Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Ingekuwa muungano tuliutaka sisi ndiyo ungesema yote hayo. Huu muungano ni wa Uingereza na Mmarekani. Kama wao hawautaki utavunjika siku moja tu.

Tumewachiwa dudu la "divide and rule" sisi kwa ujinga wetu tunaona tuna muungano.
BIG OK
 
Wazanzibari walipodai Zanzibar yao, hakuna madhara makuwa yaliyojitokeza labda tu kule kuchafuka kwa hali ya kisiasa; leo waTanganyika wakidai Tanganyika yao eti kutatokea madhara makubwa!
Ninachoona ni kuwa Watanganyika walikuwa wamelala sasa wanaamshwa kudai Tanganyika yao, wapewe kama Wazanzibari walivyopewa Zanzibar yao.
Utasikia Mzanzobari anasema 'tunajitambua' na Katiba yao inawatambua kuwa wao ni Wazanzibari lakini Watanganyika hawajajitambua na Katiba haimyambui Mtanganyika bali inamchanganya na Mzanzibari kuwa wote ni Watanzania- Shida iko hapo.
Sasa Wazanzibari wanasema wamemezwa na Tanganyika, na Watanganyika wanasema wamemezwa na Tanzania maana yaye wote hawaridhiki na hali ilivyo - wote wasikilizwe ili muafaka mpya upatikane.
Muungano uvunjwe haraka
 
Hizi hisia ni za zamani sana kwamba Zanzibar ikiachwa itaangukia kwa alshababi. Tukubali kuwa Dunia imesonga mbele na siyo kama zamani. Umetoa mfano mzuri kuwa vipo visiwa vya usheli na comoro ambvyo vipo jirani na vipo salama kwamba havina hao maadui je woga huo kwetu unatoka wapi. Lakini pia ujue hauwezi endelea kukaa na mtu asiyekutaka ukadhani utamtawala milele siku ya kutoka ni vita kama Urusi na ukraine je ndivyo unataka itokee

Ama kuleta hii mifano ya mikoa yenye uchumi kujitenga bado unatembelea kivuli cha Nyerere ambacho kwa wakati ule ilikuwa sahihi lakini pia uelewe Zanzibar tayari ni nchi iliyo na Rais, tamaduni, na mambo mengi ya ki mamlaka kama nchi, hivyo mfano huo hauwezi kuwa halisi kwa mikoa ya bara kujitenga.
Muungano uvunjwe
 
Hata Wayemen ambao ndio wakorofi waliachana na kurudiana na kuachana
Itakuwa sisi?
Kama tunapenda sana visiwa mbona tunavyo na kama tunaogopa Usalama wetu, ambayo ni maneno ya kisiasa tu hayana uhalisia hata chembe zaidi ya chuki

Eti mwarabu atarudi hivi leo wakitaka kununua visiwa ambavyo havikaliwi na mtu watashindwa?
Maana duniani Kuna visiwa vya kuuzwa na watu wananunua
Wapige kura ndio jibu sahihi hata Scotland walipiga kura ila wengi wakaipa Uingereza iendelee
 
Mdanganyika ukienda zenj unaonekana hufai kwa kilakitu unabaguliwa, hata ukiwa ni swala 5 watakuita wewe ni swala 5 jina tu umejaa ukafiri... Mzenj akija bara hasumbuliwi haulizwi kwa lolote anamilik ardhi nyumba na cheo anapewa... Halafu mnasema kuna usawa na haki... Ifike mahala kilamtu ashike 50 zake... Kodi anakamuliwa bibi yako kule kishumundu ludewa chunya ileje na koromije ila anapelekewa ale kodi mzenj asiyejua hata kulima mbogamboga...
 
Kwa hapa tulipofikia ccm lazima wajue kizazi kimebadilika, na yenyewe sio sehemu ya kizazi hiki. Ni vyema wakaruhusu rasimu ya Warioba itengeneze katiba yenye maoni halisi ya wananchi, na sio katiba ya kuifanya ccm isalie madarakani. Kinyume na hapo machafuko ama mapinduzi ya kijeshi lazima yatatokea hapa nchini Ili kupata mabadiliko ya kweli.
Mapinduzi ya kijeshi kwa Tanzania ni ngumu kidogo ila ntaungana na wewe kwenye mabaadiliko ya kimazingira, utashi na uelewa wa wananchi.

Kuhusu machafuko HAPANA bado kwa aina ya jamii ya kitanzania hatujafikia huko.
 
Mapinduzi ya kijeshi kwa Tanzania ni ngumu kidogo ila ntaungana na wewe kwenye mabaadiliko ya kimazingira, utashi na uelewa wa wananchi.

Kuhusu machafuko HAPANA bado kwa aina ya jamii ya kitanzania hatujafikia huko.
Hatuko mbali sana na huko.
 
Hujui au umejisahaulisha kuwa katika Muungano wetu kimekufa kimoja tu, kingine kikabaki; katika hali hiyo hoja yako ya chemical reaction to form a compound si sahihi. Kwa mantiki hayo hayo basi hii ni mixture.
Kunahitaka sana elimu ya uraia kuhusu huu Muungano wetu, ni muungano adimu na adhimu.
1. Kimataifa ni Muungano wa Union, nchi mbili zimeungana, zimekuwa fused together into a new compound, JMT, both countries died, nchi ni moja na Rais mmoja.
2. Kitaifa ni Muungano wa federation ya nchi mbili na marais wawili, Tanganyika changed it's name to Tanzania Bara, Zanzibar maintained it's name, Zanzibar but both have no sovereignty, the sovereign is JMT.

Hivyo hiyo Zanzibar sio nchi ni sehemu ya JMT yenye utawala wake wa ndani.
P
 
Back
Top Bottom