hometown
JF-Expert Member
- Jul 30, 2016
- 939
- 1,302
Mpaka hapo kwa mawazo yangu nadhani muungano ubaki tu kwa raia, kila nchi ijimiliki yenyewe, ila sisi raia tuwe free na undugu wetu,Naomba kueleweshwa, kinachosababisha Tanganyika na Zanzibar ziitwe nchi zilizoungana ni kipi? Nauliza haya kwa sababu
1.) Kila nchi ina Rais wake
2.) Kila nchi ina katiba yake
3.) Kila nchi inajeshi lake
4.) Kila nchi ina mamlaka yake ya mapato na mamlaka zingine zote husika katika kuemdesha nchi
5.) Kila mchi ina bunge lake
Kilichokuwa kimebaki ni katika Mambo ya soccer, lakini hata hilo nalo liko mbioni kuondoka, na kila nchi itakuwa na timu yake ya taifa. Sasa hiki kinachoitwa Muungano ni kwa vigezo vipi?
- Raia wa Zanzibar kutawala Tanganyika ila kinyume chake ni marufuku?
- Raia wa Zanzibar kumiliki ardhi Tanganyika ila kinyume chake ni marufuku?
- Mkopo kukopwa na Zanzibar ila deni kulipishwa Tanganyika?
- Kodi zikusanywe Tanganyika ila mapato yakatumike Zanzibar?
- Umeme utoke Tanganyika kwenye mgao wa umeme kisha uende Zanzibar bure bila malipo?
- Wanafunzi watole Zanzibar waje kusoma Tanganyika ila mkopo wachukue bodi ya mikopo ya Tanganyika?
- Wabunge toka Zanzibar kushiriki bunge la Tanganyika na kula posho za waTanganyika ila kinyume chake ni marufuku?
- Utambulisho wa Tanganyika kuzikwa ilihali utambulisho wa Zanzibar unaachwa uishi?
Hicho ndio kinasababisha huu uitwe Muungano, au kuna jambo lingine?
Zanzibar iwe na uhuru wake nasi Tanganyika tuwe na uhuru wetu
Mali ya zanzibar iwe yao hata kama ni kijiko
Vivyo hivyo nasi pia