Utofauti kati ya kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa na akili (Mind)

Duuh basi mm nilihisi kuna kitu nimekukosea ndio maana nikasema hivo.
Kupenda sifa ni asili yetu wanadamu.. Japo hua tunajionyesha hatupendi. But no one is immune to flattery
Ujanikosea na hujawahi kunikosea, tupo humu kufurahi Da'vinci!
Cheers🥂
 
MATE;
Previous I wrote a topic centered on Illusion projection and I discussed a bit about how the brain process and encode memory, So this Topic will be serving as a stand-alone sequel of that Topic. Will be focusing on memory stored in brain and Soul respectively.

Kuna hivi vitu viwili tunaweza kua tunavichanganya pindi tunapokua tunataka kuvitumia, vitu hivyo ni kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Akili (Mind). Sababu ni kwamba tunachanganya tofauti ya ubongo na akili. Ubongo ni mfumo endeshi (operating System upande wa Hardware yaani physical body) wa mwili wa binaadamu ambao umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Ubongo wa mbele, wa kati na wa mwisho….. Roho (Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind, Intellect na Impression, tunaweza kusema soul ni mfumo endeshi wa mwanadamu ambao unashughulikia mambo ya kiroho na mazingira/Nature (operating system inayoongoza upande wa Software katika mwili wa mwanadamu). Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasa kwenye kutambua lipi baya na lipi jema.

Memory ni kisehemu katika ubongo ambapo taarifa (data au information) zinachambuliwa, zinahifadhiwa na kutolewa pindi zinapohitajika. Lakini pia Memory/kumbukumbu ni uwezo wa kukumbuka mambo ya zamani kama vile tabia/habits, uzoefu/experience, maarifa/skills, hisia, facts nk. Ubongo na Akili vyote vinatumika katika kuhifadhi kumbukumbu lakini zimetofautiani katika utendaji kazi, hivyo hapa tutaangali jinsi ubongo unavyokusanya taarifa na kuzihifadhi pia na akili jinsi ikusanyavyo.

Taarifa zinazotunzwa na Ubongo(Brain)

Katika ubongo wa mwanadamu sehemu inayohusika kuhifadhi kumbukumbu inaitwa Hippocampus ambapo kama sijasahau inapatikana katika ubongo wa kati, Ubongo wa mwanadamu hukusanya taarifa(data) mbalimbali kwa kupitia milango mitano ya fahamu ambayo ni Pua (Taarifa za harufu), Ulimi (radha), Macho(taarifa za picha), Masikio (taarifa za sauti), na Ngozi (taarifa kuhisi/sense). Kumbukumbu za mwanadamu zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni Kumbukumbu ya muda mfupi (short-term memory) hii utunzwa kwa muda mfupi sana kichwani yaweza kua sekunde,saa au siku na hutokea labda pindi umepishana na mtu barabarana kadri unavyotembea utasahau kama ulikutana na mtu huyo au ukiwa unasoma namba labda za simu baada ya muda utazisahau na Kumbukumbu ya muda mrefu (Long-term memory) hii hutokea pindi kitu ulikiona mara kwa mara au mlitumia muda mrefu kua pamoja hata kwa nusu saa.

Chukulia kwamba ubongo ni CPU ya computer na Flash/Hard Disk yako ni mlango wa fahamu, CPU haina chochote ndani tofauti na sehemu ya kuhifadhi computer ambayo inaitwa Cache Memory hivyo basi unapoweka flash kwenye computer na kufungua vile vitu vilivyomo ndani ya Flash CPU itaviona ba kuvifungua kwenye kioo chako cha computer, lakini pia vile vitu ulivyofungua hua vinatunzwa ndani ya CPU katika eneo hilo liitwalo Cache Memory ili pindi utakapotaka kufungua kitu ulichokifungua muda uliopita computer isichukue muda mrefu lakini jinsi unavyokaa muda mrefu bila kufungua kile kitu ndio Cache memory inakipoteza taratibu.

