Watu Wengine Wanakufa Kabla ya Wakati

John Magongwe

Member
Jan 4, 2024
28
29
Watu Wengine Wanakufa Kabla ya Wakati

Kibiblia, kuna vifo ambavyo havistahili kutokea kwa mwanadamu, isipokuwa kutokana na sababu za kiroho, yaani za kiimani. Hii ni kutokana na kutokuwa timilifu katika imani na matendo yetu mbele ya Mungu. Sababu hizo zimeelezwa katika sehemu zinazofuata.

Maisha ya Dhambi
Dhambi ni mbaya. Inakutenga mbali na Mungu (Isaya 59:2; 1Yohana 3:4). Lakini kibaya zaidi, inapunguza maisha yako. Inakufanya ufe kabla ya muda wako.
Katika Warumi 6:23, Biblia inasema, “Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti (kifo), bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu”. Pia, katika Eze 18:20, Biblia inasema, "Roho itendayo dhambi, ndiyo itakayokufa; mwana hatauchukua uovu wa baba yake, wala baba hatauchukua uovu wa mwanawe, haki yake mwenye haki itakuwa juu yake, na uovu wake mwenye uovu utakuwa juu yake".
Maisha ya dhambi yanakata muda wa mtu kuishi. Ni wangapi waliokufa wakiwa vijana wadogo kwa sababu ya UKIMWI, kwa kutoikwepa dhambi ya uzinzi. Au, ni wezi wangapi wamekufa wakiwa katika harakati za kuiba.
Je, ni mzinzi, mwongo, msengenyaji, usiyesamehe, mwenye kinyongo, kisasi, nk? Ikiwa hivyo, unajipeleka kaburini kabla ya wakati wako. Unafanya kazi ambayo utapata mshahara uitwao ‘mauti’.

Kutomcha Mungu
Kumcha Mungu ni kuishi maisha yanayoongozwa na hofu ya Mungu. Ni maisha ambayo moyo, mwili, nafsi na roho ya mtu inakuwa imejawa na kiu na njaa ya kumpendeza Mungu na kuyafanya maagizo yake yote, tena kwa furaha.
Mithali 10:27 inasema, “kumcha bwana kwaongeza siku za mtu, bali miaka yao wasio haki itapunguzwa”. Pia, Mhubiri 7:17 inasema, “Usiwe mwovu kupita kiasi; wala usiwe mpumbavu; kwa nini ufe kabla ya wakati wako?”

Kwa mujibu wa ushahidi huo wa Neno la Mungu, ni dhahiri kuwa maisha yasiyo na uchaji Mungu na yasiyoongozwa na hofu ya Mungu, yanawafanya wengi wafe kabla ya muda wao waliokusudiwa kuishi.

Kumuwekea Mungu Mipaka
Hii ni hali ya mwanadamu kuamini kuwa Mungu anaweza hili na lile haliwezi. Kitendo hicho Mungu anakiita kuwa ni ‘dharau’ kwake. Zaburi 78:41 inasema, “Wakarudi nyuma wakamjaribu Mungu; Wakamwekea mpaka Mtakatifu wa Israel”.
Mstari huu wa Zaburi unaelezea maisha ya wana wa Israel njiani kutoka Misri kwenda nchi ya Kanaani. Ni kielelezo kuhusu kumuwekea Mungu mipaka.

Biblia inaeleza jinsi Musa alivyowatuma wapelelezi 12 kwenda kuipeleleza nchi ya ahadi, waone kama kweli ni nchi ya ‘maziwa na asali’. Waliporudi, 10 kati yao walirudisha ripoti ya kuwa kweli ile nchi ni ya maziwa na asali, ila, inakaliwa na Wanefili, wana wa Anaki, majitu, na ya kwamba wao ni kama panzi tu, na hawawezi kwenda kupigana nao na kuimiliki Kanaani. Yaani, pamoja na kuwa Mungu ndiye alikuwa anawapigania, wao waliona kuwa Mungu asingeweza kuyapiga majitu yale. Walimuwekea Mungu mpaka.

Wawili waliobaki, yaani Joshua na Kalebu, kati ya wale 10, walileta habari njema waliyoona kwa macho, lakini wakazungumza kile ambacho ni ‘uhakika wa mambo yatarajiwayo’. Wakamwamini Mungu kuwa anaweza kuwapa ile nchi kuwa milki yao sawa na alivyomwapia Ibrahim (Hesabu: 13, 14).

Wote waliomwekea Mungu mpaka katika uwezo wake walikufa huko jangwani, hawakuingia nchi ya Kanaani. Walifupisha maisha yao kwa kutokuamini kwao. Ila Kalebu aliishi muda mrefu sana, alikuwa na nguvu kama za mtu wa miaka 40 hata alipokuwa na miaka 85 (Joshua 14:6-14). Inaeleza pia kuwa Joshua alikuwa mzee sana, alikufa akiwa na miaka 110, lakini alikuwa na nguvu zake kamili mpaka pale Bwana alipompumzisha (Joshua 24:29)

Kama unataka kuwa na maisha marefu, na unataka kuziongeza siku zako, ishi maisha ya imani. Usimuwekee Mungu mipaka. Kumbuka kuwa “Njia zake zi juu mno na fahamu zake pia” (Isaya 55:8-11).

