Alubati
JF-Expert Member
- May 29, 2016
- 5,832
- 12,462
Ulemavu ni hali ya mtu kuwa na upungufu kimwili ambao hufanya iwe vigumu kufanya shughuli kulingana na mazingira yanayomzunguka. Kuna aina nyingi za ulemavu kama usikivu hafifu, ulemavu wa viungo vya nje ya mwili kama kama miguu, ulemavu wa ngozi,ulemavu wa kutoweka kutamka maneno, kushindwa kuona au uoni hafifu n.k.
Jamii hii ya watu wenye ulemavu imekuwa ikikosa fursa ta ushiriki kwenye mchakato wa kupata ajira kwenye vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kama : Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jeshi la Kujenga Taifa(JKT), Jeshi la polisi, Jeshi la Magereza,Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,Jeshi la Uhamiaji na Usalama wa Taifa.
Ulemavu si ugonjwa ninapendekeza Tanzania tuitakayo iunde sera na mkakati kuhusu watu wenye ulemavu kwa kuwapatia nafasi maalumu za ajira kwenye majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama hasa wali waliohitimu mafunzo katika vyuo vya ufundi stadi, Stashada na Shahada katika vyuo vya kati na vyuo vikuu katika taaluma ya fani mbalimbali kama Udaktari wa mifugo na binadamu, wataalamu wa Uchumi, Wahandisi mitambo, umeme, na miundombinu kama barabara, wataalamu wa kompyuta na mawasiliano,wataalamu wa nyuklia n.k.
Sera hii ya ajira kwa watu wenye ulemavu ijikite katika mafunzo maalumu ya kijeshi kulingana na aina ya ulemavu wa wahusika,na shughuli kiutendaji kwao zihusu katika kuhudumia jamii ya waTanzania katika kazi za kiofisi bila ya wao kuhusishwa katika operesheni za mapambano mstari wa mbele (frontline).
Nafahamu suala la utimamu wa mwili ni jambo la kuzingatia katika katika kutoa nafasi za ajira kwenye majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama, lakini kupitia kuundwa sera na mkakati maalumu kuhusu ajira kwa watu wenye ulemavu kwenye majeshi yetu kunaweza kuleta tija na matokeo chanya kwakuwa watu hawa wana uwezo mkubwa kiutendaji katika fani mbalimbali. Pia itasaidia kuimarisha mahusiano baina ya majeshi yetu ya Ulinzi na Usalama na Jamii ya watu wenye ulemavu kwa kuwa kwa sasa ajira kwa watu wenye ulemavu katika majeshi yetu limekuwa ni jambo lisilowezekana.