Niulize kuhusu fursa ya masomo Sweden

Wakuu, imekuwa ni adimu sana kuona Wabongo tukishikana mikono ili kuvuka hatua moja kwenda nyingine yenye mafanikio. Tumezoea kupambana wenyewe na wengi wetu huwa hatupo wazi inapokuja suala la kumueleza mtu mwingine juu ya fursa fulani, tunapenda kuwa wabinafsi na wachoyo.

Kauli hii nimeithibitisha baada ya kutembelea nchi za wenzetu walioendelea (Ulaya) na kuona namna ambavyo Waafrika kutoka magharibi wanavyochangamkia fursa za hapa na pale na namna wanavyoshikana mikono ili kuvuka mahala.

Ni kwa mantiki hiyo basi, ili kuvunja kasumba ya ubinafsi wetu Wabongo, nipo hapa kujibu maswali juu ya fursa ya kimasomo unayoweza kuipata Sweden kwa ngazi ya Shahada ya Uzamili (Masters Scholarship).

Sio masuala ya kuja inbox, wewe uliza hapa hapa public nitakujibu. Sihitaji mtu kuja kunifuata inbox.

Karibuni.
Mkuu naomba msaada wako kuhusu hii fursa, japo imenipita kwa mwaka huu nitajitahidi mwaka ujao nijaribu. Ila nina maswali machache ambayo kwa hakika yatanisaidia sana pindi watakapoanza ku accept application mwaka ujao.

Maswali yangu ni haya hapa

1. Nimesoma kwenye link lakini sijaelewa, je unaanza apply chuo then ukikubaliwa chuo ndio una apply for scholarship?

2. Naomba unifafanulie pale wanaposema "Two different letters of reference are mandatory, one must be based on work experience, second must be based on your involvement in networks or civil society organizations outside your regular work". Je hizi barua nazitoa wapi?

3. Cv must use SI's form for CV 2023/2024.

4. Naomba unifafanulie wanaposema "You do not need to meet work experience requirement in one period of employment, nor do you need to have been working in your current employment for 3000 hours in order to be eligible to apply"

5. Leadership experience.
6. La mwisho ni kuhusu passport, je ni lazima niwe na passport wakati wa application?

Ukinijibu haya utakuwa umenisaidia mno angalau nipate mwanga wa kuanzia ili niepuke kuwa disqualified. Natanguliza shukran
 
1. Ndio scholarship hii ya Sweden unapaswa uwe admitted kwenye chuo/vyuo husika, kuna sehemu ya ku attach admission letter

2. Reference letter ya work experience utaiomba kwa mwajiri wako au aliekua mwajiri wako, reference letter ya pili utaiomba katika civil society org au mashirika uliyowahi kujitolea katika shughuli zao tofauti na mwajiri wako (A civil society organization (CSO) or non-governmental organizaiton (NGO) is any non-profit, voluntary citizens' group which is organized on a local, national or international level) kama huna nashauri weka academic reference letter, hiyo utaiomba kwa aliekua mwalimu/professor/lecturer wako chuoni
3. ingia hapa wameelezea namna wanavyotaka CV yako iwe

4. experience ya masaa elfu tatu ni sawa na mwaka mmoja na nusu (kwa kuzingatia masaa 8 kwa siku, siku tano kwa wiki), hivyo sio lazima uwe na experience ya kiwango hicho katika taasisi moja au katika kazi yako ya sasa

5. Uzoefu wa uongozi

6. Passport lazima

Nimejibu kwa kadri ya uelewa wangu, pia binafsi nimeshindwa ku apply kwasababu sikujua kua ni lazima uwe na admission ya chuo kwanza, na vyuo vingi vishafunga dirisha la application, good luck.
 
Mkuu naomba msaada wako kuhusu hii fursa, japo imenipita kwa mwaka huu nitajitahidi mwaka ujao nijaribu. Ila nina maswali machache ambayo kwa hakika yatanisaidia sana pindi watakapoanza ku accept application mwaka ujao.

Maswali yangu ni haya hapa

1. Nimesoma kwenye link lakini sijaelewa, je unaanza apply chuo then ukikubaliwa chuo ndio una apply for scholarship?

2. Naomba unifafanulie pale wanaposema "Two different letters of reference are mandatory, one must be based on work experience, second must be based on your involvement in networks or civil society organizations outside your regular work". Je hizi barua nazitoa wapi?