Kutoheshimu baba na mama
Biblia imesisitiza uhusiano mzuri na wa uhakika kati yetu na wazazi wetu, kinyume chake laana zitayaandama maisha yetu na maisha yetu hayatakuwa ya heri na marefu.
Waefeso 6:1-3 inasema, “Enyi watoto watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba na mama yako, amri hii ndiyo ya kwanza yenye ahadi (za ustawi, baraka na wingi wa miaka), upate heri, ukae siku nyingi (uishi siku nyingi) katika dunia”.

Pia, katika Kumbukumbu la Torati 5:16, Biblia inasema, “Waheshimu baba na mama yako; kama Bwana, Mungu wako alivyoamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako”

Kwa mujibu wa maneno hayo ya Mungu ni dhahiri kuwa watu wote wasioheshimu wazazi wao, ni ngumu kufanikiwa, laana zinawafuatilia, na hivyo wana muda mchache wa kuishi, wanakufa mapema.

Kutomtumikia Mungu
Biblia inasema katika kutoka 23:25-26, ”Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; Nami nitakuondolea ugonjwa kati yako, na hesabu ya siku zako nitaitimiza”.

Huo ni ukweli ambao unahitaji kuwekwa katika matendo. Je, unataka kuishi muda mrefu hapa duniani. Kazi ni rahisi tu. Mtumikie Bwana, naye ataitimiza hesabu ya siku zako. Hutakufa kabla ya wakati.

Kutokuwa na maono
Maono ni kuona ambacho hakionekani. Maono ni ndoto kujumlisha na uhalisia.

Katika Mithali 29:18, Biblia inasema kuwa pasipo maono, watu huacha kujizuia; bali ana heri mtu yule aishikaye sheria. Biblia inasema, “pasipo maono watu huangamia”. Biblia haisemi, pasipo fedha, watu huangamia. Biblia haisemi, pasipo chakula watu huangamia, bali pasipo maono watu huangamia.

Kuna usemi kuwa “Mtu bila maono ni mtu bila wakati ujao. Mtu bila wakati ujao atageukia wakati uliopita. Atausifia wakati uliopita".

Kuna mfano kuhusu wajenzi watatu waliokuwa wanajenga ukuta. Mpita njia alimuuliza wa kwanza, mnafanya nini? Alijibu, “tunapanga tofari.” Alimuuliza wa pili, mnafanya nini? Alijibu, tunajenga ukuta. Alimuuliza wa tatu, mnafanya nini? Akajibu, “tunajenga benki".

Wa kwanza hakuwa na maono. Kuna watu wanafanya shughuli zao kama vile wanapanga tofari. Hawana maono. Hawajui lengo la shughuli ni lipi. Wa pili naye hakuwa na maono, alifikiria ukuta badala ya benki. Hajui baada ya ukuta kitatokea nini. Wa tatu alikuwa na maono, yaani kujenga benki. Maono ni mtihani.

Kwa mujibu wa Biblia, (Mithali 29:18), mtu anayeishi ili mradi tu, asiyejua kwa nini yupo duniani, asiyekuwa na kusudi na mpango katika maisha yake, na asiyeweza kupanga hata mipango ya ‘kesho nitafanya nini’, yuko katika hatari kubwa ya kuondoka duniani kabla ya muda wake.

Kutompenda Mungu kwa Bidii
Katika Zaburi 91:14-16, Biblia inasema, “Kwa kuwa amekaza (ameweka bidii katika) kunipenda, Nitamwokoa; na kumuweka palipo juu (nitamwinua) kwa kuwa amenijua Jina langu. Ataniita nami nitamwitikia; Nitakuwa pamoja naye taabuni. Nitamwokoa na kumtukuza; kwa siku nyingi nitamshibisha, Nami nitamwonyesha wokovu wangu”

Biblia inasema atakayekkuwa na bidii katika kumpenda mungu atashibishwa kwa wingi wa siku. Yaani ataishi maisha marefu.
Yesu ameweka wazi ni namna gani unaweza kumpenda Yeye. Yohana 14:21 inasema, “Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye, naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; Nami nitampenda na kujidhihirisha kwake”.
Nayo Mithali 3:1-2 inasema, ”Mwanangu, usiisahau sheria yangu, bali moyo wako uzishike amri zangu. Maana zitakuongezea wingi wa siku, na miaka ya uzima, na amani“.

Kwa jumla, unapozishika sheria na amri alizozitoa Bwana maishani mwako, huo ndio udhihirisho wa upendo wako kwa Mungu. Kila unapoongeza bidii ya kumtii na kumheshimu Mungu, ukakaza kumpenda, anakushibisha siku nyingi.
Kutokana na imani yako na matendo yako mbele ya Mungu, wewe ndiye unayeweza kumwambia Bwana, hii miaka 100 inatosha, nimekwisha shiba maisha, nataka kurudi nyumbani. Au, miaka 70 inatosha Bwana, nimeshiba siku, nataka kurudi nikae na wewe. Wewe ndiye unayeamua wingi wa siku zako. Hivyo, amua kukaza kumpenda Bwana.
 
Vyuma vyenyewe vyapata kutu na kubadilika kuwa udongo/mavumbi

Na kila mwenye pumzi na amsifu Mungu/Allah
 
Kila kifo hupangwa utakufaje Pindi tu umezaliwa.
 
Back
Top Bottom