Uhasama wa Tanzania bara na Zanzibar unazidi kukua na utaleta madhara makubwa kama yanayosemwa hayatashughulikiwa

Synthesizer

Platinum Member
Feb 15, 2010
11,208
19,001
Jinsi masuala ya muungano yanavyoshughulikiwa na kwa sasa, ni mtu kipofu wa akili tu ndio hataona kwamba kadiri siku zinavyopita mbegu za uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar inazidi kuota mizizi, majani ya chuki yakizidi kuchanua. Ni kiongozi mjinga tu asieweza kuona kwamba jinsi haya mambo ya muungano yanakoenda, yanaweza kusababisha mgongano (confrontation) mkubwa sana kati ya wakazi wa Zanzibar walioko bara na wakazi wa bara walioko Zanzibar.

Badala ya kujibu hoja zinazowekwa mezani, viongozi wameamua kwa makusudi kuwashambulia wale wanaozitoa, bila kuona kuwa kwa kufanya hivyo wanazidi kuchochea uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Kwa kumfurahisha nani?

Kama Tanzania bara wanaona kwamba kwao kero kubwa ya muungano ni kutokuwa na serikali ya Tanganyika, kwa nini hawasikilizwi? Wakati wa Nyerere huenda kulikuwa na sababu za msingi kuwa na serikali mbili, lakini ni wazi hilo halikubaliki kwa sasa, na huwezi kulilazimisha likaendelea kuwapo bila kuleta madhara.

Muungano tunaweza kulazimishwa uendelee kuwapo kwa kutumia nguvu ya dola, lakini haitazuia watu kuanza violence (kupigana) uhasama unaojitokea ukizidi kukua. Amini nawaambieni, huu muungano mnaodai uko imara unaweza kuvunjwa kwa nguvu na kuleta hali ya machafuko bara na visiwani. Watanzania bara walioko visiwani wataondolewa kule kwa nguvu, na wa-Zanzibar walikoko bara wataondolewa huku kwa nguvu, na hata kupoteza mali au uhai wao. Ndilo tunalosubiri? Au tunadhani haliwezi kutokea Tanzania, vitu kama hivyo vinatokea Rwanda tu?

Muungano ulifanyika zaidi ili Zanzibar kusiwe na counter-revolution ya Waarabu (wajomba) walipopinduliwa na kuchinjwa, na kwa Tanganyika kulinda usalama wake katika kuwa kitovu cha kupigania uhuru wa Afrika. Sasa hizi sababu sio hoja tena. Kama imefikia mahali Watanzania hawautaki muungano, basi ni bora uvunjwe kwa utaratibu na kuelewana, watu waulizwe je ungependa kubaki bara au kurudi visiwani, au ungependa kubaki visiwani au kurudi bara nk. Labda tuanze na "Referendum", wananchi ndio tuamue kidemokrasia kama tunataka au hatutaki muungano, sio serikali ituamulie kwa maslahi yake, au maslahi ya serikali ya Mapinduzi Zanzibar, au maslahi ya CCM.

Tusione aibu kukaa chini na kutafakari kuuvunja muungano, kama kuwa na serikali moja au tatu haiwezekani, kwa sababu mfumo wa muungano uliopo sasa hivi unazidi kukuza uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Mwaka 1982 Senegal na Gambia waliungana na kuwa nchi moja ya Senegambia. Iliposhindikana, waliuvunja muungano, mwaka 1989. Juzi hapa Uingereza imejitoa kwenye muungano wa Ulaya. Kwa hiyo Tanzania haitakuwa ya kwanza kuvunja muungano. Muungano ni mkataba.
 
Mambo mengi yaliyofanyika wakati ww Nyerere yalikuwa ya kulazimisha, na alitumia uelewa duni wa wananchi kuyaimplement. Kwa bahati mbaya washauri wake wengi yeye ndio aligeuka mshauri wao. Hata hii katiba tunayoipigia kelele leo hii, ilitungwa rasmi kuendana na utashi wake. Kibaya zaidi alijua ubaya wa katiba hii, lakini hakutaka kuibadili maana aliogopa chama chake Cha ccm kitang'olewa madarakani.

Kwa hapa tulipofikia ccm lazima wajue kizazi kimebadilika, na yenyewe sio sehemu ya kizazi hiki. Ni vyema wakaruhusu rasimu ya Warioba itengeneze katiba yenye maoni halisi ya wananchi, na sio katiba ya kuifanya ccm isalie madarakani. Kinyume na hapo machafuko ama mapinduzi ya kijeshi lazima yatatokea hapa nchini Ili kupata mabadiliko ya kweli.
 
