Wito: Mdahalo uitishwe baina ya Lissu na viongozi wa CCM kuhusu hoja ya 'ubaguzi wa kimuungano'

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,419
35,969
Kumetokea patashika ya kisiasa tangu Tundu Lissu aushambulie muungano wa Tanzania kwenye kona ya kumgusa Rais Samia Suluhu kama mzanzibar katika kuamua (kikatiba) mambo mahususi ya watanganyika yenye kuathiri mustakabali wa maisha ya watanganyika moja kwa moja.

Lissu ametoa hoja zake akijificha kwenye kivuli cha katiba ya Tanzania (yenye kumpa mamlaka Rais Samia kuamua mustakabali wa watanganyika) na katiba ya Zanzibar (yenye kumtambua rais Samia kama raia kamili wa nchi ya zanzibar, na hapo hapo kutomtambua mtanganyika mwingine yoyote kwenye maslahi ya Zanzibar). Viongozi wa CCM wao wamejificha katika kivuli cha uzito wa maneno aliyotumia Lissu kuwa yana taswira ya kibaguzi na yenye kuchochea chuki dhidi ya rais halali wa Tanzania mwenye asili ya uzanzibar.

Kwa kuwa hoja inagusa muungano wetu, katiba yetu na umoja wa taifa letu, wadau mbalimbali wameomba kuitishwe mdahalo wa kisiasa wenye lengo la kumleta Lissu na kiongozi wa juu wa CCM katika kupambana kwa hoja ili watanzania tujifunze na kupima hoja zao.
 
Ccm hawana uwezo wa kujibu hoja za Lisu,hawana utamaduni wa kujibu hoja za aina hiyo. Nakumbuka wakati wa bunge maalumu la katiba Lisu alizua tafrani ya huo muungano hapakutosha. Ikatafutwa hati ya muungano ya mchongo. Naona kwa sasa ameibua tena hoja hiyo huku akiwa na mfano halisi wa rais mzanzibar kuuza raslimali za Tanganyika.
 
hawawezi kuitisha. kitu ambacho huwa najiuliza, binafsi sijawahi kuona faida ya muungano, pili, kila zinapoibuliwa kero, zipo tu kero za wazanzibar, sijawahi kusikia kuna kero za watu wa bara, kama kuna kero yeyote ya muungano kwa watu wa bara tuambieni? ipi kwanini tunatoa incentives kwa wazanzibar peke yake na bado wanatubagua na hawatupendi?

Kwanini wao hapa wanamiliki ardhi sisi kule hatumiliki? kwanini wao hapa wanakuwa marais sisi hatuwezi kuwa marais kwao? kwanini wanaajiriwa bara ila sisi hatuwezi kuajiriwa serikali yao? anayejua atuambie.
 
Ni kawaida ya Lissu kuzungumza mambo ambayo wengi huogopa kuyasema hadharani kwa sababu ya unafiki. Tundu Lissu huwa nasema sio mwanasiasa mzuri kwakuwa sio mnafiki, ni mwanaharakati zaidi.

Wengi wanaomtukana Lissu, pengine huwa wanayasema hayo aliyosema ila huwa wanayasemea uchochoroni na kwa usiri mkubwa.

Lissu alisimama peke yake wakati wa uongozi wa Rais JPM na akamsema wazi kuwa ni dikteta uchwara na anaongoza nchi bila kufuata sheria. Wengi wengi wa waliotoka hadharani na kusema anamtukana JPM ndio leo wanamuimbia mapambio Rais Samia kwa kurudisha uhuru kwa vyama pinzani kufanya siasa na mikutano yao.

Waliozoea vya kunyonga, vya kuchinja kwao ni haramu!
 
Hii katiba iliyopo ni kwa ajili ya nchi au ni kwa ajili ya ccm?
Mbona makando kando mengi sana?
 
Ni kawaida ya Lissu kuzungumza mambo ambayo wengi huogopa kuyasema hadharani kwa sababu ya unafiki. Tundu Lissu huwa nasema sio mwanasiasa mzuri kwakuwa sio mnafiki, ni mwanaharakati zaidi...
Unapokuwa na Taifa la watu milioni sitini, wanachukizwa na mambo yanavyoendeshwa, Ila wanasemea uchochoroni, anayesema hadharani wanamtukana na kumtisha, huku moyoni wanamuunga mkono, ni dalili za Taifa hilo kulogwa kwa mazindiko, tunahitaji kufunguliwa
 
Back
Top Bottom