Hivi kati ya Mbagala, Gongo la Mbotoa na Mbezi Mwisho sehemu gani kuna mzunguko mkubwa wa pesa

Habrin wanajf
Swali langu ni kama hivo lilivyo naomba tujuzane kwa mwenye uelewa
ZINGATIENI NATAKA KUFUNGUA DUKA LA NAFAKA
Kwa hizo location ipi itafit hapo
Kuna mizunguko ya hela ya aina mbili
Mizunguko

1.mzunguko kajambanani

Huu ni aina ya mzunguko wa hela buku mia tano 5000 mara 10000.......eneo husika linakuwa lina biashara ndogo ndogo nyingi hata serikali haini jinsi ya kukata kodi inapotezea TRA ....jiji ndo wanachukua hizi kodi za kina kajamba nani...vibiashara mara kuuza ndizi mara kutandika mara viosk uchwala mara tigo pesa ambayo hata laki moja haiwez kutoa hela nyingi unaweza toa 50000..... hapa mizinguko hiii ipo mbagala sana na maaneo yao fanana mbagala hapa mbezi mwisho nao wapo kwenye mzunguko kajamba nani tu hakuna cha maana sana


2.MZUNGUKO MSHINDOO
Hawa ndo wazee simu unasikia nimetuma million 50 umeona .....mara contena zimefika ....mara billion moja nadaiwa tra kodi..... mara million mia moja sijui imefanya nini hujakaa saa mara na kikao na polisi na TRA...... mara takukuru wanakufuatilia....mara nyingi watu wa mzunguko mshindo ndo wanachangia pato la taifa kiasi kikubwa biashara zao nyingi zipo mitaa kariakoo pugu road yote hadi uwanja wa ndege kuja viwanda vya mikocheni kwenda kuranisi kwenye ma ware house yale .... hawa ndo wanakopa hadi billion 100 bank..... wengine billion 10 yaani wanakopeshaka wanaaminika kiasi kikubwa

Ukiwa unapita pugu road kwenda uwanja wa ndege PEMBENI UKIANGALIA NDO UCHUMI WA TAIFA😁😁😁😁

Sasa jiangalia biashara unayofanya ni mzunguko kajamba nani au mzunguko mshindo......Nawasilisha
 
Back
Top Bottom