Mambo mengi yaliyofanyika wakati ww Nyerere yalikuwa ya kulazimisha, na alitumia uelewa duni wa wananchi kuyaimplement. Kwa bahati mbaya washauri wake wengi yeye ndio aligeuka mshauri wao. Hata hii katiba tunayoipigia kelele leo hii, ilitungwa rasmi kuendana na utashi wake. Kibaya zaidi alijua ubaya wa katiba hii, lakini hakutaka kuibadili maana aliogopa chama chake Cha ccm kitang'olewa madarakani.

Kwa hapa tulipofikia ccm lazima wajue kizazi kimebadilika, na yenyewe sio sehemu ya kizazi hiki. Ni vyema wakaruhusu rasimu ya Warioba itengeneze katiba yenye maoni halisi ya wananchi, na sio katiba ya kuifanya ccm isalie madarakani. Kinyume na hapo machafuko ama mapinduzi ya kijeshi lazima yatatokea hapa nchini Ili kupata mabadiliko ya kweli.
Sababu za Nyerere na Karume kutaka kuungana haraka haraka zilikuwa za msingi sana. Lakini baada ya miaka kadhaa ya utulivu muungano ulipaswa kuwa reviewed. Lakini usisahau taifa la mwisho kupata utawala wa kidemokrasia kusini mwa Afrika lilikuwa South Africa, 1994. Nyerere alikuwa ameshaondoka. Ni baada ya 1994 Tanzania ilipaswa kusema wazi sababu zilizofanya kuwapo muungano hazikuwapo tena
 
Naunga MKONO HOJA, watu wenye akili,wangekaa chini,kuzitambua na kutatua kero zote za Muungano..na njia nzuri ni kuanza na KATIBA MPYA ILIYO BORA
Nikweli. Hadi sasa kero za muungano zimekuwa ni zile zinazohusu malalamiko ya Zanzibar kupewa mamlaka zaidi. Na viongozi wetu labda kwa makusudi au kwa kukosa uwezo wa kufikiri sawasawa, wametenda kwa namna ambayo kila hatua zinazochukuliwa kuondoa kile kinachoitwa kero za muungano, imesababisha muungano kudhoofika zaidi na Zanzibar kupata nguvu ya kujiona ni taifa huru zaidi nje ya muungano, na kutaka kujiongoza kuwa na mamlaka yao hata zaidi.

Sasa suluhisho za kero za muungano za wa-Zanzibar zimegeuka kuwa kero za muungano kwa Watanzania bara
 
Mpaka siku yatukie mazito ndo watasikua la sivyo wanakula bati tu.
Tuseme wazi, wanasubiri wasikie watu wamechinjwa kutokana na chuki za Ubara na Uzanzibar. Na ndani ya moyo wangu naona wazi hili litaanza Zanzibar, na huku bara watu wataanza kulipa kisasi. Zanzibar wameshaanza kuwaita watu wa bara kule majina ya kudhalilisha na kubagua, na hili limejitokeza sana katika kipindi hiki cha Raisi Samia
 
Jinsi masuala ya muungano yanavyoshughulikiwa na kwa sasa, ni mtu kipofu wa akili tu ndio hataona kwamba kadiri siku zinavyopita mbegu za uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar inazidi kuota mizizi, majani ya chuki yakizidi kuchanua.
Serikali 3 ni kurudi nyuma na madhara yatakuwa makubwa kwa raia. Bora kwenda mbele kwenye serikali moja.
Madhara ya erikali moja ni baadhi ya wanasiasa kukosa vyeo na madaraka.
 
Serikali 3 ni kurudi nyuma na madhara yatakuwa makubwa kwa raia. Bora kwenda mbele kwenye serikali moja.
Madhara ya erikali moja ni baadhi ya wanasiasa kukosa vyeo na madaraka.
madhara yatakuwa makubwa kwa raia? raia gani? tueleweshe, serikali tatu Tanganyika watapata madhara gani, na zanzibar watapata madhara gani.
 
