Naingia Shambani very serious kulima Alizeti

Dada yangu nipitishie, mm nimeshavuna, bado eneo moja nitaenda May mwishoni, eka 15 za mwanzo nimepatwa gunia 18 nyingine imebaki shambani wataivuna baadae
Walichoniudhi wananishauri niiuze kila gunia 90,000/ na kuna walanguzi kibao wanasarandia
Ila imenikata NI wastani wa gunia moja na nusu kwa eka, pia upepetaji mbaya, wamedondosha Sana Alizeti ambapo huenda nilipoondoka waliirudia
Ukweli ndio huo nimepigwa ngoja nisikie wenzangu km wanapaita guni 18 kwa eka HICHO NDIO NAKATAA
Mpaka sasa sijajua hilo gunia ni debe ngapi mweeh😥
 
Ardhi inayofaa alizet ni ipi mm nachanganyikiwa wengine anasema dongo nyekundu sio nzuri wengine anasema mfinyanzi sio nzuri wajuzi tuelimishane
 
Wakuu naombeni tathmini ya mbegu zilizotolewa na serikali binafsi nimeiona changamoto.
 
Nipo very interested na hii kitu mnayo izungumzia huku na isitoshe mimi ni makazi wa hayo maeneo panaitwa NDAGO
 
Nipo very interested na hii kitu mnayo izungumzia huku na isitoshe mimi ni makazi wa hayo maeneo panaitwa NDAGO
Mayu mbona hujarudi kuwaelewesha hawa watu,
hebu waepushe na hasara watakayoipata
KILIMO CHA ALIZETI kinakata jamani mpaka leo namjavuna
tunataka mahesabu ya kilimo hicho
 
Wakalime wataelewa tu ukitaka kuujua utamu wa ngoma ingia kati isakate
 
Wakalime wataelewa tu ukitaka kuujua utamu wa ngoma ingia kati isakate
ni dhambi kubwa kuwaingiza wenzako MKENGE
toka mwanzo tuliwatahadharisha member kuwa Alizeti inawakata wakulima jamani, kwenye matikiti maji (water lemon) tuliwaambia vivi hivi.
 
Nimejitahid nimenunua gunia 64 za alizeti lakn shambani kwangu heka 2 nimepata roba 5.

Kilimo Uti wa mgongo
 
Mkuu, Alizeti Gunia la Debe Saba Makadirio mazuri ni Lita 20 tu sawa na Dumu moja. maana hapo nimeona unasema itakupa Dum mbili sawa na lita 40 ambacho hicho kitu hakina uhalisia sana kwa sababu nimelima sana Alizeti,Huko jirani na Singida maeneo ya Kondoa pale
Habari mkuu,, vip alizeti kondoa inastawi vizuri ?
 
Wakalime wataelewa tu ukitaka kuujua utamu wa ngoma ingia kati isakate
Mkuu wewe unaishi huko ndago au ni kwenu ila unaishi mjini?

Asilimia kubwa ndago alizeti wanalima kama shamba la ziada baada ya kumaliza kulima mahindi

Wanapanda kwa kumwaga mbegu(kuminza) halafu ndio wanalima, palizi yenyewe ya juu juu tu, hawapunguzii mimea nk
Kulima hivi ni kilimo cha mafuta ya kula tu
 
ni dhambi kubwa kuwaingiza wenzako MKENGE
toka mwanzo tuliwatahadharisha member kuwa Alizeti inawakata wakulima jamani, kwenye matikiti maji (water lemon) tuliwaambia vivi hivi.
Mkuu niwaingize watu mkenge ili nipate nini sasa?
Nime share kila hatua hapa toka mwanzo hadi mwisho kwa kufanya updates kwenye thread No 1

Biashara yoyote ile ina risk ya hasara
Natamani kujua kama ulilima Alizeti na ikakukata ulilima kwa mfumo upi? Ulipata kiasi gani? Nk

Asikudanganye mtu kilimo ni kigumu na kinataka uwe front mwenyewe
Lakini pia kilimo kinataka ufuate kanuni zake na sio kwenda kienyeji
 
Mkuu wewe unaishi huko ndago au ni kwenu ila unaishi mjini?

Asilimia kubwa ndago alizeti wanalima kama shamba la ziada baada ya kumaliza kulima mahindi

Wanapanda kwa kumwaga mbegu(kuminza) halafu ndio wanalima, palizi yenyewe ya juu juu tu, hawapunguzii mimea nk
Kulima hivi ni kilimo cha mafuta ya kula tu
Naishi Ndago na nina ishi mjini pia kwa vipindi tofauti tofauti. Kuhusu kilimo cha alizeti nafahamu nje ndani. Kuhusu watu wa Ndago ni kweli huwa wana fanya ziada kilimo cha alizeti walio wengi na huwa wana tumia aina ya kienyeji ya upandaji (kumimza)
 
Mkuu mwakani andaa shamba ekari moja kwenye mbuga isio jaa sana maji au kwenye nkulusi
Kama ni kichanga hakikisha unatumia mbolea ya kukuzia

Lima mapema kabisa mwezi wa 12 uwe umemaliza kulima alizeti

Panda mbegu ya kisasa kwa mstari na vipimo sahihi, ngolea libaki shina moja moja na mawili kwenye vichuguu au shamba lenye rutuba sana.

Palilia kwa wakati na palizi ya maana kama unavyopalilia mahindi( sio kuparaza kama wanavyofanya)

Kama aridhi ni kichanga weka mbolea ya kukuzia baada ya palizi

Vuna mapema usiache alizeti ikauke hadi ianze kupukutika na upepo au wakati wa kuvuna

Omba Mungu wako nvua zinyeshe za kutosha

Utanishukuru baadae

Usilime alizeti mwishoni mwezi wa pili huko
Usipande mbegu za kienyeji wala usipande kienyeji kwa kumwaga mbegu
Usiache mimea imebanana itazaa alizeti kama ngumi
Usianze palizi baada ya mimea kuzongwa na majani itadumaa
Usipalilie juu juu, palilia kama mahindi yanavyotaka
 
Back
Top Bottom