Sasa kama ilivyo CPU ubongo pia hua haukasanyi data bali huletewa data kwa kutumia milango hiyo ya fahamu niliyoitaja na kuzifanyia (executing data), mfano kama macho yalimuona mtu Fulani sehemu falani mkaongea na kuondoka ubongo wako kupitia macho utachuku data kuhusu mtu huyo kama vile urefu wake, unene,rangi yake,jinsi alivyovaa nk nk piakupitia masikio ubongo utachukua sauti yake, mambo mliyoongea, kama kapaka mafuta Fulani basi ubongo kupitia mapua yako utachukua data hizo kuhusu harufu na kuzihifadhi kwenye Hippocampus.

Blending in….

Kwa siku moja ubongo huhifadhi mabilioni ya taarifa kichwani so kama ulimuona mtu sehemu mkaongea kidogo mkaachana kadri ya muda unavyoenda Folder lililotunza taarifa zake kichwani linazidi kua mbaaaali zaidi kabisa Sasa ikitokea siku umemuona tena Yule mtu labda baada ya miaka kumi ubongo kupitia macho,masikio na mapua utachukua taarifa ya picha ya mwili mzima, sauti yake nk kisha inafananisha/Matching/inaScan vitu hivyo kule kwenye Hippocampus ili kuona kama kuna taarifa zinazomuhusu mtu huyo baada ya kuScan itakuletea machaguo/suggestion kadha zilizofanana na taarifa za mtu huyo sasa hapo utaanza kuchukua zile taarifa za machaguo uliyoyaaona ndani ya kichwa na tarifa za huyo mtu aliyopo mbele yako ndio utaanza kusema sasa hivi wewe sio Fulani, wewe au ni Fulani hapo ubongo unakua unapekua mafaili chapchap ili kupata matokeo mazuri sasa kama Yule mtu anakukumbuka akikuambia “hunikumbuki ni mimi Fulani tulikutana sehemu Fulani mwaka Fulani” ubongo utayachukua hayo maneno na kuyaScan na kupata folder zima la mtu huyo nawe ndio utajikuta unasema aaahaaa ni wewe ilikua hivi na hivi..
Hivyo basi kumbukumbu zote zinazohifadhiwa na ubongo ni kwa ajli ya kumuwezesha mwanadamu kuyakabili mazingira yake na vyote vinavyomzunguka .



Kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Akili (Mind)

Roho
(Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind/Akili, Intellect na Impression.Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasakwenye kutambua lipi baya na lipi zuri ,Mind imegawanyika katika pande tatu ambazo ni Conscious mind, Unconscious mind na Subconscious Mind …..Subconcious Mind hii ndio sehemu kuu ya Roho (Soul) ambayo kazi yake ni kurekodi shughuli zetu zakila siku ziwe za kimwili au kiroho. Huku juu tumeona jinsi Ubongo unavyokusanya taarifa kupitia milango ya fahamu na kuzihifadhi kwa ajili ya matumizi ya baadae…Akili pia (subconscious mind) hukusanya na kutunza kila taarifa sema kumbukumbu zinazotunzwa na akili huhifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya kiroho.



BIOS (Basic Input/Output system) hiki ni kifaa kidogo ambacho hua kimepachikwa kwenye motherboard ya Computer, kinabeba na kuhifadhi taarifa za Computer husika kama vile jina la computer nk lakini pia kazi yake ni inaongoza mzunguko wa data kati ya Operating system na baadhi ya vifaa vingine vilivyounganishwa kama vile Video Adapter,Hard disk , Keyboard,mouse nk Bila hii chip huwezi kuwasha computer. Sasa basi Soul ni kama Bios chip ya mwanadamu, mwanadamu bila roho si mwanadamu maana Subconscious Mind ndio imebeba taarifa zake zote kama vile wapi alipotoka, wapi alipo, wapi anaenda, vitu upendavyo, hisia, tabia, vitu unavyofahamu kila anachotenda mwanadamu iwe kwa kuwaza,kuongea,kuona,kunusa,kuhifadhi Subconscious Mind hurekodi na kuhifadhi nk nk. Subconscious Mind pia inauwezo wa kuingia kwenye ubongo na kuchukua taarifa/kumbukumbu zote zilizopo humo na kuzihifadhi ila ubongo hauwezi kuingia kwenye Subconscious Mind na kuchukua taarifa.



