Inasikitisha sana tunapoona viongozi waandamizi wa nchi hasa wabunge wakikubali kununua cheap doctorates kutoka vyuo vya kitapeli (rogue colleges). Hiyo inakupa picha kwamba hawa viongozi wetu hawajui hata kuangalia authenticity wakati kila kitu kipo online. Kwanza hiki sio chuo maana hakina address, hakina majengo na wala hakina makao makuu yanayoeleweka. Ni taasisi ya kijanjajanja tuu iliyoanzishwa na matapeli kwa ajili ya kuwatapeli watu wanaotaka umashuhuri nafuu hasa wa udaktari bila kutumia jasho
Hiki chuo kilichowapa udaktari wa heshima Mbunge Musukuma na wenzake kina kashfa ya siku nyingi ya kuuza hizi degree za heshima. Ukweli ni kwamba wanauza na sio wanatoa bure ama kulingana na mafanikio uliyonayo katika nyanja husika...