3. Cv must use SI's form for CV 2023/2024.

4. Naomba unifafanulie wanaposema "You do not need to meet work experience requirement in one period of employment, nor do you need to have been working in your current employment for 3000 hours in order to be eligible to apply"

5. Leadership experience.
6. La mwisho ni kuhusu passport, je ni lazima niwe na passport wakati wa application?

Ukinijibu haya utakuwa umenisaidia mno angalau nipate mwanga wa kuanzia ili niepuke kuwa disqualified. Natanguliza shukran
Mkuu, bila shaka majibu ya maswali yako, Mdau hapo juu kakujibu vizuri kabisa. Kama bado una dukuduku unaweza kuuliza tena Mkuu. Karibu.
 
Mambo vipi mkuu, vipi naweza pata scholarship kwaajili ya admissions ya mwaka 23/24 katika education especially in science subjects...

Kama zipo je, mda wake wa kuziomba ni upi...nipe mrejesho mkuu
23/24 utakuwa umechelewa tayari. Kwahiyo jipange kwa ajili ya mwakani Mkuu. Mchaklato wa admission utaanza kati ya October hivi..
 
Mimi nina ndoto za kuunganisha masters maana nahitimu bachelor mwaka huu,
Hivyo sina work experience na leadership experience. Je, naweza kuapply au niache kwa kuwa haitawezekana!

Na pia gharama za usafiri umesema nitagharamia mwenyewe, Je inaweza cost kama kiasi gani mpaka kufika!?
 
Scholarships nyingi kwa uzoefu wangu zinahitaji work experience. Ila pia moja kwa moja bila work experience inawezekana. Unaweza kupata kwa njia nyingine ila uwe na ufaulu mkubwa sana. Unfortunately, scholarships za namna hii sina experience nazo sana kwahiyo siwezi kuwa na msaada mkubwa kwako. Ushauri wangu ni kuwa usiache kujaribu. Jifunze namna nzuri ya kutumia mitandao maana mtandaoni kuna kila taarifa.

Kuhusu nauli inategemea na msimu uliokata ticket na muda wa tarehe ya kukata ticket mpaka siku ya kusafiri. Gharama za ticket ya ndege kwenda Ulaya kwa one way, kwa wastani ni kati ya 1.5M - 2.5M kwa Economy class.
 
Ahsa
Taasisi inayotoa full funded Scholarship ya Masters kwa Sweden kwa nchi yetu inaitwa Swedish Institute Scholarships for Global Professionals (SISGP). Kwa kuanzia inatakiwa ufanye application kupata admission katika moja au vyuo husika unavyohitaji kusoma.

Dirisha la kufanya application kwa ajili ya admission hutolewa kuanzia kipindi cha mwezi kama October hivi na kukamilika Januari. Hivyo, kwa mwaka huu wa masomo utakuwa umechelewa, ukihitaji basi itakuwa kwa ajili ya mwaka ujao wa masomo. Baada ya hapo, kaunzia Januari mpaka februari huwa ni kipindi cha application kwa ajili ya Scholarship.

Link kwa jaili ya apllication ya admission ni hii hapa..>>>>Apply to Swedish universities, courses, and programmes: University Admissions in Sweden – Universityadmissions.se
Na link kwa ajili ya application ya Scholarship ni hii hapa..>>>>Swedish Institute Scholarships for Global Professionals | Swedish Institute
Ahsante Sana Mkuu Kwa huu Uzi maana watu wetu wa karibu waliopata hzo scholarship ukimuuliza atakwambia easy tu unaingia mtandaoni una apply halafu unasikilizia, Sasa ili usionekane mnyonge unamkubalia tu fresh ntaingia mtandaoni.

Mimi naomba kujua kama Kwa mwezi Huu naweza kupata admission na kuitumia ku apply scholarship nakupata?
Na hiyo admission fee ya 900SEK Inakua Kwa program ngapi?
 
Habari zenu wote? nimefanikiwa kupata admission mwaka huu Sweden lkn sijapata SI scholarship...je kuna namna yeyote ya kupata mkopo/mfadhili ndani au nje ya nchi?? Anayefahamu anijulishe kwani muda wa mwisho wa kulipa ada ni 15 Mei 2023...natanguliza shukrani.
 
Dah mkuu nna experience kama yako, inaumiza sana ndoto zinapozimika. Nimekosa scholarship nilipata chuo Malmo.

Heaven Seeker atatusaidia labda mwakani tuboreshe wapi. Sweden is my dream country
 
Ndugu zangu naombeni hapa tusaidiane kabla sijamlipia kijana wangu hapa je baada ya course hii inayotolewa British counsel kwa miezi mutatu nitakuja kulipia tena mtihani wake ili kupata cheti
1000031246.jpg
 
Hongera sana mkuu kwa Uzi huu... Utakuwa very helpful maana Nina ndoto za kwenda kupiga shule ya masters Ulaya...
 
Back
Top Bottom