidhaa. Hivyo sio vibaya kwa Rais kusisitiza ongezeko la watu ili tutengeneze soko kubwa la bidhaa zitakazozalishwa kutoka katika viwanda tutakavyovijenga. Ila tutumie uungwana katika kusisitiza hiyo dhana ya kuongeza idadi ya watu.
Wingi wa watu nchini Nigeria ulikuwa ni mzigo kwenye miaka ya nyuma, lakini leo hii ndio umegeuka kuwa chanzo cha mabilionea wa kinigeria. Wingi wa watu ndio umegeuka kuwa soko la bidhaa za Dangote. Wingi wa watu ni neema kama wakipatiwa elimu ya maana na isiyo na magumashi. Ujerumani ina watu milioni 80, wakati uchumi wa dunia ulipoyumba yenyewe wala haikuyumba. Cha muhimu ni kutatua kero zote zenye uhusiano na upatikanaji wa elimu bora. Unaweza ukawa unatoa elimu bure lakini walimu hawalipwi mishahara ndani ya muda wanaostahili, pamoja na uwepo wa matatizo mengine ambayo huchangia katika viwango duni vya elimu inayotolewa.
 
Umenena hakika
 
Watoto wa Tanzania wanafyatuliwa kama matofali!!! Hawahitaji KULA, kuvaa na Malazi.

Juzi Rais kasema hatawapa chakula ..... Leo anawataka wasitishe majina wafyatue, yeye atawasomesha.

Cha kushangaza na kufedhehesha, anazungumza as if he is doing us a faver. Poor Tanzania!!
Hata tofali linamwagiwa maji mpaka liwe imara kabisa
 
Back
Top Bottom