Midomo ya mwanamke ina uhusiano na uke wake yaani kama akiwa na midomo mikubwa na uke wake unaweza kuwa mkubwa?
- Tunachokijua
- Uke ni kiungo kinachounda sehemu ya mfumo na mfereji wa uzazi wa mwanamke ambacho hufanya kazi kuu tatu ambazo ni;
- Kuruhusu utoaji wa masalia ya damu na tishu za mji wa uzazi kupitia hedhi.
- Kupokea uume wakati wa kushiriki tendo la ndoa pamoja na kuhifadhi mbegu za kiume kwa mda hadi zitakapo ufikia mji wa uzazi.
- Kuruhusu kupita kwa mtoto wakati wa uchungu wa kuzaa.
Mashavu yanayozunguka uke ambayo kitaalamu huitwa labia huwa na muonekano wa aina nyingi ambazo hutofautiana miongoni mwa wanawake. Kwa baadhi yao, labia hizi huwa ni kubwa, huonekana zimevimba, nyembamba, zimechomoza nje na wengine huwa wazi kiasi cha kufanya baadhi ya sehemu za ndani zionekane kirahisi.
Pamoja na uwepo wa tofauti hizi, JamiiForums inatambua kuwa ukuaji wa uke na labia zake pamoja na ukuaji wa midomo vyote kwa pamoja huongozwa na taarifa za kijenetiki (Genetics) na homoni za mwili.
Pia, JamiiForums imefanya mazungumzo na Madaktari Bingwa wa Masuala ya wanawake waliothibitisha kuwa ukubwa wa midomo na uke huwa havina uhusiano.
Aidha, hakuna maelezo yoyote ya kitafiti yanayothibitisha uhusiano wa ukubwa wa midomo na ukubwa wa uke hivyo mwanamke anaweza kuwa na uke mkubwa pasipo kujali udogo wa midomo yake, pia anaweza kuwa na uke mdogo hata ikiwa muonekano wa umbo la midomo yake ni mdogo.
Suala hili halina uthibitisho wa hoja za kisayansi hivyo linabaki kuwa ni uzushi.