Mwaka 1982 Senegal na Gambia waliungana na kuwa nchi moja ya Senegambia. Iliposhindikana, waliuvunja muungano, mwaka 1989. Juzi hapa Uingereza imejitoa kwenye muungano wa Ulaya. Kwa hiyo Tanzania haitakuwa ya kwanza kuvunja muungano.
Sheria iliyounda Senagambia, had provisions za kuuvunja. Ule ulikuwa ni mkataba, the same to UK kujitoa EU.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu ni Muungano wa dhima ya Muungano wa milele, zile Articles of the Union, sio mkataba, ni makubaliano ya milele, hakuna provision ya kuuvunja Muungano, tumeunganisha nchi mbili kwa kuchanganya udongo, na kuumwaga bara na Zanzibar, ili kuuvunja, lazima tuutafute ule udogo, tuupembue, punje za udongo wa Tanganyika, zirejeshwe Tanganyika na punje za Zanzibar zirejeshwe Zanzibar.

Kikemikali, muungano wetu ni compound na sio mixture!. Kikemikali, Ukichanganya vitu viwili na kuwa mixture, vitu hivyo vinakuwa havijaungana kikemikali, mfano kuchanhanya pombe na maji, kwa kutumia fractional distillation inawezekana kuitenganisha pombe na.maji. Vitu kama maji, H2Ounaweza kutenganisha hydrogen na oxygen, chumvi, unaweza hydrogen na.chlorine etc.

Lakini vitu viwili vinapoungana kwa chemical reaction, vitu viwili vile hufa na kuzaliwa kitu kipya kinachoitwa compound, huwezi tena kuvirejesha kwenye hali ya awali kama kuyeyusha sabuni ya unga kwenye maji, kunatokea chemical reaction, huwezi kutenganisha.

Huu Muungano wetu adimu na adhimu, ume undergo chemical reaction kwa mataifa mawili Tanganyika na Zanzibar kuungana, kupoteza utaifa wake.na kuunda taifa jipya la Tanzania ambalo ni compound, halivunjiki tena!.

Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote.
P
 
Tusione aibu kukaa chini na kutafakari kuuvunja muungano, kama kuwa na serikali moja au tatu haiwezekani, kwa sababu mfumo wa muungano uliopo sasa hivi unazidi kukuza uhasama kati ya Tanzania bara na Zanzibar. Mwaka 1982 Senegal na Gambia waliungana na kuwa nchi moja ya Senegambia. Iliposhindikana, waliuvunja muungano, mwaka 1989. Juzi hapa Uingereza imejitoa kwenye muungano wa Ulaya. Kwa hiyo Tanzania haitakuwa ya kwanza kuvunja muungano
Mkuu 'synthesizer', mimi nitakueleza kwa kifupi iwezekanavyo kitu muhimu kinachokosekana sasa. Uongozi.
Viongozi wa sasa ndio wanaozidi kuchochea hayo uliyoyaelezea hapo juu.

WaTanzania kwa ujumla wetu siyo watu wa kubaguana hata kidogo. Hali hii tulikuwa tunaisikia tu toka nchi zingine. MTanzania ulikuwa hata hufikirii ukifika Mtwara toka Mwanza itakuwaje, taratibu, hata hapa Tanganyika (naheshimu amri ya Joka), tunaanza/vimelea vimeanza kuota. Ukienda huko Usukumani, kama hujui kisukuma unaanza kujisikia mpweke sana, ndani ya nchi hii.

Kwa hiyo, bahati yetu mbaya sana, wakati tunapohitaji viongozi wa kutuleta karibu zaidi sisi raia wote, hii kazi hawaiwezi kabisa. Hakuna kiongozi yeyote kwa wakati huu anayeweza kusimama na kuijengea hoja ya kueleweka tatizo hili. Siyo Samia, Siyo Kikwete na wala, sijui nimtaje nani.
Kinachoonekana mbelle ya macho, hasa ya waTanganyika, ni kwa mZanzibar kuwajengea wigo zaidi watu wake huku Tanganyika. Usifikiri watu hawaoni, wanaona hata kama hawasemi kitu.
Kero zote zilizolegeza kila sehemu ya Muungano zimetokea Zanzibar, na kwa kiasi kikubwa sana zimetekelezwa; kwa msukumo wa waZanzibar wenyewe bila ya waTanganyika kushirikishwa. Zanzibar imejipambanuwa wazi kabisa, kwamba wapo njiani kupata madaraka yao kamili kama nchi. Pamebakia vitu vichache sana kutimiza azma hiyo, kama kuwa na jeshi; ambalo sasa wanalifanyia kazi na maswala ya Uhusiano wa Kimataifa. Wakikamilisha yote haya, hakuna sababu tena ya wao kujihusisha na huu muungano kiini macho.

Kuna kiongozi anayeweza kuuokoa huu muungano? Kwa maoni yangu ni kuwa 'It's too late'. Acha tusambaratike tu, kila mtu ashike lake.
 
Back
Top Bottom