Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,575
- 51,373
Kuna watu wanajaribu kuchukulia kauli za Lissu kukerwa na aina hii ya muungano kuwa eti anajaribi kuleta mgawanyiko wa Utanganyika na Uzanzibari.
Kiukweli kabisa kama ukifuatilia miongoni mwa watu waliojaribu kuwatetea Wazanzibari dhidi ya muungano huu ni Tundu Lissu. Lissu amekuwa consistent kwa muda mrefu kuwa muungano huu unawaumiza Wazanzibari sana, na kwamba Zanzibar imepoteza mengi kutokana na muundo huu wa muungano. Amefanya hivyo katika mijadala na hata katika mikutano ya hadhara. Nakumbuka amewahi kufanya mkutano mkubwa sana kule Zanzibar akieleza ni kwa namna gani muungano huu unavyowaumiza Wazanzibari.
Leo Lissu ameanza kuzungumza pia namna muungano unavyowaumiza Watanganyika, kuna watu wanatoka huko mbiombio kutaka kumnyamazisha!. Yaani Lissu akitetea wazanzibari hiyo inakuwa sawa, lakini akitetea Watanganyika hiyo inakuwa nongwa!. Kwa nini?
Ukimsikiliza Lissu kwa makini hana Tatizo na Uzanzibari wa Samia kama mtu ila ana tatizo na muundo wa muungano unaomfanya Mtu ale "kotekote" with impunity huku maslahi ya upande mmoja ( Wa Zanzibar yakilindwa kwa katiba yao) huku maslahi ya Tanganyika yakiwa hayana mtetezi (Kikatiba).
Leo inakuwaje Rais kutoka upande mmoja wa muungano anakuwa na mamlaka kwa mambo ya upande wa pili wa muungano ambayo siyo ya muungano?. Utalii siyo Jambo la muungano, iweje Mzanzibari awe na power ya kuwaamulia Watanganyika mambo yao ya utalii lakini mtanganyika hana power hizo kwa Zanzibar?
Leo tuna katiba ya Zanzibar, inayopingana hata na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mambo kedekede na hayo mambo yako wazi na yanajulikana na yako documented lakini watu wazima wamekaa kimya wanajifanya hawayaoni. Leo akitokea mtu kama Lissu akashikia bango mapungufu haya ili yaondolewe inabidi apongezwe siyo kubezwa!.
Katiba ya Zanzibar inasema Kutakuwa na "Mzanzibari" na imeorodhosha mzanzibari ni nani. Sasa Tujiulize Mzanzibari akishika madaraka ya Muungano kisha maslahi ya Zanzibar yakagongana na Maslahi ya Tanganyika katika mambo yasiyo ya Muungano yeye atatetea maslahi ya wapi?
Na katiba ya Zanzibar ikaenda mbele kusema kuwa Zanzibar ni nchi miongoni mwa nchi mbili ZINAZOUNDA jamhuri ya muungano wa Tanzania, Pigia msitari neno ZINAZOUNDA siyo ZILIZOUNDA, Sasa hiyo nchi nyingine inayounda muungano na Zanzibar iko wapi na kiongozi wake ni nani na watu wake ni akina nani?.
Hoja ya Lissu siyo Uzanzibari wa Samia. Hoja ya Lissu ni muundo mbovu wa Muungano. Uraisi wa Samia ni mfano tu kuonyesha muundo huo ulivyo na tatizo.
Ni mpaka tukae chini tusolve hili tatizo, la sivyo huko tuendako ni shida tu. Ndiyo maana leo Kuna Wazanzibari wanataka Watanganyika waende Zanzibar na Passport. Na mimi sioni shida Wazanzibar wakija Tanganyika kwa passport.