Ifahamu Rebar Coupler: Teknolojia mpya ya kuunganisha nondo ukiwa site ili kupunguza matumizi ya nondo

Limbu Nation

Member
Apr 18, 2024
15
5
Rebar coupler, ni aina mpya ya uunganishaji wa nondo za nguzo (column) au nondo za beam au za retaining walls wakati wa zoezi la ufungaji wa chuma (usukaji wa nondo).

Aina hii hutumiwa zaidi na wachina katika shughuli ya ujenzi. Mfano katika ujenzi wa bwawa umeme la mwalimu Nyerere (JNN) teknolojia/Mbinu Hii imetumika pia.

Mbinu hii humsaidia mteja/mshitiri (client) kutumia gharama ndogo sana katika matumizi ya nondo ambayo huhitaji ghama kubwa katika manunuzi.

Hii pia humsaidia mkandarasi kupunguza matumizi ya nondo ukiwa kazini na kuongeza faida kwa kupunguza gharama za manunuzi.

Kila mmoja anayo nafasi ya kutumia teknolojia hii mpya hapa nchini na kwenye kazi unazo zipata.

Badala ya ku overlap nondo kwa nondo kwa mita moja (1m) unatumia rebar coupler kupunguza na kuokoa matumizi ya 2M (mita mbili) ambazo unge tumia.

NB: kanuni ya kuunganisha nondo ukiwa site ni 50D for maximum na 40D for minimum overlap.

Yapo mengi kuhusu hili wasiliana na sisi kupitia 0621003092 tukupe ushauri na maelezo ya ziada Buuureeee kabisa.

Au fuatilia kwenye Google “Rebar Coupler “ kwa maelezo zaidi.

9BF95882-4EE7-4BAE-BAF1-74AED1121828.jpeg
2C6C3460-65D2-410E-BAEE-D93616882040.jpeg
 
Back
Top Bottom