Kila kilichorekodiwa na kuhifadhiwa kwenye Subconscious Mind huja kutimika katika maisha ya mwanadamu, kila unachokiwaza,kuongea au kutenda sana basi Subconscious Mind huwasiliana na Nature kisha itakua inakulete yale inayoyaona kwako mara nyingi. Kwa mfano ukiwa unawaza kwa muda mrefu kwamba kitu Fulani kitakutokea basi Subconscious Mind inawasiliana na nature kwamba mtu huyu anahitaji na kupenda kitu Fulani basi nature itakuletea kitu hicho ndio maana unashauriwa kujiwazia mambo mazuri tu, na kama hupendi vitu Fulani vikutokee basi usijaribu kukitenda kitu hicho maana nature itakua inakuletea kitu hicho mara kwa mara kwakua Subconscious Mind inakua imesharekodi kwamba unapenda kitu hicho. Ukifa Mungu hana haja na Mwili wako anachukua tu Roho yako maana humo ndio kuna kila taarifa.

Akili na ubongo vyote vinahifadhi kumbukumbu ila akili ikihifadhi kitu basi hakipotei daima lakini ubongo hua unafuta baadhi ya kumbukumbu kama nilivyoeleza, akili inaweza kuchukua taarifa za ubongo ila ubongo hauwezi, akili inaunganisha ubongo,mwili, mazingira/nature na mambo ya kiroho. Kama ubongo ni hardware basi akili ni Operating System.

Alamsiki…..

Da’Vinci

-Excelsior​
Mkuu nimesoma thread yako hii but ningetamani sana uiwlezee bila kuhusisha computer ubezi zaidi kwenye psychology,maana muundo wa computer umeiga muundo wa mwanadamu kwa mfumo wa (IPOS) input, process, output,storage ndio maana Bado wanasayansi wanaumiza vichwa kwa robotics kama vile engineer Hanson robotics alivyounda Akina Sofia na little Sofia Ili waweze kuwaza na kung'amua kama binadamu ila Bado,so niombe ureflect zaidi kwenye saikolojia ya akili na ubongo wa mwanadamu
 
Mkuu nimesoma thread yako hii but ningetamani sana uiwlezee bila kuhusisha computer ubezi zaidi kwenye psychology,maana muundo wa computer umeiga muundo wa mwanadamu kwa mfumo wa (IPOS) input, process, output,storage ndio maana Bado wanasayansi wanaumiza vichwa kwa robotics kama vile engineer Hanson robotics alivyounda Akina Sofia na little Sofia Ili waweze kuwaza na kung'amua kama binadamu ila Bado,so niombe ureflect zaidi kwenye saikolojia ya akili na ubongo wa mwanadamu
Mkuu ulishawahi kusoma mada yangu ya Artificial intelligence??
 
Nipe dawa sasa
Mimi mwenyewe ni mkimya sijui kuongea, hadi mtu nimzoee sanaaaaa
Ila nikiingia humu naenjoy
Sio dhambi kua mkimya hivyo ulivyo ni sawa

Jitahidi kufanya vitu unavyovipenda ili uwe mtu unayefurahi muda mwingi
 
Mimi mwenyewe ni mkimya sijui kuongea, hadi mtu nimzoee sanaaaaa
Ila nikiingia humu naenjoy
Sio dhambi kua mkimya hivyo ulivyo ni sawa

Jitahidi kufanya vitu unavyovipenda ili uwe mtu unayefurahi muda mwingi
Napenda kuandika, napenda kuangalia muvis. Muda wa kufanya hivyo vitu sina, ndio nabaki sasa kwenye total loneliness. Msaada wako
 
Napenda kuandika, napenda kuangalia muvis. Muda wa kufanya hivyo vitu sina, ndio nabaki sasa kwenye total loneliness. Msaada wako
Muvis❌
Moviesâś…
Ukitoka kazini ukiwa peke yako huwa unafanya vitu gani?
 
La hasha mkuu!
Soma kwanza huu uzi hafu tutarudi kwenye comment yako
 
Muvis❌
Moviesâś…
Umekua bibi kifimbo cheza wa gazeti la sani?
Ukitoka kazini ukiwa peke yako huwa unafanya vitu gani?
Napita pita jf. Nikisema niangalie movies nasinzia sitoboi hata dk 20
FB_IMG_17139744168403376.jpg
 
Soma kwanza huu uzi hafu tutarudi kwenye comment yako
Sawa Wacha nipite apo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom