Kataa kitambi, unene kupindukia sio afya

Arnold Kalikawe

Senior Member
Sep 28, 2016
147
341
Siku zote, wenzetu wanakula, na wakila, wanakula vyakula ambavyo vinajenga miili yao. Zamani chakula kama hiki hakikuwepo Tanzania, lakini siku hizi vipo vingi tu.

Tembelea supamaketi ukakutane na vyakula mbalimbali, vyenye afya, sisi tunakula ila ulajibwetu ni wa kijinga. Ndiyo! Ni wa kijinga.

Unakula msosi, unabaki vilevile ila unaanza kupata kitambi. What the f*ck. Hutakiwi kupata kitambi ila unatakiwa kupata mwili. Tafuta mwili na usitafute kitambi. Mabilionea wakubwa hawana vitambi, cheki namba moja mpaka tano, why wewe uwe na kitambi?

So hata kama mwembamba kama mimi, ukitaka kunenepa kula sana protini na wanga, tena na unatakiwa kula sana. Unajua sisi hatuliz tunagusagusa tu, Wasukuma wanakula sana, angalia miili yao.

Mwili unahitaji chakula, usidanganyike eti kunenepa ni kuridhika. Lazima ule, ili mishipa itanuke, inahitaji chakula na hakuna namna.

Mwanamke akiolewa, ananenepa, kwa nini? Kwa sababu ataanza kula bila stress ya kukosa msosi lakini akiwa kitandani, napo anaingiziwa chakula cha kutosha mwilini mwake.

Kwa nini mwanaume akifanya mapenzi sana anakonda? Kwa sababu anaroa chakula kingi mwilini. Mshindi mmoja tu, wanasema ni sawa na kukimbia Dar mpaka Kibaha.

Wabongo ukiwaambia kunenepa, wanakimbilia kitambi. Jamani, kitambi ni ugonjwa, watu wa afya huwa hawapendi sana vitambi.

Pendelea kula chakula, achana na ugali wa mara kwa mara, huo ndiyo unakuletea mtambi.

Kunenepa kwako kunatakiwa hapa mbele kuende sambamba, unamuona mtu mwenye six packs kama mimi? Hapa mbele kupo sawasawa na kifua, so hata ukinenepa unatakiwa tumbo lako liwe sawasawa na kifua. Sio tumbo limetangulia, kifua kipo nyuma.

Hatuli vizuri, na tukila tunakula hovyohovyo. Kijana mdogo wa miaka 25 tayari ana kitambi, kula ila epuka sana kula mafuta, yana madhara makubwa sana, na kama unakula hayo, jitahidi ufanye mazoezi.

Epukeni vitambi ndugu zangu ila hakikisha mwili wako unakuwa na chakula cha kutosha, na usile hovyohovyo, lazima upangilie kwamba asubuhi nitaingiza protini, mchana wanga na usiku chakula fulani, sio daily unakula wanga tu.

Jitahidini kunywa maziwa, kula mayai na maparachichi, ukikosa, usipitishe siku bila kula ndizi.

Tujitahidi tusiwe tunafakamia vyakula mpaka tunapata vitambi. Kataa kitambi kama Zuckerberg ama Cristiano Ronaldo.

Pangilia msosi wako, kuwa na kitambi sio sifa, ni dalili za kuonyesha unafakamia vyakula bila utaratibu.
 
VYakula vinavyoongeza uwezo wa kufikiri huondoa kitambi. Kwa maana hiyo....
 
VYakula vinavyoongeza uwezo wa kufikiri huondoa kitambi. Kwa maana hiyo.....
Kama hutojali mkuu, naomba nifahamishe hivyo vyakula vinavyo ongeza uwezo wa kufikiri.... Natanguliza shukrani 🤒😎
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Kuwa na kitambi ili hali mwili wako ni mwembamba inakufanya uonekane kama kamtu fulani hivi kenye utapiamlo au unyafuzi 🤒😎
 
Back
Top Bottom