Tupeane mbinu za kuweza kujidhibiti na uraibu wa soda

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
75,013
156,449
Watu wengi sana wanapambana na uraibu wa sigara, pombe na madawa ya kulevya. Lakini wakishaushinda uraibu huo hujikuta wameangukia kwenye uraibu mwingine hatari lakini usio ongelewa. Uraibu huo sio mwingine ila unywaji wa soda, hasa mazingira yenye joto kama mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga , Lindi na Mtwara

Soda hasa za Pepsi na Coca Cola (baridiiiiii) hushuka vizuri sana kipindi cha joto kali. Ubaridi, usukari na ladha ya kupurudisha huleta msisimko fulani amazing mwilini. Msisimko huu ukikunogea unakufanya uwe teja wa soda.

Wengi walioacha kunywa pombe hujikuta wanaangukia kwenye urahibu huu na kuwa mateja kabisa.

Tupeane mbinu mbalimbali za kuushinda urahibu wa soda, maana rafiki yangu baada ya kuacha pombe sasa kwa siku ni lazima agonge Pepsi baridi tatu, anasema yeye bila Pepsi siku haijaisha.
 
Kuna mama mtu mzima aliwahi niambia akiwa barabarani yaani ni kosa akiliona bango kubwa la yule msanii ameshikilia ile soda basi na yeye hapo hapo hamu ya kuinywa huja kwa kasi na kwa kweli huwa Hana ujanja tena kifuatacho ni kuinywa tuu ilhali hospital wameshaufi asinywe soda.

Ni ngumu ngumu sana kuacha. Mimi kosa nikienda tuu yale mazingira ninapoendaga kutulia dah nitainywa tu.

Kungekuwa na dawa ningeitumia kuacha matumizi ya soda.
 
1)Akikisha chakula chako kikuu kiwe ugali,hapo soda kwisha habari yake. ugali ni adui namba moja wa kinywaji cha soda

2) asilimia 80% ya kiu au hamu ya soda tunayo pata siyo ya kweli ...kama ukipata kiu au hamu ya soda basi kabla ya kunywa soda kunywa maji kwanza kisha ukiona hamu ya soda bado ipo ndipo nunua soda unywe, very simple and perfect method it work 100%
 
Kunywa tu MAJI mengi na ufanye Zoezi LA kutoa jasho. MI nimejitahidi kuacha pepsiiiii nimeshindwa. Nimejiamulia tu liwalo na liwe. So MAJI lazima na Zoezi ili kupunguza hizo sumu.
 
Back
Top Bottom